Bunge letu ni kubwa sana kwa uchumi tulio nao na ukubwa wa eneo tulilo nalo.
Kwa sasa tuna wabunge takribani 400. Na tuna wilaya 169.
Kwanini tusiwe na wabunge wanaoendana na wilaya zetu kwa kupunguza idadi ya majimbo.
Uwepo wa wabunge wengi kwanza unapunguza muda wa kujadili mambo kwa kina kwa kuharakisha kila mtu apate muda wa kuongea.
Pia kunatoa mwanya wa wabunge wavivu kujificha kwenye umati, wanatoroka wanakula posho hawachangii chochote.
Idadi hii kubwa ya bunge ni mzigo kwa taifa ni fedha kiasi gani tutaokoa ili tuzielekeze katika mambo mengine ya msingi?
Je, kiwango cha matumizi yao kinaakisi faida wanayoleta katika taifa?
Mambo wanayopitisha na kujadili yana faida kwa taifa kiasi cha kutuingiza kwenye hii hasara kubwa ya kuwalipa?