Nashauri Serikali isitishe ujenzi wa daraja la Busisi, SGR na Makao Makuu Dodoma

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,563
50,406
Kwa mujibu wa Nape Nnauye nchi yetu inatumia shilingi bilioni 800 kwa mwezi kulipa madeni. Halafu shilingi bilioni 600 hutumika kila mwezi kulipa mishahara ya watumishi serikalini.

Lakini makusanyo kwa mwezi ni kati ya trilioni 1.2 - 1.3 kwa mwezi. Hivyo fedha hazitoshi kuendelea na miradi yote hiyo. Tunapaswa kama taifa kuachana na miradi mikubwa isiyo kuwa na tija.

1. Daraja la Busisi tuachane nalo kabisa. Kwasbb halitarajiwi kuleta tija yoyote ya kiuchumi hata likikamilika maana linaenda kijjjini (interior) Busisi. Mabilioni ya fedha yatapotea bure kabisa!

2. Ujenzi wa makao makuu Dodoma usitishwe hadi hapo serikali itakapokuwa na uwezo wa kifedha.

3. SGR iishie Morogoro hapo hapo panatosha. Awamu ya 8 itakuja kuendeleza kutoka Morogoro kwenda mbele.

4. Ndege zilizonunuliwa zinatosha. Ndege 5 ambazo ziko kwenye mpango wa kuongezwa ifikapo 2023 tuachane nazo.

N.B. JNHPP ndiyo mradi pekee ambao inabidi tuendelee kupambana nao kwa sasa maana karibia utakamilika. Japo kuna changamoto ya tabia nchi

Natanguliza shukurani endapo ushauri wangu utafanyiwa kazi.

UPDATES; .....,.....................................
Kuna utetezi dhaifu Sana kwamba daraja la Busisi linaunganisha nchi za Rwanda na Burundi. Kigoma wasemeje Sasa?

Hata kwa upande wa SGR.
40% ya miizigo toka bandari ya DSM inasafirishwa kupitia Kigoma. Mwanza inapitisha 10% tu. Kulikuwa na sababu gani ya kupeleka SGR Mwanza badala ya Kigoma? Jibu ni moja tu....ukabila na upendeleo.
 
Nyinyi na huyo bibi ako Samia mmeshafeli mnatapatapa daraja la Busisi linaenda kijijini akili yako imejaa kamasì! Si mulimuona Magufuli hafai amewaachia muendelee na Msoga wenu!
Binafsi sioni tija yoyote kutumia mabilioni ya shilingi kujenga daraja kwenda Busisi. Kiuchumi hailipi. JPM alipumbazwa na upendeleo wa ukabila.
 
Binafsi sioni tija yoyote kutumia mabilioni ya shilingi kujenga daraja kwenda Busisi. Kiuchumi hailipi. JPM alipumbazwa na upendeleo wa ukabila.
Hata Busisi hupajui unapayuka hapa tù! Hivi kisa kwa wasukuma Roho zinawauma? Hujui kuwa Mwanza anakua kwa kasi na inaifatia Dar kiuchumi? Au wangejenga Dar au kaskazini ungekuwa unachekelea hapa! Mbona hujazungumzia daraja la mto Wami kusitishwa?
 
Acha tufe njaa, hii miradi iendelee hakuna namna, tulishaianza lazima iishe hatuwezi kulaza hela...haijalishi aliyeanza alipatia au alikosea..

Hawa akina Nape ni vibaraka kupenyeza agenda za watu wapate kuishi, kwa serikali kusupply hela huko means wao hawana kitu na miradi mipya itabidi isubiri..

Mama malizia viporo, achana na hizi kelele za wafukuza upepo....mengine tutafanya tu mbele huko, wewe tukamue mpaka damu zitoke viporo viishe tuanze mengine. Mipango ha Mungu huwa ni mingi, tumalize tulichoanza hatutaki biashara ya kulima hapa na pale kila siku...
 
Agenda ya Nape ni vingine viachwe akili ihamie kwenye gas Kusini ishine...hatukatai kusini nao wanahaki lakini kama nchi hatuwezi kuwa tunateketeza hela na kuacha viporo kila uchwao.

Kwa sasa aacha makampuni ya Oil and gas yaje yaendelee na uchunguzi, acha investimeny nyingine kama ujenzi wa viwanda na zile projects ambazo serikali haitoi hela mfukoni, kuwa makini pia kwenye kutoa favor kwenye uwekezahi huku unasahau watu wako...
 
Kwa mujibu wa Nape Nnauye nchi yetu inatumia shilingi bilioni 800 kwa mwezi kulipa madeni. Halafu shilingi bilioni 600 hutumika kila mwezi kulipa mishahara ya watumishi serikalini...
Du, hakika ni hoja fikirishi zizizo na mashiko.

Unadai Tunapaswa kama taifa kuachana na miradi mikubwa isiyo kuwa na tija, wakati hutaji ni tija gani haitapatikana miradi ikikamilika.

Naamini wewe ni msomi hivyo unajua vichochea uchumi (economic drivers)
 
Point of correction - Daraja haliendi Busisi, daraja linajengwa sehemu inaitwa Busisi na magari yanayopita hapo yanaweza kwenda hadi Burundi, Rwanda na Uganda.
Hapo panapojengwa daraja kuna kivuko kinachotumia muda kuvusha magari machache kwa wakati. Magari hayo ni pamoja na ya mizigo kwenda na kutoka nchi za jirani ulizozitaja
 
Hata mkisitisha miradi yote bado hali itakuwa MBAYA SANA, kwa muelekeo huu wa wafanyabiashara wakubwa kukwepa kodi na matumizi ya ovyo ya serikali...watu tunajiuliza convoy nzima iliyoambatana na Rais kwenda Misri walikwenda kufanya nini, hadi Ndalichako! Siku si nyingi na na mishahara itakosa kwa watumishi.
 
Back
Top Bottom