Napendekeza ugali dagaa kuwa chakula cha taifa

Napendekeza ugali dagaa kuwa chakula cha taifa

Kasie,

Hapo naona BONDO tu hizo sukuma wiki sijui zege ah!!!! tena alieita Bondo ni puti kweli kweli kweli.
 
Msilinganishe vitu vingine na ugali, nenda ulaya tafuta hiyo kitu kama utaipata, na ukiupata ujue ni nadra sana, tena na dagaa ndio kabisa, ukiona mtu anasafiri na KLM na kapu la dagaa ujuwe hapo shughuli ipo.
tanzania mkuu sio chakula cha duniA
 
Hakuna kitu tamu kama kiporo cha ubwabwa na maharage (nazi iwekwe kwenye kimojawapo)...

Nakumbuka enzi zile za kusoma unarudi mchana kula kabla ya kwenda tena shule, hiyo makitu unaigonga na chai...

Ubweche maharage ni keki ya taifa na watu wote waseme amina...
 
Ugali dagaa 🙌🙌🙌

Heshima nakipa hiki chakula,utaniambia nini kwenye hiki chakula?

anaekula chakula kingine yani simuelewi kabisa yani,Bondo na dagaaa bana😋

Halafu ule hiki chakula kisha baby aanze jibebisha bebisha,ananrembulia rembulia

yani show ntayompa Hao wasafi festival na ndugu zake Fiesta wakasome😂


Ugali dagaa auweeee😋😋😋😋
 
Katika pitapita na ulizauliza zangu nimegundua hiki ni moja ya chakula kinachopendwa na wengi wa hadhi zote.

Mimi binafsi niko tayari kula ugali dagaa mwaka mzima bila kunikifu.

Sababu kuu ni unyumbulifu wa Dagaa wakati ugali unabaki vilevile bila kujali ni Dona, Sembe, Udaga au Mtama.

Dagaa ananyumbulika sana wakuu asikuambie mtu.

Mfano kuna

Ugali Dagaa wakukaanga wasio na mchuzi.
Ugali Dagaa wa Kukaanga amerostiwa
Ugali Dagaa wa kawaida walio na mchuzi.
Ugali Dagaa aliyetiwa nazi.
Ugali dagaa aliyetiwa karanga
Ugali Dagaa aliyechanganywa na mchicha au mboga nyingine ya majani.
Ugali Dagaa wabichi(Ambao hawajakauka) walioungwa
Ugali Dagaa Wabichi(Ambao hawajakauka) waliokaangwa bila mchuzi.
Ugali Dagaa Wabichi( Ambao hawajakauka) waliokaangwa na kuungwa na mchuzi
Ugali Dagaa wabichi (Ambao hawajakauka) Rost.
Ugali Dagaa wa Mayai.
Ugali Dagaa kachanganywa na Bamia

Wakuu hapa hazungumziwi Dagaa wa Baharini (Dagaa mchele/Uwono), Hapa anazungumziwa Dagaa kutoka katika ziwa safi na pendwa Victoria.

Ila Kuongezea na kutanua wigo zaidi

Ugali Dagaa Uwono wa Kuungwa
Ugali Dagaa Uwono wa kukaangwa bila mchuzi
Ugali Dagaa wa Kigoma
Ugali Dagaa wa Ziwa Nyasa


Napendekeza chakula hiki kifanywe chakula cha kitaifa, kama vazi la taifa mmeshindwa.

Naomba kuweka mezani hoja wajumbe yatari kwa kuungwa mkono au kupingwa kwa hoja.

Mukule kwa picha, hadi nimesikia njaa daah...

Ugali Dagaa...

View attachment 1279943
View attachment 1279944

View attachment 1279945

View attachment 1279947

View attachment 1279948

View attachment 1279950

View attachment 1279951

VS Wali Harage (kiisiiimmmi)....

View attachment 1279953

View attachment 1279954

View attachment 1279955

View attachment 1279956

View attachment 1279957

Aahahahhahaa Wali ndondo....

Kama wametoka droo vilee..... Kama vipi ipigwe kolabo tuu....

Pilipili isikosekane tafadhali.

Matata the K.
Post yako mtu akiisoma kwa haraka anaweza hisi umeandika kiutani utani, ila ndani yake kumbe kuna maana kubwa......hahhaahhaaaa mimi naunga mkono hoja
 
Back
Top Bottom