Aibu: Picha za Mameya wa jiji la Dar tokea Uhuru zimebandikwa ukumbi wa Karimjee isipokuwa ya Isaya Mwita

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,888
143,985
Nashindwa kuamini kabisa kuwa hii ndio chuki iliyopo katika siasa zetu.

Hapa ni Ofisi za Meya wa Jiji Karimujee hall Wamewaka Picha za Mameya wote Kabla ya Tanganyika Kupata Uhuru na baada ya Uhuru, Mpaka Meya huyu wa Sasa. Wanatambua Mameya wa Kizungu na Kihindi ila Wamegoma Kutambua Meya wa Chadema 2016 to 2020 Nchi hii inanuka Chuki na Ubaguzi

Karimjee.jpg


Ukumbi wa KARIMJEE upo jijini Dar es salaam ni Moja ya Ukumbi wa Miaka mingi toka Utawala wa Wakoloni.

Ukumbi huu umekuwa ukitumiwa na Waheshimiwa MADIWANI wa HALMASHAURI ya JIJI la Dar es salaam chini ya MSTAHIKI MEYA wa JIJI hili kwa VIKAO Vyao. KUTA za UKUMBI huu Zimepambwa Kwa PICHA za MAMEYA wote Waliohudumu ktk JIJI la Dar es salaam kama WASTAHIKI MAMEYA toka MEYA wa Kwanza wa JIJI hili ambaye alikuwa MZUNGU MKOLONI mpaka MEYA wa Sasa.

JAMBO la AJABU na KUSHANGAZA ni KUONDOLEWA kwa PICHA ya MSTAHIKI MEYA "Issaya MWITA" aliyehudumu kama MEYA wa JIJI kipindi cha UTAWALA KATILI wa AWAMU ya 5 na Kupelekea Kufanyiwa FIGUSI Meya ISSAYA MWITA na kuifunga OFISI yake ili ASIWE tena Meya na Kumweka MEYA mwingine kutoka Chama cha MAPINDUZI.

Wenye AKILI KUBWA tilijua zile FIGISU zilikuwa ni Chuki binafsi za yuke Bwana kwani Viongozi wengi wa CHADEMA walitakiwa Wahamie CCM ili kulinda NAFASI ZAO na Waliopinga kama MEYA ISAYA MWITA ndio Yaliwakuta ya kufungiwa OFISI na KUONDOLEWA.

Kabla ya Kufungiwa OFISI PICHA ya MSTAHIKI MEYA "ISSAYA MWITA" ilikuwa Imetundikwa kwenye UKUMBI wa KARIMJEE pamoja na Picha za Watangulizi Wake lakini LEO hii ile PICHA ile IMEONDOLEWA.

JE, walioondoa PICHA wanataka KUFUTA HISTORIA kuwa "ISAYA MWITA" hakuwa MEYA wa JIJI?

Ni upuuzi kuwa na MAWAZO hayo mbona PICHA za Wazungu Wakoloni zipo Mnaondoaje PICHA ya MTANZANIA mwenzenu kisa tu ni KUTOKA CHADEMA?

Mliotoa hiyo PICHA Acheni CHUKI zisizo na TIJA kwa TAIFA. Ukweli hamtaufuta kwa Kuondoa PICHA ya MEYA "ISAYA MWITA" bado MEYA "ISAYA MWITA?" Historia itamkumbuka tu kuwa Mwaka 2015 mpaka 2019 alikuwa MSTAHIKI MEYA wa JIJI la DAR ES SALAAM akitokea CHADEMA.
 
Nashindwa kuamini kabisa kuwa hii ndio chuki iliyopo katika siasa zetu.

Hapa ni Ofisi za Meya wa Jiji Karimujee hall Wamewaka Picha za Mameya wote Kabla ya Tanganyika Kupata Uhuru na baada ya Uhuru, Mpaka Meya huyu wa Sasa...
chuki ambazo hazina faida,akwezwaye atashushwa ipo siku.
 
Uhuni tu huu. Kwanini hakuna picha ya meya wa Chadema? Kama walijisahau warekebishe haraka.
 
yaani wameweka picha za wahindi na wazungu wakasahau picha ya nyani-ulaya mwenzetu kweli limagufool lilikokuwa likiipeleka nchi linajua lenyewe
 
yaani wameweka picha za wahindi na wazungu wakasahau picha ya nyani-ulaya mwenzetu kweli limagufool lilikokuwa likiipeleka nchi linajua lenyewe
Magufuli hivi bado yupo duniani hadi useme hivyo as if yeye ndiyo kawapa hiyo order.
 
11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom