Ndoa za makaburi, nyumba mboke na nyumba nthobhu si mbaya sana

Nyamesocho

JF-Expert Member
May 5, 2023
476
1,244
Unaweza ukadhani hizi ndoa ni mbaya lakini kwa jicho la tatu nimebaini hizi ndoa katika kabila la wakurya si mbaya saaana, faida ndo nyingi kuliko hasara

Maana ya hizi ndoa

1,Ndoa za makaburi ni aina ya ndoa katika jamii ya wakurya ambapo binti huolewa kwa jina la marehemu ambaye aliwahi kufa kabla ya kuoa,kwa maana kuwa familia hii ilizaa watoto wa kiume,kwa bahati mbaya sasa kabla ya kufikia umri wa kuoa akafariki

Ili kuendeleza kizazi chake mmoja wa mwanafamilia au ukoo atamuoa binti na atahudumiwa kila huduma na atazaa watoto ambao wataitwa kwa jina la marehemu aliyewahi kufariki lengo ni kuendeleza kizazi chake, mfano Steven Kanumba angekuwa ni mkurya jinsi alivyofariki, Sasa hivi huko kwao angekuwa na mke na watoto wanaoitwa jina lake hivyo kizazi na kizazi jina la Kanumba lisingepotea kwenye jamii kama asingekuwa msanii

Kwa maana gani kulingana na mila na desturi za wakurya mwanaume au mwanamke akifa hajaoa au kuolewa kamwe jina lake halitaitwa kwa ndugu wengine (yaani kuwapa majina watoto) majina yao yatakuwa yamekoma duniani ili sasa jina la marehemu liendelee kuitwa kwa watoto wa ndugu wengine ndoa ya kaburi itahusika na miongoni mwa wale watoto watakaozaliwa kwa jina la marehemu atapewa jina halisi la marehemu aliyewahi kufariki

2,Nyumba mboke ni aina ya ndoa katika jamii ya wakurya ambapo ikiwa familia hiyo haikubahatika kupata mtoto wa kiume ila walizaliwa wa kike tu hivyo mama wa familia ataamua kumuoa binti kupitia kijana wa ukoo ambaye atakabidhiwa kumzalisha ila huduma zote atamhudumia mama huyo aliyemuoa ila watoto watakaozaliwa wataitiwa jina la aliyekabidhiwa kumzalisha

Lengo la huyu mama ni kwamba iwapo atakufa bila mtoto wa kiume atakayeoa mkamwana kizazi chake binafsi kwenye ndoa ya mume wake kitakuwa kimeisha,mali zake zitachukuliwa na mtu mwingine hasa kwa mke mdogo maana mume wake alivyoona mke wake hakuzaa mtoto wa kiume automatically mwanaume yeye ataoa mke mwingne sasa naye mwanamke atasema bora na yeye aoe apate mrithi na atakayekuwa anamuhudumia ikiwa anaumwa,au kuzeeka na kuondokana na upweke kwa sababu hatakuwa amebaki na mtu wala mjukuu wa kumsaidia hivyo huamua kuoa ,kumbuka mabinti wanaolewa na kwenda kuanzisha familia zingine

3,Nyumba nthobhu ni aina ya ndoa katika jamii ya wakurya ambapo ikiwa familia haikupata mtoto yeyote na automatically mwanaume yeye ataoa ila mwanamke yeye atabaki bila mtoto hivyo mwanamke huamua kuoa binti kupitia mwanaume wa ukoo,haina tofauti sana na nyumba mboke

Mambo mazuri yaliyomo kwenye ndoa hizi

1, kuendeleza kizazi kwa familia zinazopata changamoto ya uzazi kwa sababu kila mtu anaoa na kuolewa ili kuendeleza kizazi chake na cha ukoo wake

2,Watoto wanaozaliwa kwenye familia au ndoa hizi huthaminiwa zaidi na kutunzwa na kila mwanaukoo yaani unaweza kukuta watoto wa ndoa hizi wanapata huduma kamilifu kuliko walio kwenye ndoa za kawaida

3, Wanawake waliopo kwenye ndoa hizi ndo huamua namna ya kuishi,iwapo hatakubaliana na mwanaume aliyekabidhiwa kumzalisha huamua kumtafuta mwanaume mwingine ili amzalishe na kumhudumia ila hupewa urthi wote anaopaswa kupewa kwenye ukoo

4,Si ndoa za kusagana,kuna watu wanadhani ndoa za mwanamke kumuoa mwanamke ni kwenda kusagana la hasha,aliyeolewa na mwanamke anaweza kuzeeka hata kwa bahati mbaya wasiwahi kuonana nyuchi, mwanamke aliyeoa humuita binti aliyemuoa kama mkamwana na si vinginevyo na humheshimu sana,furaha ya huyu mama ni watoto watakaozaliwa tu

Hasara za ndoa hizi ni moja tu

Magonjwa ya ukimwi,kurthi na gonorea basi,kwamba aliyeolewa na mwanamke anaweza kuwa na kila aina ya wanaume akapata magonjwa na kuambukiza wengine lakini kwa dunia ilivyo sasa walioolewa na wanaume na walioolewa na wanawake wanafanana kwa ngono zinazofanyika

Ni hivi ndoa hizi si mbaya Kama mnavyokuwa mnafikiria , ni ndoa ambazo haziwezi kufananishwa na ndoa za jinsia moja
 
Watakwambia hizo mila ni hovyo ila za baba mtakatifu papa Francis ndio nzuri.

Wazungu wamefundisha waafrika upumbavu mwingi sana na waafrika wameupokea bila kujiuliza.

Mzungu atakwambia mwanaume kuoa mke zaidi ya mmoja ni makosa ila mwanaume kumfumua mwanaume mwingine makalio na kufumua mavi ni sawa ni ustaarabu.

Watakwambia mwanamke kuoa mwanamke mwingine ni sawa kabisa.
 
Wanawake wa Kikurya wana raha sana km Wahadizabe wanachagua Mwanaume
Wanawake waliopo kwenye ndoa hizi ndo huamua namna ya kuishi,iwapo hatakubaliana na mwanaume aliyekabidhiwa kumzalisha huamua kumtafuta mwanaume mwingine ili amzalishe na kumhudumia
Hii ni Wahadizabe copyright
 
Huwa namuwazia sana Rais wa France
Macron
aliyemuoa aliyekuwa mwalimu wake.
Kifupi wao hawatarajii kuzaa mtoto
Mwalimu yeye wakati anaolewa na Macron tayari alikuwa na watoto
Ila pia mtoto wa mwisho wa yule mama ni mkubwa kiumri kumzidi Macron (ambaye ni dingi Fala wake).

Nadhani hili la kuendeleza ukoo ama Jina ni sisi ndiyo tunahangaika nalo Africa.

Macron kumbe angekuwa mkurya angechapwa viboko na ukoo wake?
 
Huwa namuwazia sana Rais wa France
Macron
aliyemuoa aliyekuwa mwalimu wake.
Kifupi wao hawatarajii kuzaa mtoto
Mwalimu yeye wakati anaolewa na Macron tayari alikuwa na watoto
Ila pia mtoto wa mwisho wa yule mama ni mkubwa kiumri kumzidi Macron (ambaye ni dingi Fala wake).

Nadhani hili la kuendeleza ukoo ama Jina ni sisi ndiyo tunahangaika nalo Africa.

Macron kumbe angekuwa mkurya angechapwa viboko na ukoo wake?
Angeoa tena kwa kulazimishwa ila uzuri mwingne uliyopo ukuryani ni kwamba mtoto aliyezaliwa kwingine anaweza kupewa ubini wa mwanaume aliyemuoa mama yake ingawa hajamzaa yeye
 
Back
Top Bottom