Ulaji wa dagaa kila siku katika mlo wa Mtanzania ni mazoea au kukosa mbadala?

Undava King

JF-Expert Member
Aug 11, 2017
3,205
5,333
Hakuna asiyejua kuwa kitoweo hiki pendwa chenye kiwango kikubwa cha protini ni kitoweo muhimu kwa afya zetu.

Lakini pia hakuna asiyeweza pinga kuwa kwa asilimia kubwa, watanzania wengi ni walaji wa wa ugali na dagaa na familia nyingi si mijini wala vijijini ujikuta wakifululiza ratiba toka Monday mpaka Sunday mwendo ni ugali na dagaa wakibadilisha kidogo wametupia mboga za majani au ubwabwa maharage kisha ratiba inarudi palepale.

Hii hali inapelekea ziwa Victoria ambalo ndilo tegemeo kubwa na lenye kulisha vinywa vingi zaidi ya mamilioni ya watu kuzidiwa, mara kwa mara ziwa hili kupitia mamlaka za uvuvi ulazimika kuweka zuio kwa kipindi fulani hili kufanya kitoweo hiki kisije kikaisha/kutoweshwa na kuleta dhahama, just imagine Tanzania bila dagaa wa ziwa Victoria?

Je, hali hii ya kutegemea sana haina moja ya kitoweo na ugali katika milo yetu hata kama kuna mbadala wa nyama na samaki, mimea jamii ya mikunde, vyakula jamii ya mizizi, matunda au ngano, unasababishwa na nini?

Je, ni kwa sababu watanzania wengi wanapenda sana kula ugali na dagaa kwa kuwa ni desturi na wanafurahia kula chakula hicho kila siku kuliko vyakula vingine?

Au pengine ulaji wa dagaa kupita kiasi ni gereza ambalo masikini walio wengi hawawezi kuliepuka, hivyo basi kwa Tanzania dagaa ndiyo "sukuma wiki" kikubwa uhai?
 
Ukeli ni kuwa mada inataka kumdhihaki Mtanzania.

Ukweli ni kuwa Dagaaa ndie samaki anayetumika hata katika mapishi ya Mabilionea Duniani....ikiwa na pamoja na utumiaji wa mafuta yanayotoka kwa samaki.

Ukweli ni kuwa, hakuna chechote kibaya au cha kudhalilisha kula Ugali na Dagaa kila siku.

Dagaa ni Afya asikudanganye mtu.

niongezeee tu, kule italia wanakula pasta au niseme spaghetti na dagaa na nyanya kila siku. Ati Ugali na Dagaaa. Mfyuuuuuuuuuu!
 
Binafsi napenda kupika, na mojawapo ya vyakula napenda sana ni ugali na dagaa. Usithubutu kujikuta mahali ambapo unalazimika kula chakula kimoja daily, utachoka hata kiweje.

Namaanisha hata kama ni wali nyama, utachoka tu. Kama dagaa unajikuta unakula kila siku kwa sababu hauna mbadala lazima uzichoke hasa kama mpishi hajui kubadilisha ladha.
 
Back
Top Bottom