Nashauri tupunguze idadi ya wabunge

Wazo zuri...... Ila Mimi niliwaza mbali zaidi.......

Nawaza kwamba walimu wakuu wa shule za sekondari ambazo zipo kila kata ndio wawe wawakilishi wa wananchi bungeni.....

Waongezewe tu mshahara hata 500k kila mmoja na posho kidogo wakienda kuwawakilisha wananchi bungeni......

Na bunge Hilo likutane walau Mara mbili kila mwaka. Mara ya kwanza kupeleka matatizo ya kata husika na Mara ya pili kufuatilia utekelezaji.

Usafiri, Hawa wanawe,a kupelekwa kwa Costa au mabasi......

Kuliko hii gharama tunaingia Sasa hivi.

Africa tuamke
 
Wabunge wa hoja kama hizo za nguvu za kiume wengi hupitia vichochoro vya akina polepole kiujanja janja mpaka kupenya wanajikuta wapo mjengoni, hawa wabunge wa hivyo wengi hawajui kujenga Hoja mpaka waandikiwe kila kitu na akina hao hao waliowasaidia kuingia huko Bungeni
Kama yule Neema ni mbunge anaewakilisha NGO's.
 
Nikianza na mfano wako wa SA Watu weusi wamekuwa majority siku zote. Makuburu ndio walikuwa minority na Utawala wao ulijulikana kama "White-minority rule"

Tukija hapa kwetu bado ni mjadala kusema wanawake ni minority group kama vile walemavu katika uwakilishi wa ubunge na udiwani.Wanawake Tanzania wanaweza kugombea katika vyama vyao kupata nafasi za uwakilishi bila ubaguzi, hakuna sheria, mazingira au mifumo katika vyama vyetu vya siasa zinazozuia wanawake kuwa wagombea ndio maana unaona wako wengi katika nafasi hizo.

Pia tufahamu kwamba ubunge ni kazi ya uwakilishi wa wananchi wa eneo fulani.Watu wa jimbo wanakuchagua ukawe sauti yao bungeni. Kama wananchi wa jinsia zote kutoka majimbo yote ya nchi wameamua kuchagua wanaume kuwa wabunge kupitia uchaguzi huru na wa haki "well and good" wameona hao ndio wanafaa kuwa wawakilishi wao. Lazima tuheshimu hivyo

Hatuhitaji kuwa na wabunge wasiowakilisha maeneo kama hawa wa viti maalum na wakuteuliwa na rais kwa kigezo chochote.

Nadhani hawa wa kuteuliwa na Rais ingekuwa tu kama wanaenda kuwa mawaziri na hawakuwa wabunge. Sio mambo ya Polepole na Bashiru
 
Wazo zuri...... Ila Mimi niliwaza mbali zaidi.......

Nawaza kwamba walimu wakuu wa shule za sekondari ambazo zipo kila kata ndio wawe wawakilishi wa wananchi bungeni.....

Waongezewe tu mshahara hata 500k kila mmoja na posho kidogo wakienda kuwawakilisha wananchi bungeni......

Na bunge Hilo likutane walau Mara mbili kila mwaka. Mara ya kwanza kupeleka matatizo ya kata husika na Mara ya pili kufuatilia utekelezaji.

Usafiri, Hawa wanawe,a kupelekwa kwa Costa au mabasi......

Kuliko hii gharama tunaingia Sasa hivi.

Africa tuamke

Kwanini waalimu wa kuu na wakiwa huko bungeni shule zitasimamiwa na nani?
 
Bunge letu ni kubwa sana kwa uchumi tulio nao na ukubwa wa eneo tulilo nalo.

Kwa sasa tuna wabunge takribani 400. Na tuna wilaya 169.

Kwanini tusiwe na wabunge wanaoendana na wilaya zetu kwa kupunguza idadi ya majimbo.

Uwepo wa wabunge wengi kwanza unapunguza muda wa kujadili mambo kwa kina kwa kuharakisha kila mtu apate muda wa kuongea.

Pia kunatoa mwanya wa wabunge wavivu kujificha kwenye umati, wanatoroka wanakula posho hawachangii chochote.

Idadi hii kubwa ya bunge ni mzigo kwa taifa ni fedha kiasi gani tutaokoa ili tuzielekeze katika mambo mengine ya msingi?

Je, kiwango cha matumizi yao kinaakisi faida wanayoleta katika taifa?

Mambo wanayopitisha na kujadili yana faida kwa taifa kiasi cha kutuingiza kwenye hii hasara kubwa ya kuwalipa?
Haya ndo tunapaswa kujadili JF siyo masuala ya legacy ya mwendazake kila siku. Naunga mkono hoja.

Sent from my vivo 1904 using JamiiForums mobile app
 
Wabunge wa viti maalumu waondolewe wote zikiwemo nafasi 10 za rais.
Mawaziri wasiteuliwe kutoka kwa wabunge
Halafu kila wilaya iwe na mbunge mmoja
Hapo umenena ndugu, CCM inaweza kuwa janga la Taifa kwa sababu mambo muhimu kama haya yaliwekwa katika katiba pendekezwa ya Warioba lakini maSISIem yalikataa sababu ya kujali matumbo yao tu.
 
Kwanini waalimu wa kuu na wakiwa huko bungeni shule zitasimamiwa na nani?
Sio lazima wakae kikao kimoja mwezi. Fuatilia bunge la China.

Kikao kinaweza kuchukua siku tano na shule akakaimu makamu mkuu wa shule.

Pia sio lazima mambo yote yaongelewe. Mengine yanaweza kuwasilishwa on paper.
 
Ujinga Gani sijui nzuri kwenye jamii:

Nimefanya mapenzi nimechoka ikawa ujinga au Malaya

Nimejenga nyumba ikawa ujinga

Nikaoa ikawa ujinga maana Mwanamke alikuwa anawaza vitu ambavyo sina


Nimesoma Elimu siitumii ikawa ujinga

Nimekunywa bia ikawa ujinga

Nimesafiri kila mkoa ikawa ujinga

Nikafikilia kifo na kuzika watu hata mochuari wapo ikawa ujinga

+ Error term

Maisha yawezekana ni ujinga Karibu ulanzi nimemwalika na wema sepetu maana kazeeka na ujanja
 
Pia Bunge la Zanzibar sasa iwe lazima wabunge tokea Tanganyika waingie kule, siyo wao kuwa na Bunge lao binafsi kisha wao wanaingia Bungeni Dodoma pasipo wa wabunge wa Tanganyika kwenda Bungeni kwao, cha Zanzibar ni cha wazanzibar tu na cha Tanganyika ni cha wote hii dhana ifutwe sasa, wabunge wawe huru kuingia Bungeni kote kote, Zanzibar kuendelea kula posho Dodoma ni wizi lazima wabunge wa Tanganyika wale posho Zanzibar iwe ngoma sawa.

MKuu unapokwama ni hapa, Hakuna kitu cha Tanganyika, kuna cha Tanzania tu na Zanzibar ni part of Tanzania. Mnapoambia kuwe na serekali 3 hua mnashindwa kuelewa mantiki yake. Tanganyika haipo inatakiwa kurejeshwa ili mambo yapate kuenda sawa.
 
Ni kweli, Bunge limeguzwa kuwa kijiwe cha kusakia ajira ..!! wakati lengo hasa halikuwa hilo.
 
Naunga mkono hoja wabunge wapunguzwe hasa mjini hakuna haja ya wabunge maana kuna mwamko wa wananchi kujipigia kelele kero zao , vijijini sawa wabunge wanahitajika kutumia fungu la mbunge kuongeza kasi ya maendeleo, na viti maalumu waondolewe pia.
 
Hata siku moja hakuna mbunge atakaeunga hoja hii mkono maana hawajui ni jimbo gani litafutwa, hoja nzuri, wabunge wengi sana.

Kwahiyo hakuna namna ya wananchi kwenda kinyume na maslahi taifa hatuna jinsi ya kuwazuia
 
Eti Zanzibar ina wabunge wengi kuliko Dsm wakati Dsm inawatu mara 4 ya Znz
Dsm pekee ina watu milion 6 mpaka saba lakini ina wabunge wachache kuliko Zanzibar yenye watu kama milion 3 hivi idadi za wabunge zipunguzwe kuanzia Zanzibar mpaka Tanganyika
 
Kweli mtoa Mada, Wabunge wengi kwanza hawajielewi, ovyo ovyo tu. Unakuta mwenzake anachangia ajenda nzuri yenye manufaa kwa wananchi, ananyanyuka mwingine anamkatisha, taarifa mweshimiwa speaker.
Kwenye taarifa ndipo kuna Tatizo kubwa kwani taarifa nyingi huwa hazina maana na haziendani na hoja iliyopo mezani au wakati mwingine taarifa huwa za kumvuruga mtoa hoja , kipengele cha taarifa kiangaliwe upya
 
Wabunge wapunguzwe kwa zaidi ya 75%
Mikoa ipinguzwe
WIlaya zipunguzwe,

Fedha nyingi ya taifa inatumika kuhudumikia waheshimiwa kuliko wananchi
Pesa inayotumika kuwalea kuwatunza kuwahudumia utitiri wa wa hao viongozi ni nyingi na kama ingekuwa imeelekezwa kwenye maendeleo mda huu Tanzania ingekuwa imejenga Bandari kubwa yenyewe pasipo kutegemea Nchi yeyote na uchumi ungekuwa imara zaidi
 
Pesa inayotumika kuwalea kuwatunza kuwahudumia utitiri wa wa hao viongozi ni nyingi na kama ingekuwa imeelekezwa kwenye maendeleo mda huu Tanzania ingekuwa imejenga Bandari kubwa yenyewe pasipo kutegemea Nchi yeyote na uchumi ungekuwa imara zaidi

Mbaya zaidi hatuoni output ya hela tunayowalipa
 
Back
Top Bottom