Napendekeza, mke akifa akazikwe kwao

Napendekeza, mke akifa akazikwe kwao

1:Tasa- Makaburi ya watu kama hawa hayathamiwi kabisa, ni bora wazikwe kwao ambako kaburi lake litathaminiwa na nduguze.

2:Waliozaa na wanaume wengi - Wakazikwe kwao ili watoto wote wawe wanapata fursa ya kutembelea kaburi (kufagia) pasipo kuwa na masharti yoyote,na sio watoto tu hata wanaume zao waliozaa nao watakuwa wanapata hiyo nafasi.hayo ni maoni yangu.
Umewaza nini?
 
Kiukweli huwa hatupendi kuzikwa kwenu. Binafsi ningependa kuzikwa kwetu...nafikiria kuacha wosia.
Ukishaona umeanza kuwa na mawazo ya hivi basi Jua haupo Tena kwenye hiyo ndoa.
 
Naangalia angalia ka sehemu hapa hapa shamba pa kunizika, sitaki mwili upate hekaheka, maisha yangu yote nimepambana mpaka oops
 
Kuna wale ambao wakwe hawajawaelewa, nahisi kaburi litakua linasimangwa tu....bora kuzikwa kwenu
 
Umewaza nini?
Sijawaza chochote ila ninayoyaona kwenye jamii ndio yaliyonifanya nianzishe uzi huu.
Mtu anauza shamba ambalo lina kaburi na kumruhusu mnunuzi kulipoteza lile kaburi ,kwasababu tu marehemu hana mtetezi (mtoto/watoto)
Marehemu shangazi yangu alikuwa na watoto 7 aliozaaa na wanaume watatu tofauti,alifariki akiwa kwa huyu mumewe ambaye alizaa naye watoto wawili wa mwisho,sasa hawa binamu watano hawakushirikishwa kitu chochote wakati wa kujenga kaburi kama kwamba hakuwa mama yao,na mpaka sasa hawawezi kwenda kutembelea kaburi la mama yao bila uwepo wa wale wadogo wao wawili,Je hawa marehemu wangezikwa kwao hizi changamoto zingekuwepo?
 
Sijui kati yangu mimi na yeye nani atatangulia ila kuzikwa ki katika aridhi yangu ya asili
 
Kuna wale ambao wakwe hawajawaelewa, nahisi kaburi litakua linasimangwa tu....bora kuzikwa kwenu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kuna msiba nilienda mwaka huu marehemu na ma mkwe wake zilikua haziivi akasema azikwe kwao, kweli kazikwa kwao ma mkwe hakukanyaga anasema mila haziruhusu yeye kufata msiba wa mkwe akawa naongea sasa "hii mbuzi imekataa kuja kuzikwa huku mi siwezi kwenda"
 
Mtoa mada atakuwa amepigwa na kitu heavyweight kichwani,sio kwa povu hili jamani.
 
Kwetu kuoa ni kama umepata kijakazi... mke ata piga kazi mpaka achakae...

Ukiolewa ndio kwisha habari yakoo kwenu bai bai...

Kwenda kwenu ni kwa ruhusa ya mumeo ata kama mzazi wako amefariki una takiwa kwenda mzika, jua huto enda kama mumeo hataki uende Au ajakupa ruhusa ya kwenda

Ukifa utazikwa kwao mumeo na mumeo ndio mwenye mamlaka yote dhidi ya mke na watoto wake

Kuna baadhi ya watu hawa ruhusu ata kidogo watoto wake wande kwa upande wa mama yao kusalimia Au kuwa fahamu (wana sababu zao)
Ishiiiiiy mambo gani haya?
 
Back
Top Bottom