Napendekeza ukumbi wa 'Karimjee' ubadilishwe jina

Ukisikie Laana za Mungu zinavoanza kuikumba nchi... basi ni kwa njia hizi za kuvamia mali za watu na kujipandikizia majina feki na ubini bandia..... "bado hayawatoshi mlivyoiba na kutaifisha majengo/viwanda mashamba /mashule /mahoteli na hospitali ya waASIA na wazungu... balaa lote mulionalao la kimaisha hivi sasa ni moja za sababu ya udhalimu na ujanja wakunyakuwa HAKI za watu.... pyuuuuuufff

UMESEMA KWELI TUPUUUU !!!!
 
Hakuna lazima, jengo hilo lilitolewa bure kuwa ukumbi wa bunge Karimjee na vile vile Karimjee alikuwa ni spika wa bunge la kwanza la uhuru wa Tanganyika. Iwapo jina hilo ni kero, basi hata ule ukumbi wa Msekwa pale Dodoma pia ubadilishwe jina.
 
Mkuu, spika wa mwanzo sio Adam Sapi Mkwawa.
 
Saivi mtakula wa chuya Toyota importation mmepigwa chini serikali inaagiza yenyewe directly from Japan.
Mkuu, mie nakereka mno na hii dhana tuliyopandikizwa ya 'inferiority complex'. Watu hawataki kujiona wanaweza kwani kabla ya Mwingireza kuja hawa jamaa zetu toka Asia walikuwepo wengi hivo? Kila ukisema sisi tunaweza bila wao utasikia "huo ni ubaguzi"! Shame on them.
 
Watanzania wenye asili ya India tupo nao miaka yote na ni 'wahapahapa'. Pamoja na mapungufu yao, ni vyema tukawaenzi kwa juhudi zao. Huwa najiuliza mara kwa mara kwanini hakuna wahindi wanaofanya kazi serikalini? Na kuna watu najua walikuwa wanatamani wawe hata wahadhiri wa vyuo lakini mfumo uliona hawatoshi.

Naamini sio kila mhindi anapenda kufanya biashara, wengine wangependa maisha ya kuajiriwa na kutumikia serikalini. Tuwape fursa na majengo kama Karimjee yawe ni alama ya kuwaenzi kwa mchango wao.
Japo lengo ya mada yangu haikuwa hii lakini niambie kama pana mchanganyiko wa watu wa aina tofauti Jamatini kama Misikitini na Makanisani.
 
Mkuu, spika wa mwanzo sio Adam Sapi Mkwawa.
Adam Sapi alipokea kiti kutoka kwa Karimjee mwaka 1962 baada ya nchi kuwa jamhuri na baraza la kutunga sheria kubadilishwa likaanza kuitwa Bunge! Kabla ya hapo lilikuwa linajulikana kama Legislative Council (LEGCO)- yaani baraza la kutunga sheria, na spika wake alikuwa Abdulkarim Yusufali Alibhai Karimjee ambaye aliliongoza kuanzia mwaka 1956 hadi December 1962 baada ya nchi kuwa jamhuri. Kwa vikao vya vyote baada ya uhuru mpaka Jamhuri vilifayika chini ya Karimjee.
 
Japo lengo ya mada yangu haikuwa hii lakini niambie kama pana mchanganyiko wa watu wa aina tofauti Jamatini kama Misikitini na Makanisani.
Hoja yako ni kwamba wao wanajibagua, hivyo ni sawa na wao kubaguliwa. Mimi naona wale wanaotaka kufanya kazi na serikali wapewe fursa. Tusiwahukumu wote kwa makosa ya wengine.
 
Mkuu, mie nakereka mno na hii dhana tuliyopandikizwa ya 'inferiority complex'. Watu hawataki kujiona wanaweza kwani kabla ya Mwingireza kuja hawa jamaa zetu toka Asia walikuwepo wengi hivo? Kila ukisema sisi tunaweza bila wao utasikia "huo ni ubaguzi"! Shame on them.
Tatizo ni HAO na SISI. Ukisha weka dhana hiyo basi ile dhambi ya ubaguzi itakuganda [kama alivyoasa Mzee JKN]
Kwenye umoja kuna SISI tuu.
 
Tatizo ni HAO na SISI. Ukisha weka dhana hiyo basi ile dhambi ya ubaguzi itakuganda [kama alivyoasa Mzee JKN]
Kwenye umoja kuna SISI tuu.
Mkuu, sio kila neno alilotamka JKN ni sahihi, kumbuka huyu alikuwa binadam na aliipenda sana imani yake. Lakini Wakristu wanaambiwa 'mpende jirani yako kama unavojipenda wewe mwenyewe'! Sasa kama huna UMIMI utampendaje mwenzio? Yakubidi ujitafakari wewe kwanza.
 
Adam Sapi alipokea kiti kutoka kwa Karimjee mwaka 1962 baada ya nchi kuwa jamhuri na baraza la kutunga sheria kubadilishwa likaanza kuitwa Bunge! Kabla ya hapo lilikuwa linajulikana kama Legislative Council (LEGCO)- yaani baraza la kutunga sheria, na spika wake alikuwa Abdulkarim Yusufali Alibhai Karimjee ambaye aliliongoza kuanzia mwaka 1956 hadi December 1962 baada ya nchi kuwa jamhuri. Kwa vikao vya vyote baada ya uhuru mpaka Jamhuri vilifayika chini ya Karimjee.
Kwa hiyo bado marehem Adam Sapi Mkwawa ndio spika wa kwanza wa BUNGE letu. Kumbuka Mwingereza aliwatumia sana (mpaka leo) hawa wadosi.Kumbuka kabla ya uhuru ilikuwa wa 1 mzungu wa 2 mdosi na wa 3 mwafrika.
 
Kama tulivozoea kuona majini ya vitu hasa yaliyokuwa yakitumika tokea enzi ya mkoloni yakibadilishwa, mie nimeonelea ni wakati muafaka wa ukumbi huu wa 'Karimjee' nao ubadilishwe na kuita ama 'BUNGE HALL' kwa kuweka kumbukumbu nzuri ya kikao cha kwanza cha bunge letu kufanyika hapo.

Kumbuka pana majina ya mitaa kama Pugu, City Drive, Independence Avenue n.k. yamebadilishwa hivo sioni tija ya jina la Karimjee hapa.
Wewe hujui hata hisani ? Huyu karemjee kaifanyia mengi nchii kuliko wewe na babu zako wooote mkiunganishwa
 
Colonel Middleton alijenga uwanja wa mpira Arusha na kuitwa jina lake
Aliutoa zawadi kwa iliyokuwa Arusha Town Ship Counsel
Wamefuta historia hii kwa kuita Sheikh Amri Abeid,mtu ambaye hakupendwa na wenyeji wa wakati huo kutokana na dini yake ya Qadiani
Wanaofuta historia hizo sijui huwa wanaangalia nini
 
What is Karimjee Jivanjee Family foundation and their doings

1. HISTORY

The Karimjee Jivanjee family came to Africa more than 200 years ago from Gujarat in India. We came as dhow traders from India to Zanzibar and established our business in Zanzibar in 1825.

Our business prospered and by 1920 we had expanded into Tanganyika. By 1950 the family was engaged in import and export trading, sisal and tea farming and sales and service of motor vehicles and motorcycles.

President Jakaya Kikwete (right) receives Karimjee Jivanjee family book from Hatim Karimjee, Chairman of Karimjee Jivanjee Ltd during a ceremony to launch the book in Dar es Salaam recently.
The Karimjee family established several charity trusts in the 1950’s and built many schools, hospitals and dispensaries and mosques and community centres. The most famous of these donations are; Karimjee Hall, Usagara Secondary School in Tanga (formerly Karimjee School), the Karimjee Clinic in Mnazi Moja, and the old Karimjee Hospital in Zanzibar. At the same time Karimjee gave scholarships to many Tanzanians to study overseas.

The charity trusts became less active after 1966/1969.

2. KARIMJEE JIVANJEE FOUNDATION

In 2009 the family decided to revive the charity trusts and registered the new Karimjee Jivanjee Foundation (KJF). KJF commenced operations in 2011.
KJF is funded by donations from Toyota Tanzania.

The mission of KJF is to invest in Education as a means to enhance the economic development of Tanzania. Tanzania faces many short term and long term socio- economic difficulties. The long term solution to many of these challenges is education.
Our strategy is to provide scholarships to Tanzanians to study in Tanzania, and to make improvements to various schools.
KJF has approximately 50 Scholars studying at graduate and post graduate level in Tanzania.
In addition to scholarships KJF provides donations to some schools to make improve
Basi libaki Karimjee Hall kwa mchango wa familia hii.Jamani Serekali ina wajibu wa kutukumbusha sisi na vijana historia hizi ili tuelewe Umuhimu wa kitu fulani. Asante sana jina libaki hivyo hivo. Bunge lebnyewe siku hizi linatuboa asbaadhi ya wabunge hawajielewi wanashusha hadhi ya Bunge!
 
Wewe hujui hata hisani ? Huyu karemjee kaifanyia mengi nchii kuliko wewe na babu zako wooote mkiunganishwa
Nimekuelewa sana mkuu. Babu zangu (naamini zetu) akina Isike, Milambo, Mkwawa (kuwataja wachache) si chochote kwa huyu jamaa!!!!!!? Sie ni watu wa ajabu kweli.
 
Colonel Middleton alijenga uwanja wa mpira Arusha na kuitwa jina lake
Aliutoa zawadi kwa iliyokuwa Arusha Town Ship Counsel
Wamefuta historia hii kwa kuita Sheikh Amri Abeid,mtu ambaye hakupendwa na wenyeji wa wakati huo kutokana na dini yake ya Qadiani
Wanaofuta historia hizo sijui huwa wanaangalia nini
Mkuu, ndio maana nimesema 'KWA TABIA HII YA KUFUTA FUTA MAJINA TULIYOYAKUTA' na yaliyozoeleka iendelee tu.
 
Back
Top Bottom