Nashauri kazi ya kukusanya taarifa binafsi za watalii ibaki kwa wizara ya mambo ya ndani (Immigration)

Nashauri kazi ya kukusanya taarifa binafsi za watalii ibaki kwa wizara ya mambo ya ndani (Immigration)

Mparee2

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2012
Posts
3,288
Reaction score
5,762
Kuna hizi taasisi zetu kubwa kama TANAPA/NCAA/WMA nk wameboresha mifumo yao na kuhusisha kukusanya taarifa binafsi za MTALII zilizopo kwenye Passport yake kabla hajafika Nchini.

Nafikiri ifike mahala hayo majukumu yaachiwe Idara husika ambayo ni ya mambo ya ndani kwani sioni kwa nini Kampuni za wageni zilazimishwe kutafuta taarifa binafsi za wageni na kujaza kwenye mifumo (portal) za utalii wakati wageni wakiingia mipakani wataacha taarifa zao binafsi zote.

Labda tu niwakumbushe kuwa; kwa wenzetu (Wazungu) hawapendi kabisa kutoa taarifa zao binafsi za passport kwani Ile passport ina maelezo yake yote na wahalifu wa kimtandao wakizipata taarifa zake wanaweza hata kumuibia hela kwenye account zake na ndio sababu wazungu, hasa wale wanaojiweza hawapendi kabisa kutoa passport zao hovyo hovyo pengine watoe tu sehemu ambayo ni very secured kama mipakani na sio kila pahala.

Fikiria mgeni amefanya booking online hata kampuni haijui vizuri halafu TANAPA/NCAA wanashinikiza atume copy ya passport yake ili kupata maelezo yake binafsi?

Nafikiri TANAPA/NCAA/WMA nk wanachohitaji ni kupata takwimu mfano; Wanaume/Wanawake/ Watoto/na Nchi walikotoka na kama kuna ulazima wa kuwa na hizo taarifa binafsi za WATALII, kuna option mbili ambazo zikitumika zinaweza kuondoa huo ukakasi...
1. Waunganishe mfumo wao usomane na wa Immigration(Uhamiaji)
2. Waweke mashine za kuscan Passport kwenye malango ya kuingia kwenye Vivutio ili taarifa binafsi za mgeni ziingie moja kwa moja kwenye portal yao bila kumuhusisha tour operator.
NI VIZURI MASHIRIKA YETU YAWE YANAFIKIRIA NAMNA YA KURAHISISHA HUDUMA ZAO NASIO KINYUME CHAKE!
 
Kwani Denis robati anasemaje kuhusu hili,🤔
 
Nafikiria serikali ambao ndoo wahusika wapo humu ndani,
 
Back
Top Bottom