Napendekeza Katiba ya CCM irekebishwe ili Dkt. Magufuli aendelee kuwa Mwenyekiti hadi atakapoamua kung'atuka kama Nyerere

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,947
141,924
CCM ni chama dola.

CCM ni chama tawala wala hilo halina ubishi.

CCM ni chama mbeba maono wa taifa hili la Tanzania.

Dkt. Magufuli ambaye ndiye Mwenyekiti wa CCM na Rais wa nchi yetu ameonyesha uwezo mkubwa sana katika kusimamia misingi ya chama na uzalendo kwa ujumla.

Kwa mageuzi makubwa anayoendelea kuyafanya ndani ya chama ambayo yameonyesha ufanisi mkubwa kwa maendeleo ya taifa, napendekeza katiba ya CCM ifanyiwe marekebisho ili nafasi ya mwenyekiti isiwe na ukomo.

Hii itatoa fursa kwa mwenyekiti Magufuli kuendelea na uongozi hadi atakapoamua kung'atuka kama alivyofanya baba wa taifa Mwalimu Nyerere.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mwanamke ukimpa uhuru sana mwisho wa siku ni vituko.

Wazungu walitupa nchi hii kwa maandishi,naona sasa mnataka nchi kwenda kwenye machafuko.
 
Anaweza kuwa mwenyekiti wenu wa milele ila hawezi kuwa Rais wa milele, habari ya chama dola usiilete kwenye mambo ya nchi, ndio maana CCM mna katiba yenu na Tanzania ina katiba yake.
Nipe tofauti ya Tanzania na CCM!
 
Back
Top Bottom