Napendekeza ugali dagaa kuwa chakula cha taifa

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
6,544
15,215
Katika pitapita na ulizauliza zangu nimegundua hiki ni moja ya chakula kinachopendwa na wengi wa hadhi zote.

Mimi binafsi niko tayari kula ugali dagaa mwaka mzima bila kunikifu.

Sababu kuu ni unyumbulifu wa Dagaa wakati ugali unabaki vilevile bila kujali ni Dona, Sembe, Udaga au Mtama.

Dagaa ananyumbulika sana wakuu asikuambie mtu.

Mfano kuna

Ugali Dagaa wakukaanga wasio na mchuzi.
Ugali Dagaa wa Kukaanga amerostiwa
Ugali Dagaa wa kawaida walio na mchuzi.
Ugali Dagaa aliyetiwa nazi.
Ugali dagaa aliyetiwa karanga
Ugali Dagaa aliyechanganywa na mchicha au mboga nyingine ya majani.
Ugali Dagaa wabichi(Ambao hawajakauka) walioungwa
Ugali Dagaa Wabichi(Ambao hawajakauka) waliokaangwa bila mchuzi.
Ugali Dagaa Wabichi( Ambao hawajakauka) waliokaangwa na kuungwa na mchuzi
Ugali Dagaa wabichi (Ambao hawajakauka) Rost.
Ugali Dagaa wa Mayai.
Ugali Dagaa kachanganywa na Bamia

Wakuu hapa hazungumziwi Dagaa wa Baharini (Dagaa mchele/Uwono), Hapa anazungumziwa Dagaa kutoka katika ziwa safi na pendwa Victoria.

Ila Kuongezea na kutanua wigo zaidi

Ugali Dagaa Uwono wa Kuungwa
Ugali Dagaa Uwono wa kukaangwa bila mchuzi
Ugali Dagaa wa Kigoma
Ugali Dagaa wa Ziwa Nyasa

Napendekeza chakula hiki kifanywe chakula cha kitaifa, kama vazi la taifa mmeshindwa.

Naomba kuweka mezani hoja wajumbe yatari kwa kuungwa mkono au kupingwa kwa hoja.

Mukule kwa picha, hadi nimesikia njaa daah.

Ugali Dagaa

images (2).jpeg

images (3).jpeg

images (4).jpeg

download.jpeg

download (1).jpeg

download (2).jpeg


images (5).jpeg


VS Wali Harage (kiisiiimmmi)....

images (6).jpeg

images (7).jpeg

images (8).jpeg

download (3).jpeg

download (4).jpeg


Aahahahhahaa Wali ndondo....

Kama wametoka droo vilee..... Kama vipi ipigwe kolabo tuu....

Pilipili isikosekane tafadhali.

Matata the K.
 
Mkuu umesahau ugali dagaa wa maji na chumvi a.k.a chukuchuku. Ukienda chato ndo chakula cha usiku, mchana, asubuhi, adhuhuri, alfajiri, alasiri etc
Hahaha kweli, huyu anaitwa chukuchuku.

Hakuna kitunguu, wala nyanya wala mafuta.

Mchuzi unarangi ya bati flani.

Hii ukiwa umewahi kufulia lzm unielewe hawa mkanda ya ziwa
 
Hahaha My best food ever since I was school hadi leo ni wali ndondo
Hii kitu mkuu mimi nilikuwa kama nimerogwa. nikiwa dogo siku ya wali ndondo nakuwa mtiifu sana na sichezi mbali. ila dagaa ugali vinatamba kwa sababu ktk hali zote unatumia.

Wali ndondo mkuu familia ikifulia utasikilizia kwa jirani harufu. ila wali ndondo pia hatari saana
 
Back
Top Bottom