Tumekubaliana tuache kulialia na kulalamika. Hata kama amefanya unachoita ni mistake ila kiukweli ametimiza wajibu wake.
Kusema ametimiza wajibu wake ni kujipa moyo tu, ki ukweli Jasusi mbobevu kama Polepole, anayejua gharama za kuasi kambi za kijasusi hakutakiwa kufanya jambo la hatari namna ile.
Kuwaamini wazee wanaohesabu siku zao za kuishi lilikuwa kosa la kwanza, halafu kosa la pili lilikuwa ni timing. Kama aliamua kujitoa muhanga (baada ya kukosa walinzi pamoja na backup) angevuta muda wa kujilipua kusubiri wiki hii ya mwisho ili awapanikishe vizuri hao wanamtandao
Ona sasa, wanamtandao wanavyofanya cameback ya kibabe wiki hii kwa kuteka mitandao na mabonanza yasiyoeleweka eleweka kila wilaya na mbaya zaidi hizi mechi za CAF zimekuja kuwaboost zaidi. Lakini wakati wa Polepole na Gwajima, hakuna cha Simba wala Yanga kilichoweza kuhamisha focus ya watu.
Hawa kina mange wana influence kwa watu wa kawaida sana halafu wanahoja moja tu inayowasaidia kujenga hoja, miamala ya benki na umiliki wa magari!!
Polepole na Gwajima ambao wote kwa pamoja hatujui huko waliko kama wamezikwa kwa heshima au wametupwa bwawani, impact yao ilikuwa kubwa sana kwasababu pia ni watu waliokuwa wanaaminika na wengi na watu wasingeona tabu kuwatumia kama refference.
Wapumzike kwa amani (ukweli binafsi nilishakata tamaa ya kuwaona tena zaidi ya kuwaombea kwa Mungu) Polepole na Gwajima angalau wameuchangamsha uchaguzi wa mwaka huu!! Mamlaka hazitawasahau na hata wananchi wengi kwa sirini na hadharani wameuona mchango wao, wamewafumbua macho na kuwapa ujasiri.
Hata kina Mkwawa walianzisha mapambano na wakoloni lakini waliokuja kuikomboa nchi ni kina Kambarage Nyerere yule mjukuu wa Burito.
Mbegu waliyoipanda Polepole na Gwajima ipo siku itamea na kuzaa matunda