Nashauri tupunguze idadi ya wabunge

Bunge letu ni kubwa sana kwa uchumi tulio nao na ukubwa wa eneo tulilo nalo.

Kwa sasa tuna wabunge takribani 400. Na tuna wilaya 169.

Kwanini tusiwe na wabunge wanaoendana na wilaya zetu kwa kupunguza idadi ya majimbo.

Uwepo wa wabunge wengi kwanza unapunguza muda wa kujadili mambo kwa kina kwa kuharakisha kila mtu apate muda wa kuongea.

Pia kunatoa mwanya wa wabunge wavivu kujificha kwenye umati, wanatoroka wanakula posho hawachangii chochote.

Idadi hii kubwa ya bunge ni mzigo kwa taifa ni fedha kiasi gani tutaokoa ili tuzielekeze katika mambo mengine ya msingi?

Je, kiwango cha matumizi yao kinaakisi faida wanayoleta katika taifa?

Mambo wanayopitisha na kujadili yana faida kwa taifa kiasi cha kutuingiza kwenye hii hasara kubwa ya kuwalipa?
Ni wazo zuri lakini halina uthibitisho wa kutosha.
 
Tuondoe Wakuu wa Mikoa na Wilaya ila Wabunge wapunguziwe mishahara au posho
Wakuu wa wilaya na mikoa ni watendaji ( serikalini).

Wabunge ni (wanasiasa).

Naunga mkono hoja ya kuwa na wabunge wachache kulingana na wilaya.
 
Japo wabunge ndo wana jadili hoja. Lakini hawawezi kuijadili hii hoja japo ni mhimu sana.
 
Bunge letu ni kubwa sana kwa uchumi tulio nao na ukubwa wa eneo tulilo nalo.

Kwa sasa tuna wabunge takribani 400. Na tuna wilaya 169.

Kwanini tusiwe na wabunge wanaoendana na wilaya zetu kwa kupunguza idadi ya majimbo.

Uwepo wa wabunge wengi kwanza unapunguza muda wa kujadili mambo kwa kina kwa kuharakisha kila mtu apate muda wa kuongea.

Pia kunatoa mwanya wa wabunge wavivu kujificha kwenye umati, wanatoroka wanakula posho hawachangii chochote.

Idadi hii kubwa ya bunge ni mzigo kwa taifa ni fedha kiasi gani tutaokoa ili tuzielekeze katika mambo mengine ya msingi?

Je, kiwango cha matumizi yao kinaakisi faida wanayoleta katika taifa?

Mambo wanayopitisha na kujadili yana faida kwa taifa kiasi cha kutuingiza kwenye hii hasara kubwa ya kuwalipa?
Ni kweli mkuu upo sawa kabisa mimi pia nina mtazamo kama huo! Ukiangalia hata mikoani na wilayani kuna mlundikano mkubwa wa watendaji usio na tija kiuchumi zaidi tu ya kukamua bajeti.
Utakuta wilaya moja kuna mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa wilaya, mbunge wa jimbo, katibu tawala wa wilaya, Katibu tarafa wa wilaya, mtedaji wa kata n.k! Hawa wote wanatengewa bajeti na kulipwa na wilaya husika! Je kama mbunge yupo hivi mkuu wa wilaya na katibbu tawala wa wilaya ni wa kazi gani?
Mbunge anaweza kabisa kufanya shughuli zote za mkuu wa wilaya na HRO wa wilaya akafanya shughuli zote za DAS mpaka za katibu tarafa!
Kwa njia hiyo kwanza tutakuwa na wabunge kulingana na idadi ya wilaya, pili tutaokoa fedha tunazolipa kuwatuza DC, DAS na katiu tarafa wa wilaya.
Sio huko tu mifumo hii irekeishwe mpaka kweye Mikoa, kanda na wizara kuna watendaji wengi sana ambao serikali inagharamia mishahara, magari na mafuta lakini ukiangalia utaona hawana ulazima wowote wa kuibebesha serikali mzigo huo.
Pia hiki kipindi tunachotekeleza miradi mikuwa kama SGR ambao hadi sasa umeshakula Trilioi 11 huku tukiwa tumejenga km 400 tu kati ya 4,884, ni wakati sasa wa serikali kufyeka mishahara ya wabunge, mawaziri , wakurugenzi mpaka wakuu wa idara za halmashauri a mashirika ya umma, katika makudi hayo yote kama serikali itaweka kima cha juu kisizidi 3M. nina hakika fedha ya SGR lazima itapatikana tena bila kukopa kokote!
Watumishi wa umma waachwe huru na madaraja yao yapade kama kawaida wameshateswa vya kutosha!
 
Watu wa kupunguza.
1.Job Ndugai
2. Dr Tulia Ackson
3. Azzan Zungu
 
Ingependeza, ingepunguza gharama na kuongeza tija.
Wabunge wa viti maalumu waondolewe wote zikiwemo nafasi 10 za rais.
Mawaziri wasiteuliwe kutoka kwa wabunge
Halafu kila wilaya iwe na mbunge mmoja
 
Nchi ya watu 60 million, ina idadi kubwa ya wabunge sawa na India nchi yenye watu 1 Billion,
Mzee Warioba alipendekeza wabunge wasizidi 70, ambao wamesoma (Gender izingatiwe)
Ile rasimu ingepita tungepunguza kadhia ya kuwa na vichaa wengi sana kule bungeni.
Duu ndio maana walimtuma hadi Bashite akaenda kumfanyia fujo , posho na mshahara wa ubunge vinono sana !
 
Minority ni suala la Idadi ndogo kwa kuanzia mambo ya degree of vulnerability and power yanafuata baadaye.

Huko tunapoamini demokrasia ndipo ilianzia, ambapo demokrasia ndio inapaita nyumbani kwake hakuna kitu kama mbunge wa viti maalum au wa kuteuliwa.Huwezi kuingia bungeni pasipo kuchaguliwa na wananchi wa eneo fulani.

Hiki kituko cha wabaunge wasio na majimbo kipo huu ukanda wetu wa Africa, Uganda kuna hadi wabunge kupitia jeshi wakati jeshi ni chomba cha dola na liko chini ya executive!

Wabunge wote kuchaguliwa kupitia maeneo ya kijimbo haiwezi kuzuia watu kujadili mambo ya kitaifa juu ya yale yanayohusu majimbo yao. Hiyo issue ya mandate ni dilemma isiyo na mashiko, ni straw man fallacy.
Inategemea wewe unaelewaje na kutasfirije neno Minority Group. Lakini kitaalamu linatafsiriwa kwa kuangalia A Degree of Vulnerability and Power: Weusi kule Afrika Kusini walikuwa a vulnerable group with no power/authority to determine their own lives. Ukitafasiri kwa kuangalia idadi na wingi wa watu tu basi lazima kuna sehemu utakwama. Sambamba na hilo utakuwa hufahamu vizuri historia ya Tanganyika na Zanzibar hadi hao wanawake kufika hapo walipo leo.

Pili, kitaalamu hicho unachokitetea kuhusu wangunge na majimbo tunakiita THE DOCTRINE OF MANDATE na kwenye ulimwengu wetu huu wa leo kimeshapitwa na wakati. Kusema ubunge ni uwakilishi wa eneo fulani ni kosa kubwa sana kitaalamu. Ukiamini hivi ina maanisha wabunge wote waliopo bungeni watakuwa na uhalali wa kuzungumzia tu matatizo ya majimbo yao bila kugusa matatizo ya majimbo mengine au masuala mengine ya kitaifa.

Tatu, ukiamini katika THE DOCTRINE OF MANDATE inamaanisha kwamba bunge halitakuwa muhimili wa dola ambao unatoa maamuzi yanayogusa kila kundi ndani ya taifa. Ndiyo unawakilisha matatizo ya jimbo lako lakini watu wako haohao kwenye jimbo wana makundi yao mengine pia kama waalimu, wakulima, wavuvi na wafanyabiashara. Hivyo lazima uwe na bunge ambalo haliangalii tu jimbo bali mambo muhimu ya kitaifa. Naamini changamoto za makundi fulani fulani kwenye jamii hufahamika vizuri na wahusika......
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Kwa mfumo wetu wa uongozi hata wangekusanya Trillion 3 kwa mwezi bado zingeishia kulipa mishahara, posho na kununua mavietee tu. Pesa Kiduchu ndizo zitaendelea kwenye miradi maendeleo.
Ni kweli mkuu upo sawa kabisa mimi pia nina mtazamo kama huo! Ukiangalia hata mikoani na wilayani kuna mlundikano mkubwa wa watendaji usio na tija kiuchumi zaidi tu ya kukamua bajeti.
Utakuta wilaya moja kuna mkuu wa wilaya, mkurugenzi wa wilaya, mbunge wa jimbo, katibu tawala wa wilaya, Katibu tarafa wa wilaya, mtedaji wa kata n.k! Hawa wote wanatengewa bajeti na kulipwa na wilaya husika! Je kama mbunge yupo hivi mkuu wa wilaya na katibbu tawala wa wilaya ni wa kazi gani?
Mbunge anaweza kabisa kufanya shughuli zote za mkuu wa wilaya na HRO wa wilaya akafanya shughuli zote za DAS mpaka za katibu tarafa!
Kwa njia hiyo kwanza tutakuwa na wabunge kulingana na idadi ya wilaya, pili tutaokoa fedha tunazolipa kuwatuza DC, DAS na katiu tarafa wa wilaya.
Sio huko tu mifumo hii irekeishwe mpaka kweye Mikoa, kanda na wizara kuna watendaji wengi sana ambao serikali inagharamia mishahara, magari na mafuta lakini ukiangalia utaona hawana ulazima wowote wa kuibebesha serikali mzigo huo.
Pia hiki kipindi tunachotekeleza miradi mikuwa kama SGR ambao hadi sasa umeshakula Trilioi 11 huku tukiwa tumejenga km 400 tu kati ya 4,884, ni wakati sasa wa serikali kufyeka mishahara ya wabunge, mawaziri , wakurugenzi mpaka wakuu wa idara za halmashauri a mashirika ya umma, katika makudi hayo yote kama serikali itaweka kima cha juu kisizidi 3M. nina hakika fedha ya SGR lazima itapatikana tena bila kukopa kokote!
Watumishi wa umma waachwe huru na madaraja yao yapade kama kawaida wameshateswa vya kutosha!
 
Ubunge wa viti maalum na kuteuliwa hauna tija, uondolewe. Ni matumizi mabaya ya kodi za wavuja jasho na wanyonge.
Dogo unapjaribu kushawishi hoja, weka ushahidi kuntu kwenye hoja na sio kuongea tu. Mfano, kwanini unahisi ni wengi. Kwa vigezo vipi? Ulitaka wawe wangapi kwa vigezo vipi? Lakini kusema tu, haitoshi.
 
Bunge letu ni kubwa sana kwa uchumi tulio nao na ukubwa wa eneo tulilo nalo.

Kwa sasa tuna wabunge takribani 400. Na tuna wilaya 169.

Kwanini tusiwe na wabunge wanaoendana na wilaya zetu kwa kupunguza idadi ya majimbo.

Uwepo wa wabunge wengi kwanza unapunguza muda wa kujadili mambo kwa kina kwa kuharakisha kila mtu apate muda wa kuongea.

Pia kunatoa mwanya wa wabunge wavivu kujificha kwenye umati, wanatoroka wanakula posho hawachangii chochote.

Idadi hii kubwa ya bunge ni mzigo kwa taifa ni fedha kiasi gani tutaokoa ili tuzielekeze katika mambo mengine ya msingi?

Je, kiwango cha matumizi yao kinaakisi faida wanayoleta katika taifa?

Mambo wanayopitisha na kujadili yana faida kwa taifa kiasi cha kutuingiza kwenye hii hasara kubwa ya kuwalipa?
Naunga mkono hoja.
Wabunge watokane na wilaya zilizopo. Pia wabunge wa viti maalumu wasiwepo hakuna wanachokifanya zaidi ya kumaliza pesa zetu.
 
Ubunge wa viti maalum na kuteuliwa hauna tija, uondolewe. Ni matumizi mabaya ya kodi za wavuja jasho na wanyonge.
Kwa maoni yangu viti maalum waondolewe lakini wa kuteuliwa wabaki.
Wakuteuliwa wabaki kwa sababu Raisi anaweza asipate anayemhitaji kutoka kwa wabunge waliochaguliwa hivyo anaweza kuteua watu anaowaona watamsaidia zaidi kutimiza majukumu yake.
Raisi anaweza kuwa na mtu ambaye amefanya nae kazi kwa kipindi fulani akapenda utendaje kazi wake kama hakuchaguliwa kuwa mbunge ni rahisi kumteua kuja kusaidia.
Nionavyo mimi.
 
Back
Top Bottom