Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Mbona Daraja la Busisi linakaribia kuisha.Kwa mujibu wa Nape Nnauye nchi yetu inatumia shilingi bilioni 800 kwa mwezi kulipa madeni. Halafu shilingi bilioni 600 hutumika kila mwezi kulipa mishahara ya watumishi serikalini.
Lkn makusanyo kwa mwezi ni kati ya trilioni 1.2 - 1.3 kwa mwezi. Hivyo fedha hazitoshi kuendelea na miradi yote hiyo. Tunapaswa kama taifa kuachana na miradi mikubwa isiyo kuwa na tija.
1. Daraja la Busisi tuachane nalo kabisa. Kwasbb halitarajiwi kuleta tija yoyote ya kiuchumi hata likikamilika maana linaenda kijjjini (interior) Busisi. Mabilioni ya fedha yatapotea bure kabisa!
2. Ujenzi wa makao makuu Dodoma usitishwe hadi hapo serikali itakapokuwa na uwezo wa kifedha.
3. SGR iishie Morogoro hapo hapo panatosha. Awamu ya 8 itakuja kuendeleza kutoka Morogoro kwenda mbele.
4. Ndege zilizonunuliwa zinatosha. Ndege 5 ambazo ziko kwenye mpango wa kuongezwa ifikapo 2023 tuachane nazo.
N.B. JNHPP ndiyo mradi pekee ambao inabidi tuendelee kupambana nao kwa sasa maana karibia utakamilika. Japo kuna changamoto ya tabia nchi
Natanguliza shukurani endapo ushauri wangu utafanyiwa kazi.
Mbona SGR inakaribia Makutupora ya Singida na nyingine imeanzia Mwanza kuelekea Isaka.
Mbona Serikali nzima ipo Dodoma na Mji wa Magufuli unaendelea kukamilishwa.