Nashauri tupunguze idadi ya wabunge

Nashauri tupunguze idadi ya wabunge

Lisifutwe lakini pawe na mchakato wa kuwapata wabunge makini sio waimba pambio
Wabunge wa hoja kama hizo za nguvu za kiume wengi hupitia vichochoro vya akina polepole kiujanja janja mpaka kupenya wanajikuta wapo mjengoni, hawa wabunge wa hivyo wengi hawajui kujenga Hoja mpaka waandikiwe kila kitu na akina hao hao waliowasaidia kuingia huko Bungeni
 
Unamaanisha wanawake wanaopelekwa bungeni kwa viti maalum kutoka CCM, CHADEMA n.k ni minority?
Naam, tunaweza kutoa endepo tu tutatengeneza KATIBA ambayo inayozingatia Minority Rights.
Maana lengo kubwa la Special Seats ni Affirmative Action and Minority Rights...
 
Kwakweli vinchi vya Kiafrika kwa kujitutumua kuna baadhi ya Nchi zilizoendelea Wabunge wanatumia Magari ya kawaida

Hawa wa kwetu gari V8 inabugia mafuta kama haina akili halafu hapo mlipaji ni Mwananchi anayenyonywa kila uchwao

Gari kama Landrover Station wagon ingewafaa hawa Wabunge
Yaani usiende mbali.. nchi ya Botswana pamoja na kujiweza kidogo lakini wanajitahidi sana ktk kuwa na serikali yenye strict financial displine na kutokuwa na haja ya kuwa na unnecessary goverment' luxurious expenditures, wakati wanajua wenyewe bado ni third world country na wala hakuna haja ya 'kujimwambafy'....
 
Unamaanisha wanawake wanaopelekwa bungeni kwa viti maalum kutoka CCM, CHADEMA n.k ni minority?
NDIYO, nchini Tanzania wanawake ni A Minority Group. Kitaalamu tunavyotafasiri A Minority Group hatuangalii idadi ya watu peke yake. Tunaangalia vitu vikubwa viwili kama A Degree of Vulnerability and Power/Authority in Decision Making. Hivyo tukizingatia haya wanawake ni A Minority Group ukilinganisha na wanaume ambao wako wachache lakini wameshikilia asilimia 95 ya nyadhifa zote za kiutawala.

Mfano mzuri zingatia kule Afrika-Kusini kipindi cha Makabulu: Weusi walikuwa ndiyo wengi nchini lakini ndiyo walikuwa ni A Minority Group considering a Degree of Vulnerability. Hivyo nadhani mambo kama haya wewe kama msomi inabidi ujikite katika kuyazingatia ili kujenga Tanzania imara na bora kuliko hii ya sasa ambayo imejaa maharamia.
 
Kweli mtoa Mada, Wabunge wengi kwanza hawajielewi, ovyo ovyo tu. Unakuta mwenzake anachangia ajenda nzuri yenye manufaa kwa wananchi, ananyanyuka mwingine anamkatisha, taarifa mweshimiwa speaker.
 
Bunge letu ni kubwa sana kwa uchumi tulio nao na ukubwa wa eneo tulilo nalo.

Kwa sasa tuna wabunge takribani 400. Na tuna wilaya 169.

Kwanini tusiwe na wabunge wanaoendana na wilaya zetu kwa kupunguza idadi ya majimbo.

Uwepo wa wabunge wengi kwanza unapunguza muda wa kujadili mambo kwa kina kwa kuharakisha kila mtu apate muda wa kuongea.

Pia kunatoa mwanya wa wabunge wavivu kujificha kwenye umati, wanatoroka wanakula posho hawachangii chochote.

Idadi hii kubwa ya bunge ni mzigo kwa taifa ni fedha kiasi gani tutaokoa ili tuzielekeze katika mambo mengine ya msingi?

Je, kiwango cha matumizi yao kinaakisi faida wanayoleta katika taifa?

Mambo wanayopitisha na kujadili yana faida kwa taifa kiasi cha kutuingiza kwenye hii hasara kubwa ya kuwalipa?
Umenena jambo la maana sana. Tungeanza kuondoa viti maalum vya wanawake na kuweka sheria kutaka vyama kuweka mizani ya kijinsia kwenye uteuzi wa wagombea wao. Ukiangalia idadi ya wabunge nchi tajiri kama uingereza, ufaransa na nyingine utastaajabu ukubwa wa bunge letu. Kila awamu ukiondoa ya jpm nec imekua ikiongeza majimbo kwa kuzingatia ongezeko la watu bila kuzingatia uchumi au ulazima wa kuanzisha majimbo mapya. Yote hayo ikiwa ni kukidhi mahitaji binafsi ya wanasiasa.
Ili kukidhi kupunguza wabungu spika ndugai aanze mara moja kwanza kutimua wabunge 19 wasiokua na chama bungeni ambao haieleweki kwa nini anawalinda licha ya kufukuzwa uanachama na chama chao. Vinginevyo ndugai achukuliwe hatua na bunge kwa matumizi mabaya ya fedha za umma.
 
sio tu kupunguza idadi, mie natamani bunge lifutwe kabisa lisiwepo...halina tija zaidi ya kututia hasara ya kuwalipa mishahara minono maposho na gharama kubwa kwenye uchafuzi (uchaguzi??!!) mkuu.
 
Nikianza na mfano wako wa SA Watu weusi wamekuwa majority siku zote. Makuburu ndio walikuwa minority na Utawala wao ulijulikana kama "White-minority rule"

Tukija hapa kwetu bado ni mjadala kusema wanawake ni minority group kama vile walemavu katika uwakilishi wa ubunge na udiwani.Wanawake Tanzania wanaweza kugombea katika vyama vyao kupata nafasi za uwakilishi bila ubaguzi, hakuna sheria, mazingira au mifumo katika vyama vyetu vya siasa zinazozuia wanawake kuwa wagombea ndio maana unaona wako wengi katika nafasi hizo.

Pia tufahamu kwamba ubunge ni kazi ya uwakilishi wa wananchi wa eneo fulani.Watu wa jimbo wanakuchagua ukawe sauti yao bungeni. Kama wananchi wa jinsia zote kutoka majimbo yote ya nchi wameamua kuchagua wanaume kuwa wabunge kupitia uchaguzi huru na wa haki "well and good" wameona hao ndio wanafaa kuwa wawakilishi wao. Lazima tuheshimu hivyo

Hatuhitaji kuwa na wabunge wasiowakilisha maeneo kama hawa wa viti maalum na wakuteuliwa na rais kwa kigezo chochote.
NDIYO, nchini Tanzania wanawake ni A Minority Group. Kitaalamu tunavyotafasiri A Minority Group hatuangalii idadi ya watu peke yake. Tunaangalia vitu vikubwa viwili kama A Degree of Vulnerability and Power/Authority in Decision Making. Hivyo tukizingatia haya wanawake ni A Minority Group ukilinganisha na wanaume ambao wako wachache lakini wameshikilia asilimia 95 ya nyadhifa zote za kiutawala.

Mfano mzuri zingatia kule Afrika-Kusini kipindi cha Makabulu: Weusi walikuwa ndiyo wengi nchini lakini ndiyo walikuwa ni A Minority Group considering a Degree of Vulnerability. Hivyo nadhani mambo kama haya wewe kama msomi inabidi ujikite katika kuyazingatia ili kujenga Tanzania imara na bora kuliko hii ya sasa ambayo imejaa maharamia.
 
Nikianza na mfano wako wa SA Watu weusi wamekuwa majority siku zote. Makuburu ndio walikuwa minority na Utawala wao ulijulikana kama "White-minority rule"

Tukija hapa kwetu bado ni mjadala kusema wanawake ni minority group kama vile walemavu katika uwakilishi wa ubunge na udiwani.Wanawake Tanzania wanaweza kugombea katika vyama vyao kupata nafasi za uwakilishi bila ubaguzi, hakuna sheria, mazingira au mifumo katika vyama vyetu vya siasa zinazozuia wanawake kuwa wagombea ndio maana unaona wako wengi katika nafasi hizo.

Pia tufahamu kwamba ubunge ni kazi ya uwakilishi wa wananchi wa eneo fulani.Watu wa jimbo wanakuchagua ukawe sauti yao bungeni. Kama wananchi wa jinsia zote kutoka majimbo yote ya nchi wameamua kuchagua wanaume kuwa wabunge kupitia uchaguzi huru na wa haki "well and good" wameona hao ndio wanafaa kuwa wawakilishi wao. Lazima tuheshimu hivyo

Hatuhitaji kuwa na wabunge wasiowakilisha maeneo kama hawa wa viti maalum na wakuteuliwa na rais kwa kigezo chochote.
Inategemea wewe unaelewaje na kutasfirije neno Minority Group. Lakini kitaalamu linatafsiriwa kwa kuangalia A Degree of Vulnerability and Power: Weusi kule Afrika Kusini walikuwa a vulnerable group with no power/authority to determine their own lives. Ukitafasiri kwa kuangalia idadi na wingi wa watu tu basi lazima kuna sehemu utakwama. Sambamba na hilo utakuwa hufahamu vizuri historia ya Tanganyika na Zanzibar hadi hao wanawake kufika hapo walipo leo.

Pili, kitaalamu hicho unachokitetea kuhusu wangunge na majimbo tunakiita THE DOCTRINE OF MANDATE na kwenye ulimwengu wetu huu wa leo kimeshapitwa na wakati. Kusema ubunge ni uwakilishi wa eneo fulani ni kosa kubwa sana kitaalamu. Ukiamini hivi ina maanisha wabunge wote waliopo bungeni watakuwa na uhalali wa kuzungumzia tu matatizo ya majimbo yao bila kugusa matatizo ya majimbo mengine au masuala mengine ya kitaifa.

Tatu, ukiamini katika THE DOCTRINE OF MANDATE inamaanisha kwamba bunge halitakuwa muhimili wa dola ambao unatoa maamuzi yanayogusa kila kundi ndani ya taifa. Ndiyo unawakilisha matatizo ya jimbo lako lakini watu wako haohao kwenye jimbo wana makundi yao mengine pia kama waalimu, wakulima, wavuvi na wafanyabiashara. Hivyo lazima uwe na bunge ambalo haliangalii tu jimbo bali mambo muhimu ya kitaifa. Naamini changamoto za makundi fulani fulani kwenye jamii hufahamika vizuri na wahusika......
 
Watumishi wakipunguzwa itakuwa tabu mitaani familia zitataabika mno, wa kupunguzwa ni wabunge pekee ndiyo wameonekana mzigo kwa kodi za watanzania
Wengi hawafanyi kazi zao kwa mujibu wa mikataba yao hasa hawa wa UMMA,hata kama kazi yenyewe sio ya kwenda field ,mtu ukimuassess amefanya nini kwa mwezi mzima unaweza ukabaki mdomo wazi mkuu,wapewe chao wasepeshwe,familia zao haziwezi kuteteleka watatumia viinua mgongo vyao kuanzisha biashara,au kulima,ama kufuga na watazowea tu mkuu
 
Back
Top Bottom