Salaam, Shalom,
Mmoja kati ya wazee wazalendo waliobaki nchini, Mzee Joseph Butiku, ameendelea kuwaasa wanasiasa wote Wanaopuuza umuhimu wa KATIBA mpya kuacha ubinafsi na kuthamini UTU.
Ikumbukwe pia, mwezi Octoba, aliyekuwa Waziri mkuu Awamu ya Pili, Mzee Joseph WARIOBA alipokuwa katika mahojiano katika kipindi Cha DAKIKA 45, ITV, Alipendekeza pia kuwa, ni vizuri Katiba mpya ikapatikana kabla ya Uchaguzi 2025. Na muda uliopo unatosha ikiwa tutaanza ilipoishia Tume aliyoisimamia kabla.
Wanasiasa wanatakiwa kuthibitisha kuwa Wana UTU na kuhakikisha wanatoa ushirikiano kuhakikisha tunapata Katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi kabla ya Uchaguzi wowote.
Wazee ni hazina, Tuwatumie.
Na hiyo ni message Kwa kijana wa chama kuwa kamwe wazee hawawezi kunyamaza na kuacha Kutoa maoni kulisaidia Taifa Kwa kisingizio Cha "KUSTAAFU".
Source: The Chanzo tv
Karibuni🙏