Serikali igawe chakula

BabaMorgan

JF-Expert Member
Dec 18, 2017
4,050
10,495
Kama unakula milo mitatu basi itakuwa changomoto kuelewa hichi nachoandika tena utaona ni hoja ya kipuuzi.

Tuendelee baadhi ya watu ukiwaambia kuna Watanzania wenzetu wanakufa kwa njaa hawawezi kuamini ndio yale ya aliyeshiba hamjui mwenye njaa.

Mimi kama mpiga kura ambaye kura yangu ni miongoni mwa kura zilizoipa ushindi serikali ya CCM napenda kuiomba serikali ianze kugawa chakula kwa wananchi wake.

Approach ya ugawaji wa chakula iwe kama ifuatavyo waanze kugawa chakula mashuleni kwa maana mtu mzima anaweza kuvumilia njaa ukilinganisha na mtoto kwani hii italeta impact nzuri hususani kwenye mahudhurio na kupunguza tatizo la udumavu kwa watoto. Mfano break ya saa nne asubuhi watoto wapewe kikombe cha uji na maandazi mawili huku break ya mchana wapewe Ugali maharage, dagaa pamoja na mboga za majani.

Ugawaji wa chakula kwa watu wazima yaani 18+ ni kama ifuatavyo maandiko ya dini yanasema asiyefanya kazi na asile utaratibu utakuwa kufanya usafi mita moja ya barabara kwa chai asubuhi ambayo napendekeza ingekuwa chai na sahani moja ya makande au wali huku mchana ni kusafisha mifereji kwa mita mbili ambapo mtu akikamilisha anapewa ugali, dagaa, maharage na mboga za majani huku atakayetaka chakula usiku basi atafagia stendi au vituo vya daladala huyu atapewa wali maharage na ndizi moja ya kuiva.

Impact yake itakuwa kupunguza rate ya watu wanaolala njaa sorry tunaolala njaa na wakati huohuo kuwa na mazingira safi sasa kuna watu watahoji budget ya hicho chakula itatoka wapi my dear friends serikali haishindwi na kitu ni ishu ya vipaumbele.
 
Naongea kama Mpiga kura ambae napata mlo Moja! Lkn bro wapi hapo watu wanakufa njaaa?
 
Nenda ukapate hifadhi ya mahabusu huko utakula BURE asubuhi uji mchana ugali na haragwe na kazi zipo za kutosha tu Mpaka utachoka mwenyew Sana Sana waombe wakupeleke kwenye magereza ya kilimo mfano IDETE la morogoro pale,,
 
Nenda ukapate hifadhi ya mahabusu huko utakula BURE asubuhi uji mchana ugali na haragwe na kazi zipo za kutosha tu Mpaka utachoka mwenyew Sana Sana waombe wakupeleke kwenye magereza ya kilimo mfano IDETE la morogoro pale,,
Fikra zako ni udumavu uliochangiwa na uhaba wa chakula
 
Back
Top Bottom