Nashauri serikali itoe mikopo kwa wahitimu kupitia HESLB

Nao ujue walibebwa kabla ya kuwa hapo juu...kuna watu walitoa fedha zao kuwaweka hapo walipo...ebu tuwasaidie watu hawa.
Loan board ndio walitoa pesa kuwabeba Diamond? Tatizo Graduates wengi Zama hizi Ni majanga jitu linapewa Mkopo linaenda kununua iPhone, Lina mademu watano litabuni wazo la biashara au kilimo saa ngapi?
 
Habari,

Naishauri serikali kupitia bodi ya mikopo HESLB ianze kutoa mikopo kwa wahitimu wa vyuo vya elimu ya juu.
mkopo uwe wa fedha taslimu milioni tano 5,000000/=. Mkopo huo utolewe katika vigezo na mazingira yafuatayo:
  • Kabla ya kuhitimu kila mhitimu atatakiwa kubuni wazo la mradi ambao ataufanya mara amalizapo chuo.Wazo la mradi huo ataliwasilisha (present) kwa uongozi wa chuo chake...na uongozi wa chuo chake ukishalipitisha ... wazo hilo atalipeleka moja kwa moja kwenye bodi ya mikopo HESLB kuombea mkopo.Bodi ya mikopo itapitia wazo hilo la mradi na ikishalipitisha basi mwanafunzi huyo apewe mkopo huo
  • Mhitimu huyo pindi atakapopewa mkopo huo, ni sharti apewe supervisor (afsa biashara) kama ni wazo la kibiashara na (afisa kilimo) kama wazo linahusu kilimo
  • hitimu asipewe mkopo wote kwa mkupuo bali kwa awamu.Katika kutekeleza mradi wake mhitimu kupitia supervisor wake na mamlaka ya anapofanyia biashara atatakiwa kuwa anawasilisha taarifa ya maerndeleo ya mradi wake kabla ya kupewa fedha za awamu nyingine.
  • Mhitimu atatakiwa kubaki chini ya usiimamizi mpaka pale mradi wake utakapokuwa stable na kuhakikisha amerejesha fedha yote aliyokopa.
FAIDA ZA WAZO HILI
  • Itatengeneza sprit ya kujiajiri kwa wasomi wetu.
  • italeta creativity kwa wasomi wetu kwani akili na maarifa yao itakuwa inawaza project gani unique wafanye pindi wamalizapo chuo.
  • Tatizo la ajira litapungua kwakiasi kikubwa.
  • bodi ya mikopo HESLB itafanikiwa kwakiasi kikubwa kurejesha fedha zake kwani wahitimu wengi watakuwa na uwezo wa kurejesha mikopo yao kuliko ilivyo sasa.
THANK YOU
Hili WZO NI ZURI,.linaw3za boreshwa:-

Kwasasa vyuo baadhi vina kitengo cha kulea wanafunzi wajariamali, kinachiweza fanyika hawa wajaria mali ambao ni best wamelelewa vizur kwa kipind cha miaka miwili au mmoja, tubaki na vyeti vyao kisha wapewe mkopo wa kuendeleza biashara mara tu wanapo maliza chuo, vyeti vyao watapewa baadae baada muda maalum mfano miaka miwili au mitatu
 
Hili WZO NI ZURI,.linaw3za boreshwa:-

Kwasasa vyuo baadhi vina kitengo cha kulea wanafunzi wajariamali, kinachiweza fanyika hawa wajaria mali ambao ni best wamelelewa vizur kwa kipind cha miaka miwili au mmoja, tubaki na vyeti vyao kisha wapewe mkopo wa kuendeleza biashara mara tu wanapo maliza chuo, vyeti vyao watapewa baadae baada muda maalum mfano miaka miwili au mitatu
point mkuu...
 
Diamond & Harmonize hawaijui hata hiyo HESLB na Ni mabilionea kwa sasa. "Wasomi" mnaleta blah blah la mkopo waoneeni huruma wadogo zenu angalau nao wapate japo kusoma Elimu ya Juu kwa mikopo mtakayorudisha
Wote hatuwezi kuwa wanamuziki! Nchi inamahitaji mengi ikiwemo pia na vyanzo vya burudani. 'Dia' na 'Har' nao wanatekeleza jukumu lao la uzalishaji burudani.
 
Back
Top Bottom