Barbarosa
JF-Expert Member
- Apr 16, 2015
- 22,584
- 27,786
Wana MMU....
Kwa heshima na taadhima bila taraghani wala tahanani naomba mniweke kwenye sala zenu ili safari yangu iwe ya mafanikio.
Ni ombi la dhati kabisa na nawasihi msilichukulie kuwa takriri wala tashtiti za Ngabu.
Hii si mara yangu ya kwanza kujaribu bakhti yangu katika medani za wapendanao.
Miaka takriban hamstaashara ilopita nilijaribu lakini mambo yakaenda mramba.
Sasa napiga tena moyo konde nijaribu nione.
Naomba niwashirikishe kwa picha mtiririko wa safari yangu kuanzia Ubungo hadi Ikungulyabashashi....karibuni sana.
Safari ni hatua na yangu ilianza jana saa kumi na mbili asubuhi pale Ubungo....
View attachment 366753
Mishale ya saa tano hivi tukaigongea hodi Morogoro.....mimi huyo hapo naongea na mchepuko kwenye simu.
View attachment 366754
Shinyanga tukaingia usiku....nikalala hapo hapo stendi kwenye vibanda na asubuhi nikajidamka na kupanda Ally's hadi Ikungu....
View attachment 366755
View attachment 366756
Hatimaye majira ya alasiri nikakanyaga nyumbani Ikungulyabashashi...
View attachment 366758
Karibuni nyumbani. Karibuni sana. Na karibuni wanzuki.
Hii Wazungu wanaita ,,midlife crisis" hakuna kingine!