Napendekeza ugali dagaa kuwa chakula cha taifa

Napendekeza ugali dagaa kuwa chakula cha taifa

Tule mahindi mabichi zaidi badala ya ugali
 
Woiii hamna kitu apo
Katika pitapita na ulizauliza zangu nimegundua hiki ni moja ya chakula kinachopendwa na wengi wa hadhi zote.

Mimi binafsi niko tayari kula ugali dagaa mwaka mzima bila kunikifu.

Sababu kuu ni unyumbulifu wa Dagaa wakati ugali unabaki vilevile bila kujali ni Dona, Sembe, Udaga au Mtama.

Dagaa ananyumbulika sana wakuu asikuambie mtu.

Mfano kuna

Ugali Dagaa wakukaanga wasio na mchuzi.
Ugali Dagaa wa Kukaanga amerostiwa
Ugali Dagaa wa kawaida walio na mchuzi.
Ugali Dagaa aliyetiwa nazi.
Ugali dagaa aliyetiwa karanga
Ugali Dagaa aliyechanganywa na mchicha au mboga nyingine ya majani.
Ugali Dagaa wabichi(Ambao hawajakauka) walioungwa
Ugali Dagaa Wabichi(Ambao hawajakauka) waliokaangwa bila mchuzi.
Ugali Dagaa Wabichi( Ambao hawajakauka) waliokaangwa na kuungwa na mchuzi
Ugali Dagaa wabichi (Ambao hawajakauka) Rost.
Ugali Dagaa wa Mayai.
Ugali Dagaa kachanganywa na Bamia

Wakuu hapa hazungumziwi Dagaa wa Baharini (Dagaa mchele/Uwono), Hapa anazungumziwa Dagaa kutoka katika ziwa safi na pendwa Victoria.

Ila Kuongezea na kutanua wigo zaidi

Ugali Dagaa Uwono wa Kuungwa
Ugali Dagaa Uwono wa kukaangwa bila mchuzi
Ugali Dagaa wa Kigoma
Ugali Dagaa wa Ziwa Nyasa

Napendekeza chakula hiki kifanywe chakula cha kitaifa, kama vazi la taifa mmeshindwa.

Naomba kuweka mezani hoja wajumbe yatari kwa kuungwa mkono au kupingwa kwa hoja.

Mukule kwa picha, hadi nimesikia njaa daah.

Ugali Dagaa

View attachment 1279943
View attachment 1279944
View attachment 1279945
View attachment 1279947
View attachment 1279948
View attachment 1279950

View attachment 1279951

VS Wali Harage (kiisiiimmmi)....

View attachment 1279953
View attachment 1279954
View attachment 1279955
View attachment 1279956
View attachment 1279957

Aahahahhahaa Wali ndondo....

Kama wametoka droo vilee..... Kama vipi ipigwe kolabo tuu....

Pilipili isikosekane tafadhali.

Matata the K.
 
Back
Top Bottom