Nashukuru Mungu Tanzania nimeimaliza

Nashukuru Mungu Tanzania nimeimaliza

Si kitu rahisi,Kwa umri wangu wa miaka sitini na...++ namshukuru mwenyezi Mungu saana,manake nchi hii nimejaaliwa kukaa angalau kila wilaya ya Tanzania Bara kwa kipindi kirefu.

Nina uhakika hakuna Mtanzania yeyote anayeifahamu nchii hii vizuri kuliko mimi.

Hivyo basi namkaribisheni kwa anayehitaji ushauri kuhusu sehemu yeyote ya nchi ya Tanzania.

Namshukuruni sana.
Kiongozi hapo kwenye redi, una uhahika na unachokisema ??
 
Acha ujinga wa kujisifia wewe. Eti hakuna mtanzania anayefahamu nchi hii kuliko wewe? Sasa umefanya kitu gani cha maana kama hii nchi unaifahamu kuliko mtu mwingine? Kama huna topiki ya maana nyamaza kimya. Tulia kabisa.
Naam hakika nastahili kuingia kwenye guiness book of records,wewe huamini hayo kama yanawezekana....Lakini tuliza preshaa relaxxxxx

Cha maana hapa ninachokifanya ni kuwaonyesha vijana fursa mbalimbali zilizopo katika nchi hii kwa uhakika zaidi..na kwamba ni vyema waelewe wanaweza kwenda popote katika nchi hii kutafuta rizki Ila tu wasivunje sheria.
Swali?
 
Hayo unajibiwa hata na mtu aliopo Pyongyang.
Uko sahihi mkuu hapa alitakiwa aulize vitu ambavyo hata uki google huvipati.
Ingawa Jomu ndio Tinde na Tinde ndio Jomu.....Sasa aulize unamfahamu mtu anaitwa Jamal pale Tinde?..nitamjibu namfahamu ni mwembamba na mara nyingi nilikuwa nakunywa nae pale kwenye duka la Mrema njia panda.
 
Ni kitu gani kinakufanya ujihisi kwamba wewe ndie uijuaye Tanzania kuluko yeyote wakati unaonekana bado kijana mbichi wapo wenye 80s na walitembea hii nchi tokea ujana.

Tupe sababu inayokufanya ujione wewe pekee tu na si mwingine yeyote.
 
Hahahaa upo sawa hapo.
 
Mkuu naomba unijulishe kuhusu tabia za wenyeji wa Ukara. Na zipi fursa za huko?
Kwa wenyeji wa Ukara hata mie naweza kukumegea japo hukuniuliza mimi: kwanza ni kisiwa ambacho kiko ndani ya Kisiwa cha Ukewere, ni tarafa ya Ukara, ina vivutio vya asili mfano kuna jiwe ambalo wazee wakiliimbia nyimbo wanazozijua wao linacheza lakini wewe mtu mtu hata ungeimba hadi miaka 100 halichezi! wenyeji wa kule wanapenda mchezo wa kupiganisha madume ya ng'ombe kiasi kwamba dume lako likishinda ni sawa na Yanga au Simba wakishinda au kushindwa, pia akina dada wa Ukara kwa utaratibu wao ikifika usiku ndio wanaruhusiwa na wazazi wao kwenda kutembea, mchana marufuku kuzurura ni KAZI TU. Vile vile Ukara kuna wazee wanafuga Mamba, kiasi kwamba hata wakiwa ziwani wanajua huyu ni mamba wa mzee Fulani kama wewe unavyoweza kujua huyu ni ng'ombe wa Fulani, sasa hao mamba huwa wanawatumia kwa mambo ya kiutamaduni! kwa mfano wewe kijana unaweza kumpa msichana wa kikara mimba halafu ukajidai kumtosa, kinachofanyika anatumwa mamba kuja kukuchukua huko uliko hata kama ni Mbeya lazima siku hiyo utajisogeza tu karibu na ziwa au bwawa na huyo mamba anakumeza atakupeleka hadi kwa mzazi wa msichana anakutapika halafu hapo utajibu mashitaka yako ya uharibifu wa binti yao:
 
Naam hakika nastahili kuingia kwenye guiness book of records,wewe huamini hayo kama yanawezekana....Lakini tuliza preshaa relaxxxxx

Cha maana hapa ninachokifanya ni kuwaonyesha vijana fursa mbalimbali zilizopo katika nchi hii kwa uhakika zaidi..na kwamba ni vyema waelewe wanaweza kwenda popote katika nchi hii kutafuta rizki Ila tu wasivunje sheria.
Swali?
Ndg. Nzalendo Mwenyeezi Mungu akubariki mema na uwe mfano bora kwa jamii....

Suali langu ni kuweka bayana yale yaliyo kukuta bila kuyategemea huko ulipo ishi:-
Wilaya/kijiji au mji gani ni mgumu (kwa ujumla) ? (maisha ya shida na utata)
wilaya/kijiji au mji gani una uhalifu/ukatili endelevu ? (ukosefu wa uvumilivu,uungwana)
Wilaya/kijiji au mji gani bado wamelala/wemeduwaa ? (juu ya rasilimali zote walizonazo)

hapo tutaweza kuanzia....
 
Ni kitu gani kinakufanya ujihisi kwamba wewe ndie uijuaye Tanzania kuluko yeyote wakati unaonekana bado kijana mbichi wapo wenye 80s na walitembea hii nchi tokea ujana.

Tupe sababu inayokufanya ujione wewe pekee tu na si mwingine yeyote.
Naam swali zuri sana mkuu.
Safari ya kuizunguka nchi hii inaanzia miaka ya hamsini katikati..Mzazi wangu alikuwa mwalimu enzi za mkoloni.
Kwa kifupi mpaka nafikisha miaka 12 nilishakaa Burka(Arusha),Mpwapwa,Mbulu,Korogwe,Pugu,Tabora,na Iringa.
...Kuanzia hapo nikapata shetani wa kupenda nchi hii.....Wakati nafanya kazi nilikwisha kanyaga kila Ardhi ya Wilaya unayoifahamu nchi hii.(kuna siku nililala kwenye nyumba aliyo lala mwalimu nyerere akiwa kwenye harakati za kutafuta uhuru.....nyumba hii ipo Ruvuma Barabara inayokwenda Namtumbo Upande wa kulia kabla hujafika njia panda ya Chengena)
 
Si kitu rahisi,Kwa umri wangu wa miaka sitini na...++ namshukuru mwenyezi Mungu saana,manake nchi hii nimejaaliwa kukaa angalau kila wilaya ya Tanzania Bara kwa kipindi kirefu.

Nina uhakika hakuna Mtanzania yeyote anayeifahamu nchii hii vizuri kuliko mimi.

Hivyo basi namkaribisheni kwa anayehitaji ushauri kuhusu sehemu yeyote ya nchi ya Tanzania.

Namshukuruni sana.
Naomba uniambie hari ya hewa ya Songea na maisha yao kwa ujumla
 
Labda aeleze alikuwa anazunguka kwa uhamisho, utafiti, biashara au kwa sababu gani ndipo tutaweza kumjaji anavyostahili. Ila kwa kweli kujinasibu hakuna anayeijua hii nchi kamq yeye ni kujidanganya.
tuambie wewe nanni anajua zaidi yake,
 
Ndg. Nzalendo Mwenyeezi Mungu akubariki mema na uwe mfano bora kwa jamii....

Suali langu ni kuweka bayana yale yaliyo kukuta bila kuyategemea huko ulipo ishi:-
Wilaya/kijiji au mji gani ni mgumu (kwa ujumla) ? (maisha ya shida na utata)
wilaya/kijiji au mji gani una uhalifu/ukatili endelevu ? (ukosefu wa uvumilivu,uungwana)
Wilaya/kijiji au mji gani bado wamelala/wemeduwaa ? (juu ya rasilimali zote walizonazo)

hapo tutaweza kuanzia....
Mkuu hili swali nitakujibu k
Naomba uniambie hari ya hewa ya Songea na maisha yao kwa ujumla
Kwanza ukifika pale mjini...kuna sehemu inaitwa Manzese A..kuna pombe fulani inatengenezwa kwa kutumia muhogo..kama sijakosea jina lake ni yamkaya...
Songea kuna baridi lakini si kali kama ya Njombe au Ludewa.Songea vyakula vinapatikana kwa unafuu ..gharama za ujenzi si ghali kama ukipata eneo zuri la kufyatulia matofali ya kuchoma utajenga nyumba nzuri kwa tope na baadae ukipiga plasta inakuwa nyumba nzuri ya kisasa.
Ulanzi pia unapatikana songea..kule mtu maarufu kwa mika michache iliyopita ni ottawa ana ghorofa mjini vituo vya mafuta pia ana nyumba pale Utwango karibu na Namabengo ambayo nyumba hiyo hakai mtu hata wala ndum walishindwa kukaa humo.
 
Si kitu rahisi,Kwa umri wangu wa miaka sitini na...++ namshukuru mwenyezi Mungu saana,manake nchi hii nimejaaliwa kukaa angalau kila wilaya ya Tanzania Bara kwa kipindi kirefu.

Nina uhakika hakuna Mtanzania yeyote anayeifahamu nchii hii vizuri kuliko mimi.

Hivyo basi namkaribisheni kwa anayehitaji ushauri kuhusu sehemu yeyote ya nchi ya Tanzania.

Namshukuruni sana.
maweeeeeeeeeeeeeeeeee
 
Mkuu hili swali nitakujibu k

Kwanza ukifika pale mjini...kuna sehemu inaitwa Manzese A..kuna pombe fulani inatengenezwa kwa kutumia muhogo..kama sijakosea jina lake ni yamkaya...
Songea kuna baridi lakini si kali kama ya Njombe au Ludewa.Songea vyakula vinapatikana kwa unafuu ..gharama za ujenzi si ghali kama ukipata eneo zuri la kufyatulia matofali ya kuchoma utajenga nyumba nzuri kwa tope na baadae ukipiga plasta inakuwa nyumba nzuri ya kisasa.
Ulanzi pia unapatikana songea..kule mtu maarufu kwa mika michache iliyopita ni ottawa ana ghorofa mjini vituo vya mafuta pia ana nyumba pale Utwango karibu na Namabengo ambayo nyumba hiyo hakai mtu hata wala ndum walishindwa kukaa humo.
Asante!
 
Mkuu naomba kujua kuhusu wilaya ya kilombero na wakazi wake ni makabila gan
 
Niambie Useketwa ipo wilaya gani na mkoa gani nitakuamini unaijua TZ
 
Back
Top Bottom