Hili gazeti mbona halijaibalance hii taarifa?zimewekwa tuhuma za EPA na tuhuma za Nape kugombea Ubunge kupitia Chadema bila kuweka majibu ya Nape kwenye masuala hayo, hii sio sahihi, i guess hili ni la Tanzania Daima hili, gazeti la Uhuru la Chadema.

Kimsingi sioni hoja hapa, CCM inatambua kuwa kuna wanachama wake waliokuwa wamekatishwa tamaa na mwelekeo ya chama chao na ndipo walipokuja sasa na mpango wa kujivua gamba ili kuwarudishia wanachama hawa matumaini mapya na kuwafanya warudi kundini, kwa mantiki hiyo CCM hawana shida na Nape kuwahi kutaka kujitoa na kuanzisha CCJ, sasa pilipili wasiyoila yawawashia nini Chadema? naona Nape anawapa tabu sana.

Lakini lingine...hivi unaenda Mbambabay unaongelea mambo ya Nape na CCJ wakati wananchi unaowaambia ata hawajui kama CCJ ni mdudu au ni mnyama? Huku ni kupoteza nafasi ya kuwaeleza wananchi mambo yanayowahusu wao na maisha yao na namna gani Chadema itayabeba matarajio na changamoto zao kwa kesho bora zaidi.
Kwani nikisema watakaowachagua viongozi wa ccm ni wana ccm kwasababu ndo wanawajuwa viongozi wao basi ina maana na mimi ni mwana ccm?Just a little common sense mkuu.Hakuna linalonifika.I am free, with free mind.Sina maslahi,and so i will speak my mind bila kujali kama ilivyo kwe wengi wetu humu.- Mushi jana ulisema wewe si mwanachama wa Chadema, sasa leo ya wanachama wa Chadema yamekufikaje? I mean kwa mtu ambaye sio mwanachama mbona unaonekana kuyajua sana ya huko?
Es!
- Hivi vita vya kelele zisizo na tija kwa taifa haviwezi kuisaidia Chadema kwa sababu vinaisaidia CCM kutojadili hoja muhimu kwa taifa, na the more vikiendelea ni the more Chadema will lose, Marando alikuwa anatafuta nini kwenye ndege ya Rais Mkapa kila wakati, kule EAC alipelekwa na nani? ha! ha! ha! ndio maana ninasema kwa njia hii mpya ya kuchafuana Chadema will pay more kuliko CCM ambao wamezoewa na machafu!
Es!
Vita umeanza mwenyewe, sasa unalia nini?
Nape unarusha mawe, Vita umeianzishaa!
Mawe warusha vyovyote, hata hauna malengo
Ulianza na Mafisadi, sasa umewagwaya
Mara Slaa mwana zuoni, jiwe ukamrushia,
Umekuwa kama chizi, Unarusha bila dira,
Dawa ya moto motoni, Dawa ya mawe unaipata,
Ulianza na Mafisadi, Aibu umeipata
Aibu umeipata, Mafisadi sasa wako
Sasa unawatetea, Magamba ni nguo zako
Umma hauna chelea, wanapima kwa vigezo
Ulianza na Mafisadi, sasa umetota jasho
Vita umeianzisha, subiri utaipata
Wameanza kupuuza, kumbe hauna dira
Dira yako yote tamaa, na uchu wa madaraka
Ulianza na Mafisadi, sasa unawatetea
Eti kwa ufinyu wako, wadhani bado twalala,
wataka kutuadaa, ili kutupumbaza,
Hatudanganyi kwa kanga, kwa chumvi wala kofia
Ulianza na Mafisadi, mbona wamekushinda
Shirikisha akilizo, Fikiri kabla ya kunena,
Mja na mwana vitendo, Tanzania ndio baba,
Tetea kwanza nchi yako, ndipo utaeleweka,
Mafisadi ulianza nao, sasa unawatetea.
Nape endelea kuwasha moto hili la mbowe kuuzia chadema screpa za magari kwa 500 milioni tusinge fahamu ufisadi huo! Nape nakukubali sana!
Kuna mengi kumhusu huyo jamaa na Chadema wasipokuwa waangalifu watakuja kuvuna mabua baadae. Mwenzao yuko kazini na kadri wanavyomshangilia ndiyo anavyoingia katika ghala lao la mikakati na baada ya muda watajikuta wanalia!
Nimemshusha heshima baada ya kuanzisha ccj na kukaa kimya..kisha kurudi tena ccm baada ya kupewa madaraka..it means kijana ana uchu wa madaraka na mnafiki.
Supposing this information or revelation by Mpendazoe is anything to go by, what does it tell us. Does Mpendazoe tell us that those who warmed up to CCJ do not retain the right of associating with other like minded people in political parties. Does this place Nape any worse than himself? Why don't we rise about petty issues and focused what really is the priority for this country. It is actually Chadema who lose alot in this debate because CCM would enjoy the distraction. But it will take time for Chadema to realise that their followers need something better than name calling!![]()
VITA vya maneno kati ya Chadema na CCM jana imechukua sura baada ya Fred Mpendazo kumtaja Katibu Mwenezi na Itikati wa CCM, Nape Mnauye kwa miongoni mwa vigogo sita walianzisha Chama cha Jamii (CCJ) .
Mpendazoe alitoboa siri hiyojana alipokuwa akituhubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mbamba Bay kilichopo katika wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Mpendazoe alijitoa CCM Machi 30, mwaka jana akiwa Mbunge wa Kishapu na kujiunga na CCJ Aprili 16, mwaka huo kabla ya kuhamia Chadema, baada ya CCJ kukosa sifa na kufutwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Mbamba bay, mkoani Rvuma jana, Mpendazoe alisema ameamua kuliambia taifa ukweli kuhusu Nape, ili umma uepuke kudanganywa na propaganda za kijana huyo.
"Kelele zote anazopiga Nape kuitetea CCM ni za kinafiki kwani aliwahi kukigeuka chama hicho na kushiriki katika mipango yote ya kuanzisha CCJ".
Hata hivyo, Nape alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusiana madai hayo ya Mpendazoe, hakukataa wala kukubali kushiriki kuanzishwa CCJ, badala yake alisema, "Cha msingi waeleze (Chadema) CCJ ilikufaje, wasiseme ilizaliwaje, maana kuzaliwa ni sherehe na kufa ni kilio."
Nape ambaye hakusema lolote kama kombora la Mpendazoe ni la kweli aliwageuzia kibao Chadema akisema, "Pamoja na hayo yote, waache (Chadema) kubaka demokrasia."
Alifafanua akisema "Watanzania walipiga kura kuichagua CCM iwaongoze kwa miaka mitano ijayo, sasa wanaposema tutaandamana nchi nzima ili serikali iondoke kabla ya muda huo, huku ni kubaka demokrasia na ni uhaini."
Mpendazoe alisisitiza kuwa Nape alishiriki katika kuandaa na kuandika katiba ma miiko ya uongozi ya CCJ, kutafuta fedha za kukuza chama na jengo la kuweka ofisi za chama hicho. Alisema: " Huyo Nape anayepiga kelele za kuitetea CCM ni mnafiki mkubwa pengine kuliko wanafiki wote hivi sasa. Mimi na yeye pamoja na wana-CCM wengine wanne, ndio tulioamua kuanzisha CCJ.
"Nape ndiye aliyepewa jukumu la kutafuta nakala za katiba za vyama tawala vya nchini za Afrika, ili kupata katiba nzuri ya itakayoigwa katika kuandika katiba CCJ." Alisema Nape alilitekeleza vizuri jukumu hilo na kufanikiwa kuipata katiba ya chama tawala cha Afrika Kusini cha ANC, ambacho ndiyo kilitumika kwa kiasi kikubwa kuandaa katiba ya CCJ.
Alisema yeye, Nape na vigogo wengine aliosema atawataja muda ukifika walifanya vikao vyote vya siri hadi wakaanzisha chama hicho cha CCJ.
"Tulifungua mtandao maalum wa kuwasiliana kwa internet, ambao baadaye wenzangu waliufuta baada ya kubadili mawazo dakika za mwisho. Iilipotulazimu kukutana mimi na Nape tulipendelea kukutana katika eneo la vinywaji pale Mlimani City, jijini Dar es Salaam". Alisema walifanya hivyo ili wasitiliwe shaka na maafisa usalama wa taifa waliopewa kazi ya kupeleleza wanaCCM waliohisiwa kutaka kuanzisha chama kipya.
"Nape alibadili mawazo ya kutaka kuihama CCM baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi, kwa kuwa alikuwa na uchu wa madaraka ," aliongeza. Alisema Nape aliisaidia CCJ kwa kukipa siri nyingi ikiwemo mambo yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mikutano ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec)n a hata vikao vilivyokuwa vikifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyopo Lumumba.
"Nape pia alitupa siri kwamba baadhi ya walioanzisha CCJ walikuwa wanakaribia kufukuzwa kwani katika mkutano wa NEC, majina ya baadhi yao yalitajwa na kujadilia kwenye kikao hicho.'
Source: Mwananchi.
My Take:
Kama mwenyewe Nape hakanushi basi atakuwa ni hatari kwa chama chake kauli yake ya 'PAMOJA NA HAYO' inadhihilisha amebanwa kwenye kona.
Sasa ndiyo wakati wa kupata mengi wengine tunajumlisha na kutoa siku ya siku tutakuja na jibu sahihi.
Kati ya vitu ambavyo haviwezi kuvumilika katika jamii ya waungwana ni usaliti, tuhuma ambazo zimetolewa na Fredy Mpendazoe za kuwa wewe ni mmoja wa waanzilishi wa CCJ ni mbaya mbaya na mbaya zaidi ni kitendo chako cha kudhoofisha chama cha mapinduzi kwa kutoa SIRI za vikao vya chama, Najua mwenyekiti wako atakuita na atakwambia upime mwenyewe uzito wa tuhuma hizi, ila nakushauri kama kijana mwenzetu usisubiri uitwe, uchukue hatua stahiki za kuachia ngazi kwenye nafasi zote za uongozi ndani ya chama.
Hakuna mtu aliyesema ni kosa kuhama chama ila hapa tunajadili uaminifu na unafiki wa wanasiasa wanao hamahama au wanaobaki kwenye chama kwa maslahi yao.
you got it wrong, its not chadema who are doing this.... its nape's friendsChadema mbona Nape anawasumbua sana! Mwacheni Nape na CCM yake naona Nape ametawala sana hapa JF! Nape anawapa presha sanaaaaaaaaaaa!