Nape Nnauye kuongea na wanahabari

Nape Nnauye kuongea na wanahabari

Status
Not open for further replies.
d14c99dd0721ce0f47f82755ccec37d5.jpg

Duuuuuuuuu
 
Ama kweli siasa haina rafiki wa kudumu wala adui wa kudumu,nashangaa sana kuona Nape leo kawa shujaa wa watanzania,mmeshasahau yote dah!
Kwani maana ya ubinadam ni nini?

Unaweza fanya mazuri na kukosea pia sasa wataka tuhukumuje labda katika jema?
 
Hii iwe fundisho kwa watu wote wenye tabia kama hizo, ni nani alitangaza kufuta Bunge Live, ni Nani alisema hata kwa Goli la Mkono na hila nyingine nyingi. Mbona hakutangaza kujiuzulu wakati wa Bunge Live ambalo lilikuwa na maslahi kwa wengi.
Afu leo kuna wajinga wanamuita shujaa,.....
Hicho ndicho alichokipanda October 2015
 
Malipo ni hapahapa duniani mmesahau alivyovuruga wenyenianjema kwa maneno yake akiwa itikadi na uenezi.ccm, sasa mimi nasema hana cha ushujaa chochote ila malipo ya dhambi.ya jana inamtafuna, hawa ndio waliotufikisha hapa na hayo ndio malipo ya kutokwa kwa aliyempigania.
Ukifiga simba usishangae siku akila mtoto wako
 
Nape funga hilo 'Vuvuzela' lako, utakuja kuharibikiwa mapema, you are still young, hamia Chadema uendelee kuila nchi
 
Nape angekausha tu,anaweza kuvuliwa uanachama kabla ya saa 4 au hata kum-Saanane,Lissu aliwaambia mapemaaaaa
Kwamba akimalizana na wapinzani atahamia kwingine na kwingine na kwingine..

Wanasema ukizoea kula nyama za watu huwezi kuacha ati..
 
Nape 2015 wakati wa uchaguzi na baada ya kuzima bunge live, nilikuchukia na ulikiwa unanikera sana lakini katika hili nakuunga mkono na roho yangu imekusamehe!
Aliyezuia Bunge Live alishajitokeza na kukiri kuwa yeye ndiye kizuizi na hiy ilimsafisha Nape..
 
Katiba mbovu hutoa viongozi wabovu.....kina nape walifurahia sana katiba hiyo sbb iliwapa uhakika wao kutawala daima sasa kapatikana kiboko wa wote kupitia katiba hiyo hiyo mbovu...
 
Aliyekuwa Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo Nape Nnauye ambaye leo ametenguliwa na Rais Magufuli amefunguka na kusema leo mchana atakutana na waandishi wa habari kutoa ufafanuzi wa jambo hilo.
Nape Nnauye ambaye ni Mbunge wa jimbo la Mchinga amesema hayo kupitia mtandao wake wa twitter
"Ndugu zangu naomba tutulie! leo mchana nitakutana na Wanahabari na tutalizungumza hili. Nitawaambia saa na mahali, kwasasa naomba tutulie" Nape Nnauye
Rais Magufuli leo asubuhi amefanya mabadiliko madogo ya baraza lake la Mawaziri kwa kumteua Dr. Harrison Mwakyembe kuwa Waziri wa Habari, Sanaa utamaduni na michezo. ambayo ilikuwa chini ya Nape Nnauye pia amemteua Prof. Palamagamba Aidan John Mwaluko Kabudi kuwa Waziri wa Katiba na Sheria.
 
Msimdanganye Mhe.Mbunge,hawezi kushindana na mwenye nchi.Nape ongea na media lakini refrain from exchanging words with Mr.President.
Kwani wanashindana yeye si anatoa alicho kiona au ndo unataka tusijue hakuna mashindano hapo kika mtu anatenda yampasayo kutenda
 
Aaaaaaahhhh.....ongea baba ongea muosha uoshwa ulimkataa lowasa ukampendekeza mkulu sasaaaaaaa. Umekuwaje vile
 
bora aongee kile kilichopo moyoni mwake asikae nacho
Angejipa muda wa kutafakari na kisha kuongoea na kufanya jambo sahihi. Sasa hivi atakacho ongea kitatokana na msukumo wa jambo flani kama hasira au furaha iliyo pitiliza. Labda kama alijiandaa siku nyingi kwa hili lililotokea.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom