Nashukuru Mungu Tanzania nimeimaliza

Nashukuru Mungu Tanzania nimeimaliza

Mkuu, kutokana na majukum yangu ya kikandarasi mimi pia nimezunguka sana nchi hii yote pamoja na majiran zake..
Sema ckua mtu wa kukaa muda mrefu kama wewe (Now I am 25 yrs).

Sasa baba (au we ni mama??) nimabie maeneno haya chini yako wilaya gani mkoa gani:

Mshikamano, Ndemdezi, Bushushu, Mwasele na Lubaga.

#Chief Eng.
Yaani wewe unamtajia maeneo ya mjini atashindwa kuyafahamu wakati amekwambia keshatembelea wilaya zote? Ungemwambia ndani ndani huko, wilaya kama Chemba, Kakonko, Buhigwe n.k
 
Nzalendo uko Vizuri sana. Kuhusu hiyo ngoma ya Wafipa ya kugeuza chungu na kukiparaza kwa kigoda inaitwa KIZANGALA. Kuhusu Nkasi aliyepelekwa huko ukifika upunguze dharau kwa wenyeji, usijependekeze kwa binti zao maana atajitangazia ndoa ndani ya mwezi tuuu tangu umlale. Usiwe mlafi wa vyeo pia
na kinu kinaitwa kigwegwe,pale halmashauri wenye vyeti feki ni wengi.kaa kimya usiwaumbue
 
Kwangu mimi huu uzi ni shule tosha. Siui kwa nini wengi wetu tunapenda kuwa negative. Ask question ujue ambalo hujui. Alienda kufanya nini..its non of your business. wewe uliza unachotaka kujua. kama hana jibu atakwambia.

Hongera Mkuu. I am impressed.
 
Si kosa lako ni ufahamu wako.
Kama ukijiona panzi hakika wewe utakuwa panzi.Ni aina ya uandishi wa kuvuta umakini wa msomaji iwe kwa jema au kwa baya.
Relaaaaxxxx
nzalendo asante sana mkuu wa thread hii. Hizi ndio thread ninazozitamani hapa JF kwani mtu unajifunza na kufurahia mengi. Hongera sana na usikatishwe tamaa na baadhi wanaoandika na ku-challenge huky hawajui lolote. Unajua tena shule za siku hizi zinakuwa kama zinasomesha ujinga. Endelea kutupa burudani!
 
kakwambia umuulize sehemu yoyote uanyotaka kujua unaleta bla bla kabla hujampinga muulize kwanza akishindwsa owte tutajua hajui.
Unajua maana ya bla bla bls au una kipaji cha kuropoka?
 
Unaweza kuijua nchii kuliko mzee wa msoga? ? ! ! mpaka useme hakuna anayeijua zaidi yako? kwanza wewe ndo wakwanza kuifanya hiyo kazi iliyofanya uzunge sehemu za tanzania? ?
Umemaind kinoma

Uliza swali mkuuu
 
Ok sawa mkuu ni kweli kuhusu vyakula ila kabila ni wandamba na wapogoro kwa sana!!!! Marbury xn aise ila nyama pori cku hiz hakuna mkuu nzalendo
 
Si kitu rahisi,Kwa umri wangu wa miaka sitini na...++ namshukuru mwenyezi Mungu saana,manake nchi hii nimejaaliwa kukaa angalau kila wilaya ya Tanzania Bara kwa kipindi kirefu.

Nina uhakika hakuna Mtanzania yeyote anayeifahamu nchii hii vizuri kuliko mimi.

Hivyo basi namkaribisheni kwa anayehitaji ushauri kuhusu sehemu yeyote ya nchi ya Tanzania.

Namshukuruni sana.
Hongera kwa kutumikia wa Tz wote na kwa kustaafu(nahisi)! Furahia maisha yako ya pensheni vizuri!
 
naomba maelezo kuhusu mji wa VWAWA mkoa mpya wa songwe, tabia za wakaz wa pale, hal ya hewa n.k
 
Mkuu shukrani kwa kutupa habari za wadada wa kikara, kwakweli ntafanya juu chini nsiingie anga zao, maana sitaki kabisa kumezwa na mamba na kusafirishwa kwa njia isiyojulikana na mwisho kwenda kutemwa ukweni huko ukara-ukerewe. Hakika wadada wa kikara sio watu wazuri kwa mgegedo
 
Naam hiyo sehemu ipo,kilichonivutia zaidi si uzuri wa mandhari au fahari waliyo nayo...ila ni utu wao...walikuwa hawanifahamu na mimi nilikuwa ni mgeni kabisa lakini walinikarimu mpaka nikapata hofu,chakula kwao si tatizo unakula mpaka jasho linakutoka....Nilipewa chumba nikakaa miezi miwili kabla ya kuanza kulipa kodi...sehemu hii naomba nisiitaje kwa jina lakini ni kanda ya Ziwa.Kwa wananzengo.
Asante sana
 
Naam kuna kiongozi maarufu wa nchi hii,anatokea pande hizo,kila anpoenda kusalimu halali huko hurudi mpaka Mwanza kwa ajili ya malazi.
[emoji23] [emoji23] viongozi anaogoma umafia wa nyumbani.
 
Acha ujinga wa kujisifia wewe. Eti hakuna mtanzania anayefahamu nchi hii kuliko wewe? Sasa umefanya kitu gani cha maana kama hii nchi unaifahamu kuliko mtu mwingine? Kama huna topiki ya maana nyamaza kimya. Tulia kabisa.
Hivi umejiunga jf tangu 2007 halafu unaweza kupost hivyo? Kweli?
 
Hivi umejiunga jf tangu 2007 halafu unaweza kupost hivyo? Kweli?
Mkuu sio nia yangu kufanya haya ninayoyafanya. Ninachojaribu kufanya ni kuwa "watch dog", kuwasaidia moderators katika kurekebisha tabia za baadhi ya wanachama hapa JF. Wanachama wengine wanakera sana. Wanaanzisha topiki ambazo hazina kichwa wala miguu.
 
Na hizi wilaya mpya umekaa? Bado mkuu. Endelea na zoezi?
Hizi mpya ni za sasa kwa umri wake amestaafu sasa maana kwa umri tuu ni sawa na baba yake magufuli ama kikwete. Mtu anaitumikia serikali Kwanzia miaka ya sitini huko[emoji57] [emoji57]
 
unapajua mbinga??
Mbinga napajua kuna mchaga mmoja pale stendi anaitwa Mmasi ni mpika supu mwaka 2006....07.Kipindi hicho kuna mabasi yalivuma sana yanaitwa Bambo.
Kuna udongo mwekundu,pia wanalima Kahawa kipindi napita huko kulikuwa hakuna barabara nzuri.
Nakumbuka hapa nilisafiri na tippa la Mzee Masanje kuelekea Mbamba bay...tulisafiri usiku,kwa mbaali tukaona taa nikajua kuna bonge la mji kama vile New York,Daah kuja kugundua kumbe ni wavuvi wa Ziwa nyasa.(wanavua kwa kutumia karabai).
 
Back
Top Bottom