Nashukuru Mungu Tanzania nimeimaliza

Huyu jamaa inaonekana hana kazi ya kufanya leo ameona ngoja apoteze mda na wajinga wa jf!

Hamna mtu yoyote anaeifahamu dunia zaidi ya JK!!
 
What question is this? First of all he should tell us what he knows about every place in this country before he/she brags nobody else knows the country than him/her. Use your brain properly, if you have any, and you will be able to ask relevant questions.
Mkuu hebu kiswahilisha basi..maana uzi wenyewe unahusu Tanzania na Watanzania,ambao kwa pamoja tunaunganishwa na Swahili..Can you please write Swahili
 
Kwa wenyeji wa Ukara hata mie naweza kukumegea japo hukuniuliza mimi: kwanza ni kisiwa ambacho kiko ndani ya Kisiwa cha Ukewere, ni tarafa ya Ukara, ina vivutio vya asili mfano kuna jiwe ambalo wazee wakiliimbia nyimbo wanazozijua wao linacheza lakini wewe mtu mtu hata ungeimba hadi miaka 100 halichezi! wenyeji wa kule wanapenda mchezo wa kupiganisha madume ya ng'ombe kiasi kwamba dume lako likishinda ni sawa na Yanga au Simba wakishinda au kushindwa, pia akina dada wa Ukara kwa utaratibu wao ikifika usiku ndio wanaruhusiwa na wazazi wao kwenda kutembea, mchana marufuku kuzurura ni KAZI TU. Vile vile Ukara kuna wazee wanafuga Mamba, kiasi kwamba hata wakiwa ziwani wanajua huyu ni mamba wa mzee Fulani kama wewe unavyoweza kujua huyu ni ng'ombe wa Fulani, sasa hao mamba huwa wanawatumia kwa mambo ya kiutamaduni! kwa mfano wewe kijana unaweza kumpa msichana wa kikara mimba halafu ukajidai kumtosa, kinachofanyika anatumwa mamba kuja kukuchukua huko uliko hata kama ni Mbeya lazima siku hiyo utajisogeza tu karibu na ziwa au bwawa na huyo mamba anakumeza atakupeleka hadi kwa mzazi wa msichana anakutapika halafu hapo utajibu mashitaka yako ya uharibifu wa binti yao:

Very very interesting.....!!!

Haya yapo kweli Tanzania? Mbona Nchi yetu inashika mkia kwenye suala zima la Utalii?

Let me assume, hapa umetupiga kamba mkuu?

BACK TANGANYIKA
 
Si kitu rahisi,Kwa umri wangu wa miaka sitini na...++ namshukuru mwenyezi Mungu saana,manake nchi hii nimejaaliwa kukaa angalau kila wilaya ya Tanzania Bara kwa kipindi kirefu.

Nina uhakika hakuna Mtanzania yeyote anayeifahamu nchii hii vizuri kuliko mimi.

Hivyo basi namkaribisheni kwa anayehitaji ushauri kuhusu sehemu yeyote ya nchi ya Tanzania.

Namshukuruni sana.
Natafuta mke wa kuoa. Nisaidie nichague mkoa gani. Wilaya gani umeona afadhari. Na kabila gani
 
Si kitu rahisi,Kwa umri wangu wa miaka sitini na...++ namshukuru mwenyezi Mungu saana,manake nchi hii nimejaaliwa kukaa angalau kila wilaya ya Tanzania Bara kwa kipindi kirefu.

Nina uhakika hakuna Mtanzania yeyote anayeifahamu nchii hii vizuri kuliko mimi.

Hivyo basi namkaribisheni kwa anayehitaji ushauri kuhusu sehemu yeyote ya nchi ya Tanzania.

Namshukuruni sana.

Nadhani jambo la maana hapo mkuu ni kwamba kunafaida gani ya wewe kuweza kukaa wilaya zote za tanzania bara? je kuna mchango wowote ulioutoa kwa watanzania kote ulikopita au ndiyo zile story za tanzania imekufanyia nini na wala si wewe umeifanyia nini tanzania? Ni tafakari tu!
 
What question is this? First of all he should tell us what he knows about every place in this country before he/she brags nobody else knows the country than him/her. Use your brain properly, if you have any, and you will be able to ask relevant questions.
kakwambia umuulize sehemu yoyote uanyotaka kujua unaleta bla bla kabla hujampinga muulize kwanza akishindwsa owte tutajua hajui.
 
Ni waungwana sana, pia shukuru Mungu maeneo ya huko kuna fursa nyingi hasa kilimo na ufugaji.
Wenyeji ni wachapa kazi na pia hupenda kujiburudisha na kinywaji cha nafaka baada ya kazi.
Baadhi ya watu watakutisha kuusu imani giza..ipo lakini mpaka umuanze mtu.
Pia wenyeji wana ngoma zao za tofauti na sehemu nyingine,hutumia chungu.... kina geuzwa upside down halafu kigoda cha kukalia hutumiwa ku scratch na kutoa mlio wa kipekee....
ni raha sana.
Hiyo ngoma kutumia kigoda na kusugua kwenye mtungi huitwa vingwengwe
 
Very very interesting.....!!!

Haya yapo kweli Tanzania? Mbona Nchi yetu inashika mkia kwenye suala zima la Utalii?

Let me assume, hapa umetupiga kamba mkuu?

BACK TANGANYIKA
Sio kamba respect wa boda, hata kipindi Mama Mongela alivyokuwa mbunge alishawahi kusema bungeni kuwa kuna hicho kivutio cha hilo jiwe kiasi kwamba serikali ikikitangaza tunaweza kupata watalii na kuongeza pato la Tanzania
 
.
Nzalendo kwa tanzania ni sehem gan uliihusudu kuishi kutokana na wenyeji kuwa wakarimu ma tabia nchi kukupendeza zaidi je unasehemu kama hio katika mlolongo wa maisha yako ambayo ungependelea kurudi hata sasa kutokana na fursa zilizopo hapo pamoja n utu wa wenyeji?
 
Mkuu vipi kuhusu Tanganyikamasagati je nako ulishafika?
Wenyeji wake ni kabila gani?
Vipi kuhusu maendeleo yao?
Fursa za huko ni zipi?
 
Sio kamba respect wa boda, hata kipindi Mama Mongela alivyokuwa mbunge alishawahi kusema bungeni kuwa kuna hicho kivutio cha hilo jiwe kiasi kwamba serikali ikikitangaza tunaweza kupata watalii na kuongeza pato la Tanzania
Sio kamba respect wa boda, hata kipindi Mama Mongela alivyokuwa mbunge alishawahi kusema bungeni kuwa kuna hicho kivutio cha hilo jiwe kiasi kwamba serikali ikikitangaza tunaweza kupata watalii na kuongeza pato la Tanzania

Yaaah, hilo sipingi mkuu...

Hapo kwenye kutumiwa Mamba anitumbue nikitundika drip kwa kabinti fulani.. hapo hapooo

BACK TANGANYIKA
 
Yaaah, hilo sipingi mkuu...

Hapo kwenye kutumiwa Mamba anitumbue nikitutinda drip kwa kabinti fulani.. hapo hapooo

BACK TANGANYIKA
respect wa boda hapo ni kweli, unajua hapa Tanzania kuna sehemu watu wana mambo ambayo ukisikia unaona kama hayapo! nakushauri hapo ulipo uliza mtu yeyote anayetoka Ukerewe au hata mikoa jirani ya Mara wakuambia kuhusu hilo la Mamba ni hatari aiseee, tena siku ukimu approach mdada akakuambia ni mzaliwa wa tarafa ya Ukara, wilaya ya Ukerewe mkoa wa Mwanza, kimbia kama vile mtoto amemuona Dr. anataka kumchoma sindano
 
Mkuu naomba kujua kuhusu wilaya ya kilombero na wakazi wake ni makabila gan
Kuhusu kabila wanaitwa Wavidunda...
Kilombero wali samaki ni kama ndizi senene kwa washomire na wanyambo.
Kilombero vyakula vipo vya kutosha,miwa inastawi hata ndizi zapatikana.
Huku nilikuwa miaka ya 80 mwanzoni nyama pori zilikuwa maarufu sana kwa sasa sina hakika kama bado zipo.
 
Inawezekana kweli, ila watu wengine waajabu sana, uliza sehemu unayoijua ambayo unahis kwa namna yoyote labda hawez ijua kirahis then akikosea bas mkosoe nakusema bas haijui Tz kama anavodai, sio unakurupuka2 hata hujauliza ki2 chochote unakosoa kosoa2, kosoa hata kwa hoja basi.
 
Back
Top Bottom