Napendekeza tuwe na Mbunge mmoja tu kila mkoa. Halafu walipwe 50M kwa mwezi.

Sexless

JF-Expert Member
Mar 11, 2017
21,581
50,476
Sioni sababu ya kuwa na wabunge 393 ktk nchi maskini kama hii. Halafu tija yao mm binafsi siioni kabisa japo ni wengi kiasi hicho.

Kwann tusiwe na mbunge mmoja tu toka kila mkoa? Huyu awe anahushuria vikao vya RCC na kupokea mihutasari ya vikao vya madiwani toka halmashauri zote ktk mkoa husika kisha asome na kuyawasilisha mawazo/matatizo hayo bungeni.

Kwahiyo tutakuwa na bunge la watu 46 tu
  • 36 toka mikoa 36
  • 10 toka kwa rais.

Wabunge hawa wawe na mshahara mnono Kati ya 40M mpk 50M kwa mwezi.

Mawaziri wawe sita tu. Kwasabb napendekeza zibakie wizara sita tu
1. Afya na nini nin ibakie.
2. Tamisemi-- elimu, kilimo, mifugo,uvuvi, michezo, mazingira, habari, n.k
3. Mambo ya nje na ushirikiano wa kikanda.
4. Ulinzi na mambo ya ndani,
5. Fedha, mipango, nishati, madini, viwanda na biashara
6. Sheria, katiba, utawala bora na utumishi wa umma.

Sifa kuu za wabunge.
1. Awe ni mtu aliyeweza kufanya jambo fulani kubwa linalosaidia jamii kubwa ktk mkoa. Mfano kaanzisha kiwanda kikubwa, taasisi, amefanya uvumbuzi mkubwa, anaendesha mashamba makubwa na kutoa ajira kwa watu
2. Awe na elimu ya shahada ama zaidi. Hii itamsaidia kuchambua na kupambanua mambo kwa upana.

Viti maalumu vifutwe kabisa. Vimetuchelewesha sana hivi ndugu zangu (in mwendazake's voice).
 
... hata kwa kila wilaya it is still OK plus na wa rais hawatazidi 150 badala ya utitiri wa zaidi ya 360 waliopo.
 
Mbunge atokane ndani ya madiwani.
Madiwani wote wawe na elimu ya juu
... wazo kama hili liliwahi kutolewa humu JF siku za nyuma. Kwamba uchaguzi mkuu uhusishe Rais na madiwani ambao kimsingi ndio wanaoishi na wananchi kule vijijini badala ya wabunge ambao zaidi ya 80% wako Dar na mijini huku wakitelekeza majimbo yao.

Madiwani wakishapatikana, wamchague mmojawao atakayewakilisha halmashauri yao kwa kipindi cha miaka 2.5 baada ya hapo wamchague mwingine atakayewakilisha 2.5 mingine total 5 yrs tena ikiwezekana wa-rotate ME na KE. Kwa utaratbu huu tutakuwa na uwakilishi mzuri zaidi kuliko ilivyo sasa majitu yanalilia posho za kusinzia Bungeni.
 
Tatizo namna ya kupenya mpk likakubaliwa ndiyo mtibani. Maana litakata ulaji wa watu
Njia ya kupenya ni moja tu, rais kulivunja bunge, baada ya kuitishwa kura ya maoni ya katiba mpya, itakayo kuwa imebeba hilo 'wazo tamu sana' kwa maslahi mapana ya nchi kwa vizazi vya sasa na vijavyo.
 
... wazo kama hili liliwahi kutolewa humu JF siku za nyuma. Kwamba uchaguzi mkuu uhusishe Rais na madiwani ambao kimsingi ndio wanaoishi na wananchi kule vijijini badala ya wabunge ambao zaidi ya 80% wako Dar na mijini huku wakitelekeza majimbo yao.

Madiwani wakishapatikana, wamchague mmojawao atakayewakilisha halmashauri yao kwa kipindi cha miaka 2.5 baada ya hapo wamchague mwingine atakayewakilisha 2.5 mingine total 5 yrs tena ikiwezekana wa-rotate ME na KE. Kwa utaratbu huu tutakuwa na uwakilishi mzuri zaidi kuliko ilivyo sasa majitu yanalilia posho za kusinzia Bungeni.
Wow! Mawazo mazuri kama haya kwann hayafanyiwi kazi? Ahh! Nachoka kabisa mie.
 
Wengine tutapata wapi ulaji jamani? Mbona munataka kutuzibia riziki zetu? 😁 😁 😁

Na akipata huo mshahara wa 50m bado atasema hautoshi kwani jimbo ni kubwa!
 
hivi mikoa ipo 36 au 30?

anyway; ni wazo zuri hata ikiwa kila wilaya pia siyo mbaya

ila siyo milion 50 aseh... labda 25m
 
Back
Top Bottom