Baada ya kukiri kuwa alikosea na kuomba msamaha Ndugai amezika kabisa kaheshima kadogo alichobaki nacho. Simpendi kabisa Ndugai, nadhani ni spika wa hovyo zaidi kuwahi kukalia hicho.Hapa lazima uelewe hoja ni nini
Kumpinga Rais kama kiongozi wa mhimili mwingine si jambo geni au baya.
Alichozungumza si kibaya au kigeni
Tatizo ni hili, kusingizia alinukuliwa vibaya
Kuomba msamaha kwa aliyosema kwa maana hajui alisema nini au alikusudia nini
Kuzungumzia miswada iliyopita mikononi mwake kinafiki
Kuhojiwa uwezo wake ''kiakili'' na Viongozi wote wakuu wa nchi
Heshima yake haipo kwasasa mbele ya jamii. Ajiuzulu tu
Yes lakini hiyo haitaondoa ukweli kuwa popote atakapokaa, simama au kutembea watu watahoji swali moja, mkuu wa nchi alitilia shaka utimamu na umri wa Ndugai.
Hana heshima popote pale.
Juzi kasingizia media leo anaomba msamaha , huyu hana maana hata akibali Spika heshima yake haipo. Suala hapa si kuondoka au kubaki, tunahoji heshima yake , heshima ya Uspika na heshima ya Bunge.
Heshima yake ilikuwa na mashaka, sasa ametoa wasi wasi wote. Mh Rais alipohoji utimamu na umri wake(mtu mzima) sijui alimwacha na nini!Baada ya kukiri kuwa alikosea na kuomba msamaha Ndugai amezika kabisa kaheshima kadogo alichobaki nacho. Simpendi kabisa Ndugai, nadhani ni spika wa hovyo zaidi kuwahi kukalia hicho.
Akina Ndugai ! sijui wanaieleza nini jamii ya kizazi kijacho! huyu naye eti ni role model! AiseeHata hivyo kama angejipa ujasiri wa kusimamia alichokisema juzi hadharani, ningempa benefit of doubt kwani hata saa mbovu mara moja katika saa ishirini na nne husema kweli.
CCM imeiharibu sana hii nchi yetu kwa kutusukumizia viongozi wabovu moja baada ya mwingine na ilijulikana wazi kwa kila mwenye akili kwamba kuna siku tutakwama na bado.
Hili la Ndugai ni mwanzo tu na kama Watanzani hatutachukua hatua tukae tukijua tunaelekea shimoni. Kama nilivyoanza simpendi Ndugai lakini nitatetea haki yake ya kutoa maoni kama Mtanzania.
Ndio unafiki, kwake Joho la bendera ni muhimu sana kwasababu tu ya ulajiNi bahati mbaya sana kaomba msamaha kwani amedhihirisha jinsi CCM ilivyojaa viongozi wanafiki waliopo pale tu kutetea matumbo yao hivyo hana namna bali kujiuzulu nafasi yake mara moja.
Una miss point sanaNdugai sio mnyonge me nakwambia, hawez kuondoka kama watu wanavyodhania na lazima atasema, na kuna watu wako upande wake
Siasa Iko hivyo! Hata kama ni kweli anataka uraisi ni haki yake mbona mama ameonesha Nia ya kugombea mapema Sana ?
Ndugu zangu wa JF
Nitoe maoni yangu kama Mtanzania Mzalendo kufuatia kauli ya Ndugai kubeza kitendo cha Rais Samia kuendelea na Sera ya kukopa Fedha nje ya Nchi kugharamia miradi ya Maendeleo
Kauli ya Mheshimiwa Ndugai sio tu inabeza na kudharau mamlaka ya Rais bali inalenga kuhujumu jitihada za makusudi za Rais Samia kukamilisha miradi mikubwa ya maendeleo inayohitaji Fedha nyingi sana kuikamilisha
Mheshimiwa Ndugai akiwa Kiongozi wa Bunge ameshindwa kuonyesha uwajibikaji wa pamoja wa kidola na ameamua kwa makusudi kutumia nafasi yake vibaya kwa maslahi binafsi
Ieleweke Rais Samia anakopa fedha kwa maslahi ya Nchi yetu na amekuwa muwazi kwenye suala hili
Ieleweke kuwa Fedha za Tozo haziwezi kugharamia miradi yote mikubwa ya kimkakati na haiwezi kuwa mbadala wa kukopa Fedha
Mheshimiwa Ndugai angeliweza kuomba kuonana na Rais Samia na kumshauri aonavyo badala ya njia aliyoitumia ya kuropoka HADHARANI!
Kwa maoni yangu kauli ya Mheshimiwa Ndugai likusudia kukwamisha juhudi za Rais wetu kukamilisha miradi mbalimbali ya Maendeleo kama ilivyoelekezwa kwenye Ilani ya CCM
Nashauri Mheshimiwa JOB NDUGAI ajiuzulu mara moja wadhifa wake wa Uspika na akishindwa kufanya hivyo mamlaka husika zimchukulie hatua za kumvua uanachama wa CCM kwani kwa sasa sio Mwenzetu tena
Tumpe ushirikiano Rais Samia
KaziIendelee
Una miss point sana
Hoja si Ndugai kuondoka au kutoondoka. Hoja si Ndugai anautaka Urais au la na wala si kwamba alichosema hakina mantiki. Hakuna mjadala kuhusu hilo
Hoja ni kwamba, mosi, alisingizia vyombo kupotosha. Ukweli ni kuwa hakuna upotoshaji.
Aliomba msamaha kwa kauli zake. Msamaha kamkosea nani na kwanini kwa kutoa maoni yake?
Pili, miswada aya kukopa ilipita Bungeni kwake, hakuanzisha mjadala.
Ndugai anayepitisha miswada mingine usiku wa manane ili kukidhi haja za Watawala, kwa hili kilimshinda kitu gani kuanzisha mjadala kama Spika na Mbunge?
Tatu, unafiki wa kusema kitu anachoamini halafu kukikana na ikishindikana kuomba msamaha unaeleza jambo moja, kwamba, kwake Uspika si utumishi wa umma ni Joho na masilahi
Kama alivyosimama wima kutetea Bunge kutodhalilishwa, hakuna sababu ya kudhalilisha Bunge.
Tumeambia jambo kuhusu ''utu uzima wake na akili'' na wale anaofanya naye kazi kwa ukaribu
Kama kuna heshima amebaki nayo itakuwa katika nyumba yake, na kwa mantiki hiyo yeye sasa ni ''skunk'' , ajiuzulu
Kuhusu Media, Ndugai angesisitiza video nzima iwekwe, kaufanya hivyo kakimbilia msamahaMm ninachoamini ndugai mpaka ameomba msamaha kwenye hadhara lazima kuna watu walimfata na wakashauriana vizuri and I'm sure ndugai angejua mapema kuwa Rais atayaongea Yale aliongea juzi then asingeomba msamaha
Malalamiko ya yake ya media na mitandao hoja yake kubwa ni kuwa Ile clip imekatwa, haina mwanzo wala mwisho, maneno ambayo yamejaa ni Yale ambayo kila mtu kayasikia
Possible mwisho wa hotuba yake kuna Jambo la tofaut alisema
Bila shaka weye ni zao la shule za kata! kukariri kila kitu! km huyo aliye chana alikuwa kichaa je??Uswahilini kuna watu wanaamini kiongozi hatakiwi kuwa na mawazo binafsi
Akiunga mkono Rais anaitwa Zuzu, akitofautiana mawazo ajiuzulu
Spika kule Marekan alichana hadharan Hotuba ya Rais baada ya kuisha hotuba, ingekuwa huku ingeombwa apigwe kombora