Napinga mchakato wa kupata katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2025, Watanzania tukatae maigizo ya wanasiasa. Imetosha

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
56,607
93,386
Bila kutumia Maneno mengi wote tunajuwa mabilioni ya pesa za walipa kodi yalivyohujumiwa na wanaccm kukwamisha katiba pendekezwa ya tume ya Warioba.

Sasa kuna wanasiasa wanadhani tumesahau au sisi ni wajinga, eti wanataka katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2025 halafu bunge hili la DP ndio ligeuke kuwa ubunge maalum la katiba na kuongezewa idadi kidogo ya uwakilishi wa makundi unategemea nini?

Yani huku kuna Kibajaj huku kuna Msukuma, huku babu Tale mnakwenda kujadili katiba ipi? fuatilieni mjadala wa bajeti jumatatu wote mtakubaliana na Mimi na kuniunga mkono ni kwamba hatuna bunge.

Sasa wazalendo wa kweli tusikubali pesa zetu kuhujumiwa tena kwenda kulipana posho kwa mchakato hewa.

Tusubili uchaguzi ambao nina uhakika kwa viwango vyovyote vile watapatikana wabunge wenye uwiano na wababaishaji karibu wote si rahisi kurudi bungeni hapo ndio mtuletee bunge la katiba lakini kwa sasa tukatae huu ubabaishaji na hadaa za Ccm ambazo viongozi wa upinzani bado hawajauona mtego uliopo mbele yao.

Natoa hoja.
 
Naunga mkono hoja maana tuki rush Ili tuu Wanasiasa wa upinzani wapate upenyo itakuwa ni Katiba ya Vyama vya siasa sio Katiba ya Wananchi na itakuwa mbovu kuliko ya Wakenya...

Katiba Mpya ni baada ya Uchaguzi,ukiona chadomo wanang'ang'ania ujue wanatafuta ulafi wa madaraka Kwa maslahi binafsi na sio maslahi ya Umma.
 
Siyo kwa bunge hili lililojaa vilaza

Ova
Ukiona bunge limejivika jukumu la serikali kiasi kwamba waziri hana tena kazi ya kutetea hoja za serikali ni hatari sana.

Swala la katiba mpya lisubiri kwanza siyo kwa bunge hili.
 
ukiona chadomo wanang'ang'ania ujue wanatafuta ulafi wa madaraka Kwa maslahi binafsi na sio maslahi ya Umma.
Siyo upinzani tu, hata ccm ukiona wanang'ang'ania hii katiba ya sasa, ujue wanasukumwa na ulafi wa kupata madaraka bila kura halali za wananchi.
 
Ccm wamekubali ila Hawataki Katiba ya kipuuzi so why kuharakisha wakati wamesema wako tayari Katiba iandikwe?
 
Naunga mkono hoja maana tuki rush Ili tuu Wanasiasa wa upinzani wapate upenyo itakuwa ni Katiba ya Vyama vya siasa sio Katiba ya Wananchi na itakuwa mbovu kuliko ya Wakenya...

Katiba Mpya ni baada ya Uchaguzi,ukiona chadomo wanang'ang'ania ujue wanatafuta ulafi wa madaraka Kwa maslahi binafsi na sio maslahi ya Umma.
Aisee, we jamaa unatumia nini kuwaza? Ndio kushibishwa na buku saba za Lumumba Str?

Ukiusema upinzani, huku unafumbia macho ule uozo wa ccm pale Dodoma unakuwa hutendi haki, hatuna bunge, hatuna wabunge wa kutuletea katiba mpya, bunge lenye mrengo mmoja haliwezi kutupatia katiba ya wananchi.

Umekalia uccm tu ndezi we!!
 
Bila kutumia Maneno mengi wote tunajuwa mabilioni ya pesa za walipa kodi yalivyohujumiwa na wanaccm kukwamisha katiba pendekezwa ya tume ya Warioba.

Sasa kuna wanasiasa wanadhani tumesahau au sisi ni wajinga, eti wanataka katiba mpya kabla ya uchaguzi wa 2025 halafu bunge hili la DP ndio ligeuke kuwa ubunge maalum la katiba na kuongezewa idadi kidogo ya uwakilishi wa makundi unategemea nini?

Yani huku kuna Kibajaj huku kuna Msukuma, huku babu Tale mnakwenda kujadili katiba ipi? fuatilieni mjadala wa bajeti jumatatu wote mtakubaliana na Mimi na kuniunga mkono ni kwamba hatuna bunge.

Sasa wazalendo wa kweli tusikubali pesa zetu kuhujumiwa tena kwenda kulipana posho kwa mchakato hewa.

Tusubili uchaguzi ambao nina uhakika kwa viwango vyovyote vile watapatikana wabunge wenye uwiano na wababaishaji karibu wote si rahisi kurudi bungeni hapo ndio mtuletee bunge la katiba lakini kwa sasa tukatae huu ubabaishaji na hadaa za Ccm ambazo viongozi wa upinzani bado hawajauona mtego uliopo mbele yao.

Natowa hoja.
Rasimu ya Warioba inatosha. Itumiwe.
Kama hawaitaki wasubiri kwa sababu za mtoa mada kuwa Bunge kwa sasa ni kama HAKUNA!
 
Back
Top Bottom