Nashauri Serikali iajiri Walimu wenye ufaulu wa daraja la kwanza au la pili kwenye vyeti vya elimu ya sekondari(Kidato cha nne na sita)

Hashimu lwenje,

Una div two unaandika upupu wa aina hii. Tambua kwanza hao waliosomea ualimu ndio hao wanaofundisha shule za private unazosifia na wengine wanafundisha part time private wakiwa wameajiriwa serikalini.

Kama hujui pia kuanzia mwaka 2015 sifa za kujiunga ualimu zimebadilika, diploma na certificate ya ualimu unaingia ukiwa na div one hadi three pekee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uko sahihi ila wale waliochemka kupata div 1 na 2...watapinga!!
 
Hapo uliposoma kwenye four passes umeona kuna Education(Ualimu).
Hata zamani kada zingine ilikuwa four passes ila Ualimu ilikuwa mwisho division four ya 28(yaani Seven passes) sasa wewe sijui umeona wapi?

Mimi naweza kuleta ushahidi hapa hakuna mtu anasomea Ualimu kama hana division one hadi three.
Kwa kada zingine zote ni four passes.
Wanaruhusiwa mkuu. Check qualifications. Wanataka five passes na kuendelea. Haijalish una division gan

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kuelewa kitu kunatokana na utayari wa mjifunzaji..afu pia mwl habebi maarifa aliyo nayo na kuyaingiza kichwan mwa mjifunzaji bali anamuwezesha mjifunzaji kuelewa ..
 
Mkuu mdogo wangu ana division 3 lakini kwenye hesabu B physics B je huyu nae pamoja na three yake ni kilaza?
 
Nimechoka sana baada ya kusoma andiko la mtoa HOJA, nakumbuka mwaka 2004 nilipohitimu kidato cha nne baada ya kutoka matokeo ya kidato cha nne nilienda kuangalia matokeo husika katika shule ya sekondari AZANIA

Kwa wale waliosoma na kahitimu kidato cha nne miaka hiyo watakumbuka mfumo huo wa kuangalia matokeo, tulipofika pale na baada ya kuangalia matokeo kwenye mlango wa kutokea kulikuwa na walimu wanne wa Shule ya FEZA BOYS walikuwa wanauliza umepata division gani kwenye matokeo yako ukiwambia una division three au two walikuwa wana kwambia Kwa heri

Ila kwa wale waliokuwa na division one walikuwa wanachukua information zako na kukuahidi kwamba kuna shule yetu tunataka kuianzisha tunaomba mawasiliano ya mzazi /mlezi wako kwa ahadi ya kusomeshwa bure kwenye shule yao na ni kweli waliwachukua wanafunzi wengi wenye ufaulu wa division one na matokeo ya kidato cha Sita ya mwaka 2007 ambayo ndo yalikuwa ya kwanza kwa shule hiyo yalikuwa mazuri sana na ndiyo yaliyoiweka kwenye RAMANI ya ubora wa shule hiyo, hivyo dhana kusema kwamba shule za PRIVATE inachukua wanafunzi wasio na uwezo sio sahihi kabisa
 
Bado na stress za nyumbani na mtaani, kufaulu pia ni kazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanajiitaga walimu wa sayansi na namna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata maslahi yakiongezwa tatizo litabaki kuwa stereotyping, walimu wanachukuliwa kama watu waliofeli ila walimu waliopata I & II wapo wengi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ulichokisema ni kweli

Mwanafunzi gani aliepata one alieenda kusoma ualimu kwa mapenzi yake mwenyewe?

Ni aidha,alikua anataka mkopo au alikosa kozi alizozipenda
Sema utapingwa sana lakini ilitakiwa iwe MWIKO kwa mwanafunzi mwenye 3 na kushuka chini kusomea ualimu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ajira ndugu wanasema Bora kazi watoto mtoto wa mkulima hana jinsi na ndio waliowengi ...ukiwa na pesa mwanao akizungusha dv4 atasoma tu ,mbona vyuo n vyingi mno na koz nzuri n nyingi atapelkwa private universty, nasio pangu pakavu ndo maana wanasema ajira za ualim n kimbilio hasa kwa watoto maskini hawana njia nyingine...Kama umepat baht yakusoma private school washukur wazaz wako nasio kukejer wezio Hali halis ndio hiyo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…