Rohombaya
JF-Expert Member
- Jul 4, 2011
- 13,055
- 10,339
Dah....halafu tuje tufute na ruzuku za VYAMATuondoe na Ma RAS na DAS pia
Sent using Jamii Forums mobile app
Dah....halafu tuje tufute na ruzuku za VYAMATuondoe na Ma RAS na DAS pia
Kwa maoni yangu viti maalum waondolewe lakini wa kuteuliwa wabaki.
Wakuteuliwa wabaki kwa sababu Raisi anaweza asipate anayemhitaji kutoka kwa wabunge waliochaguliwa hivyo anaweza kuteua watu anaowaona watamsaidia zaidi kutimiza majukumu yake.
Raisi anaweza kuwa na mtu ambaye amefanya nae kazi kwa kipindi fulani akapenda utendaje kazi wake kama hakuchaguliwa kuwa mbunge ni rahisi kumteua kuja kusaidia.
Nionavyo mimi.
Wazo Nzuri sana, wabunge wachaguliwe kwa wilaya sio majimboBunge letu ni kubwa sana kwa uchumi tulio nao na ukubwa wa eneo tulilo nalo.
Kwa sasa tuna wabunge takribani 400. Na tuna wilaya 169.
Kwanini tusiwe na wabunge wanaoendana na wilaya zetu kwa kupunguza idadi ya majimbo.
Uwepo wa wabunge wengi kwanza unapunguza muda wa kujadili mambo kwa kina kwa kuharakisha kila mtu apate muda wa kuongea.
Pia kunatoa mwanya wa wabunge wavivu kujificha kwenye umati, wanatoroka wanakula posho hawachangii chochote.
Idadi hii kubwa ya bunge ni mzigo kwa taifa ni fedha kiasi gani tutaokoa ili tuzielekeze katika mambo mengine ya msingi?
Je, kiwango cha matumizi yao kinaakisi faida wanayoleta katika taifa?
Mambo wanayopitisha na kujadili yana faida kwa taifa kiasi cha kutuingiza kwenye hii hasara kubwa ya kuwalipa?
Wewe unapenda upinzani?Wabunge wetu bahati mbaya wamekuwa ni wachumia matumbo, na ukianza kuwasemea maslahi yao, utashangaa utajua hakuna upinzani, wataungana na lao litakuwa moja.
Watakuambia wana kazi nyingi, kazi za kupigana vijembe!
Kenyatta alithubutu, akafyekelea mbali mishahara iliyokuwa mzigo alipoingia ofisini.
Everyday is Saturday...............................
Nadhani bado unapata shida kupembua, kuchamba na kuchambua hoja tunayozungumza. Mimi nimezungumzia A Minority Group siyo Minority: Semantically and Technically haya maneno hayana maana sawa. Wanazuoni waliounda na kutafasiri hilo neno kama Prof Lous Wirth hawakuzungumzia idadi peke yake bali Power and Vulnerability.Minority ni suala la Idadi ndogo kwa kuanzia mambo ya degree of vulnerability and power yanafuata baadaye.
Pia, nadhani huna taarifa za kutosha kuhusu demokrasia, hasahasa jinsi ilivyoanza kule Athene ya Ugiriki ya kale ndiyo maana unahisi naleta maneno yasiyo muhimu (Fallacies) kwenye hoja. Ungefanya tafiti kidogo basi naamini tungekuwa kwenye ukurasa mmoja.Huko tunapoamini demokrasia ndipo ilianzia, ambapo demokrasia ndio inapaita nyumbani kwake hakuna kitu kama mbunge wa viti maalum au wa kuteuliwa.Huwezi kuingia bungeni pasipo kuchaguliwa na wananchi wa eneo fulani.
Unafahamu maana ya The Doctrine of Mandate ???Wabunge wote kuchaguliwa kupitia maeneo ya kijimbo haiwezi kuzuia watu kujadili mambo ya kitaifa juu ya yale yanayohusu majimbo yao. Hiyo issue ya mandate ni dilemma isiyo na mashiko, ni straw man fallacy.
Wabunge wanaopaswa kupunguzwa ni wa ZanzibarBunge letu ni kubwa sana kwa uchumi tulio nao na ukubwa wa eneo tulilo nalo.