Unyanyasaji wa kijinsia

Jkerry

New Member
Aug 31, 2022
2
0
Unyanyasaji ni nini?, Kwa nini mtu ananyanyasika? Kwa nini mtu anapo nyanyasika achukui atua??, Ni maswali kila mtu anauliza pale anapo sikia unyanyasaji, kuna mda jamii tunazo ishi nazo ndizo sababu ya unyanyasaji , kwasababu nyanyasaji aupo ndani ya familia tu , jamii pia uchangia unyanyasaji wa kijinsia kwa wanaume na wanawake.

Unyanyasaji ni kitendo kinacho athiri binadamu ki saikolojia , inaweza kuwa kwa matendo au maneno, katika jamii ya sasa wanaelewa unyanyasaji ni vile vitendo vya kikatili , bila kusahau ata wale wanao semwa vibaya ni unyanyasaji wa kijinsia kwasababu ina muathiri huyo mtu.

Kumcheka mtu wa jinsia fulani kuhusu maumbile au jinsi alivyo ni aina mojawapo ya ukatili wa kijinsia, kwani watu upoteza tumaini kwa jinsi walivyo, Mfano kipindi tupo shule ya sekondari tulikua tunasoma na binti alikua kabarikiwa kwa umbo lakini sura kila mtu alikua akimcheka, ubaya si wanafunzi tu adi kunakipind mwalimu alimwambia "kwaiyo sura soma sana " kile kitendo kilikua kikimuumia sana binti yule , nlikua ni mtu nnae penda kuzungumza nae.

Katika mazungumzo yetu , alidai ata ndungu walimtenga japo si sababu ya sura tu ila , sura nayo ilichangia , kunakipindi ata Mama yake mzazi alimdhiaki kwa jinsi alivyo , kitendo iki kili mfanya asiwe mtu huru katika maisha yake , ilifika kipindi yule binti alikuwa anafanya jaribio la kutoa uhai wake , ni simanzi alijihisi yeye si binadamu kama binadamu wengine, kwani ata uwezo wa darasani ulikua afifu.

Kipaji kilimpita kushoto kwani akuweza tambua anakipaji gani. Wakaka wa shule wakaona kwakua yule yuko tofauti wakaanza kumjaza ili ajiingize katika mahusiano, binti kwakua anajiona yeye ndivyo sivyo kila kijana alipita nae bila kujali , akapewa jina la chawote nyimbo akatungiwa.

Maisha yake yakawa ni ya ivyo akaona kidogo yanampa furaha wanavyo mdanganya aliona ni bora kuliko kulia kila siku, mabinti tukamrudia kumshauli lakini wapi , tabia ikakomaa , bahati mbaya alipata gonjwa la zinaa (kaswende)aliangaika maana ata ajandogo ilitoka kwa maumivu, walimu walijitahid kumtibia lakn tulikua mwisho tunamaliza kidato cha nne , na apo atukujua kilicho endelea kuhusu yeye taarifa ya mwisho tulipata kuwa kapatwa na ugonjwa wa akili , sababu ya mawazo, mwaka jana alipoteza maisha , Nani mwenye kosa?

Ni jamii tuliyo mzunguka tuliaribu maisha yake atukumpa thamani ya kibinadamu.jamii tuliusika katika kila lililo mkuta na ni kwasababu tulikua atuna uelewa , elimu yetu aikutufunza kuhusu unyanyasaji , tukajikuta tume mnyanyasa binti yule bila kutambua.

Lakini kwa mtu ambae ana utambuzi wa unyanyasaji anaweza sema binti yule alifanyiwa uchawi si kila kichaa ni mambo ya ushirikina .

Tazameni jamii na maisha yaliyo mzunguka huyo binadamu mtaweza gundua mambo tofauti na imani zetu.

Unyanyasaji umekua gumzo na tatizo katika jamii yetu , ukatili wa kimatendo na maneno umekubuu kwa wakubwa na wadogo , kila muktadha unyanyasaji unajitokeza . kuna ule msemo ulianzishwa kuwa haki sawa kwa wote lakini usawa upo katik ngozi na sio ndani , bado atujafika atua ya kuweka usawa kati ya mwanamke na mwanaume unyanyasaji bado unatawala , watu wanashindwa kupaza sauti kupiga yowe kwa wanayo fanyiwa na kuyaona nitoe ka mfano kafupi .

Kuna binti alibakwa na jirani wa karibu kwa wengi mnawaita (family friend) binti alitoka kuoga kama tunavyo faham mabafu ya watanzania wengi tinatumia ya nje , alipo rudi ndani alikuta kijana kakaa sebreni, binti alimuulizakijana kafuata nini ndipo kijana akamwambia yeye Mama yake hayupo , amekuja kula .

Binti wazazi walikua nao awapo kwaiyo akamuomba kijana asubiri avae atampakulia chakul , binti alielekea chumbani kufika kwakua akuzoea kufunga mlango na komeo aliendelea kuvaa nguo za ndani ndipo alipo vamiwa na kijana yule na kubakwa .Binti baada ya kitendo alimpa taarifa Mama yake , ilibidi wazazi wa rudi na kumpeleka mtoto polisi aweze kupata cheti cha matibabu ila wale ma polisi walimcheka binti na kusema alitaka mwenyewe, Baba wa binti alivyo panda juu ndio wakakubali kumpa binti kile cheti hivyo hivyo alivyo fika hospitali kwanza alipimwa ukeni bikra kama bado ipo na watu wa3 tofauti na daktari anae takiwa , na kuna muda binti anasema wale watu wali ongea chini chini , kuwa alitaka mwenyewe .kikweli binti alipitia unyanyasaji mkubwa . na ilimuathili .japo haki yake mwisho alipata.

Watu wanaficha unyanyasaji wanao pitia kwasababu ya jamii inayo wazunguka mtu kapigwa na mkewake, jamii inamkebehi wakati ni unyanyasaji pia anaitaji msahada ila inageuka kua kituko , binti au kijana anabakwa ni kicheko kwa wanajamii badala ya kumtetea na kumuonea huruma pia kumpa msahada ata kumfariji , kila tukio kwa watu imekua ni kichekesho na kubakia kusema " ingekua mimi" , ingekua nini ?? Kila mtu kuna jambo analo lipitia na kwamwengine anaona ni rahisi . ingekua yako ebu jaribu kutatua lile lako ambalo wengine wanasema ingekua wao .

Tufike mahala jamii tushikamane uwenda ukatili utateketea kwasababu ukatili na nyanyasaji vimekuja kwa kasi , sasa hivi ndio akuna pakupumulia , matukio ni mengi na ya kusikitisha na kutisha . tuungane tuteketeze unyanyasaji . unyanyasaji unaweza kumpata mtu yeyote hivyo tushikamane kwanza kama wana wa familia moja kesho na keshokutwa isiwe kwako au kwa familia akuna aijuae kesho . kufarijiana na kuteteana ndo kesho yetu inapo ponea .pale mtu anapolia simama tazama unga mkono panapo takiwa si kwasababu tatizo ni la familia yake atakoma mwenyewe, akuna ajuae kesho wote tupo katika nsito fahamu ya kesho wala kesho kutwa, watu wana kufa , wana pata magonjwa kwasababu ya unyanyasaji .

Watu wanao nyanyasika kijinsia ni muda wa kuinuka na kupaza sauti kabla jambo baya zaidi aijakukuta kuogopa jamii nisawasawa na kuficha kisicho fichika maana utaumbuka kwa janga kubwa, kila mtu atambue haki zake pale anapo nyanyasika aweze kupaza sauti.

Kunawatu wana ofia kuvunja ndoa na kubaki bila mume , atakama unawatoto unaogopa wata kuwa miongoni ya mtetemeko utakao tokea , wewe paza sauti angalia usipo paza sauti .ukafia katika mikono isiyo salama , je watoto unahis watakuwa salama?

Binti unae nyanyasika katika familia ukiwa na hofu familia itavurugika je huyo anae fanya ukatili anatambua umuhimu wa iyo familia?

Amkeni piganeni , usipo jisimamia nani ata kusimamia , usipo simama kwaajili ya anae teseka na unamuona unafikiri kesho yupo wa kukufuta chozi utakapo anguka na wewe?? Tusimame wote kama watoto wa baba mmoja .

Wapo wazazi / ndugu watoto wanapo fanyiwa unyanyasaji wao ukimbilia kupata hongo na kumuachia huru mtuumiwa kwa nini mtoto anyimwe haki zake kisa tamaa za watu wachache?

Ni kuingilia kati haki ya mtu kwa maslai binafsi , japo serikali imeweka sheria kali lakina watu bado , na bado jamii inalalama haki azitendeki, sheria gani mnataka isimame wakati kuna miongoni mwenu mnazilaza na kuzidumaza, ubakaji na ulawiti ni changamoto kubwa sana, ila wangapi wameweza kufika mahakamani?

Ni asilimia chache sana wengine wamekula hongo, wamezima mshumaa kwa mkono bila kujali walie mshikisha , anaumia mara mbili. Uchungu unakuwa mara dufu na afya ya akili ina dhohofika , huku wanyang'anyi wakiburudika na kufaidika katika janga la ndugu. Ni unyang'anyi wa kikatili sana.

Wapo ndugu na wazazi wanao linda jina la familia na kupoteza haki za mabinti zao au vijana wao . kwa nini kuficha sura kamili ya vazi lililopo? Kwa nini mna gandamiza haki za wanafamilia siku zote , viza likipasuka ata ufunike na pafyumu litanuka tu ata ubani hauto saidia kitu.

Pale serikali inapo fanya kazi yake inapaswa na wanajamii kujiwajibisha kusaidia serikali pia kwa kutoa elimu ni muhimu sana wale wanao fahamu kuhusu.unyanyasaji wa kijinsia kutaarifu wengine wakapata maharifa ni jambo la msingi na maana kwakua si kila mtu anafahamu kuhusu unyanyasaji wa kijinsia.

Wapo watu awafahamu kabisa kuhusu unyanyasaji kuna kipindi Elimu zilikua zikitolewa mtaani maeneo, ya kigogo baada ya elimu kuwafikia watu ndipo matatizo mbalimbali yakaibuka , watu walikua awatambui kitu kinacho endelea katika jamii katika baadhi ya nyumba ni unyanyasaji , hapo ndipo watu waligundua kunawazazi wanao waingilia watoto wao na wengine kuwa nyanganya haki wanafamilia.

Endapo watu wataibuka kutetea na kupinga unyanyasaji basi ni wazi kabisa matatizo ya afya ya akili nchini yatapungua, vifo pia vitapungua , magonjwa yatapungua ni jamii nzima kuamua nini kinatakiwa na kuanza kupinga unyanyasaji na kuweka usawa katika jamii ili jamii istawi na maendeleo yawepo katika jamii zetu.

Watanzania wenzangu kuungana na kushikamana katika swala zima la kupinga ukatili utasaidia kuteketeza unyanyasaji wa kijinsia na pia kuheshimisha kila jinsia. Vile vile kupunguza matatizo yanayo sababishwa na unyanyasaji wa kijinsia.
 
Back
Top Bottom