Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Nape ni mwanzilishi wa CCJ

acheni kumsakama Nape....Stephen Wassira alikuwa nani na saivi ni nani? Hizo ni siasa tu na kwenye siasa uadui haudumu

Akina wassira, nsazugwanko n.k hawakufanya kwa kificho walikuwa wazi ila nape alikuwa anambwelambwela mguu ndani mguu nje mpaka alipopata u-dc ndo katulia, mnafiki tu huyo, siyo muumini mzuri wa itikadi.
 
Kati ya vitu ambavyo haviwezi kuvumilika katika jamii ya waungwana ni usaliti, tuhuma ambazo zimetolewa na Fredy Mpendazoe za kuwa wewe ni mmoja wa waanzilishi wa CCJ ni mbaya mbaya na mbaya zaidi ni kitendo chako cha kudhoofisha chama cha mapinduzi kwa kutoa SIRI za vikao vya chama, Najua mwenyekiti wako atakuita na atakwambia upime mwenyewe uzito wa tuhuma hizi, ila nakushauri kama kijana mwenzetu usisubiri uitwe, uchukue hatua stahiki za kuachia ngazi kwenye nafasi zote za uongozi ndani ya chama.


on the red: Ukianza kula nyama ya mtu huwezi kuacha... utaendelea kula nyama ya mtu!
 
- As much as I like to hear really ishus, sina jinsi isipokuwa kujadili this nonsense, ambazo ni good kwa CCM kwa sababu inawapa nafasi ya kutojadili serious ishus muhimu kwa taifa na their respeonsibilities as watawala, focus ni lazima ipungue ninapoona wakombozi wangu wameanza kujikita kwenye nonishus kwa taifa na kuwatumia kina Mpendazoe, wachumia tumbo!

- CCM haipotezi direction wala focus kwa kulazimishwa kujadili CCJ, chama ambacho hakipo na wala none of us knows exactly what and who was behind it, Chadema should discuss really ishus, ama sivyo watatupoteza wananchi wote na what they stand for especially na non ishus kama hizi za kina Mpendazoe!

- I mean who is Mpendazoe in Chadema?


ES!
Ina maana wewe jana ulipoanzisha thread ya mshahara wa Slaa na magari machakavu uliona ndiyo issue ya kitaifa kwako kuliko ya Nape kuiba siri za CCM kupeleka CCJ.
 
Hakuna mtu aliyesema ni kosa kuhama chama ila hapa tunajadili uaminifu na unafiki wa wanasiasa wanao hamahama au wanaobaki kwenye chama kwa maslahi yao.

- Uaminifu ni kwa taifa sio vyama, sasa nini uaminifu wa Mpendazoe kwanza amekimbia CCM kwenda CCJ, and then amekimbilia Chadema, kwa nini asingebaki CCJ na kukiendeleza ni kwa sababu aliona hakitasajiliwa kwa hiyo hawezi kugombea ubunge na kwa sababu anataka sana cheo akakimbilia Chadema chama cha wenyewe, ambako aliishia kupigwa chini kwenye uchaguzi kwa vile hakuwa na hela za uchaguzi kama wenziwe ambao wengi ni wanasheria wa kujitegemea, au wako karibu na establishment ya Chadema ambayo pia ni money machine!

- Sasa ungetegemea by now angeshituka kwamba he is not a Chadema as par se, isipokuwa jina tu na kutumiwa ndio wanasiasa wetu hawa, halafu eti ana ubavu wa kuongeela loyalty! Unafikiri establishment ya Chadema ni wajinga wa kumuamini huyu Mpendazoe? hili taifa tumelogwa sio bure!

Es!
 
Halafu siyo kwamba eti ccm ilifanya mabadiliko ndo Nape akaamua akabaki humo,Naawa!.Issue ni kwamba hakikusajailiwa...Akadanganya wenzake.Kubaki kwake ccm ni unafiki kwasababu hakuna lililobadilika zaidi ya yeye kupewa ulaji.Atasingizia magamba,lakini wote tunajuwa ni usanii.Na pia hakwenda cdm kama Mpendazoe na sababu kaitoa kuwa hachangamani na wachagga.
 
Ina maana wewe jana ulipoanzisha thread ya mshahara wa Slaa na magari machakavu uliona ndiyo issue ya kitaifa kwako kuliko ya Nape kuiba siri za CCM kupeleka CCJ.

- Ohhh yes, kama wakipewa taifa watatuuzia nini hao? Zimwi usiolijua lazima ulichunguze kwanza ndio maana US walimtosa Odinga kule Kenya wakabaki na zimwi wanaloljiua Kibaki!

Es!
 
Halafu siyo kwamba eti ccm ilifanya mabadiliko ndo Nape akaamua akabaki humo,Naawa!.Issue ni kwamba hakikusajailiwa...Akadanganya wenzake.Kubaki kwake ccm ni unafiki kwasababu hakuna lililobadilika zaidi ya yeye kupewa ulaji.Atasingizia magamba,lakini wote tunajuwa ni usanii.Na pia hakwenda cdm kama Mpendazoe na sababu kaitoa kuwa hachangamani na wachagga.

- At least amesema ukweli wake kuliko unafiki wa kusema uongo, kwamba kwa nini hakujiunga na Chadema!
, alichofanya ni calling spade exactly what it is!

Es!
 
Slaa kulipwa milioni 7.5 ni hoja, ila Nape kuasisi CCJ siyo hoja?

kweli ni kazi ngumu kuwa mnafiki!
Kazi ni pevu ndugu yangu watu wanalazimisha kingi eti mshahara wa mtu mmoja ndiyo issue kubwa kwao kuliko kiongozi mkuu wa chama aliyekisaliti chama kwa kuiba siri za vikao wanasema eti hiyo ni non issue, duh!! upenzi ni kazi unaweza kumkana hata mzazi wako peupe pee.
 
- Ohhh yes, kama wakipewa taifa watatuuzia nini hao? Zimwi usiolijua lazima ulichunguze kwanza ndio maana US walimtosa Odinga kule Kenya wakabaki na zimwi wanaloljiua Kibaki!

Es!
Watakaowachagua ni wanachadema ambao tayari wanawajua viongozi wao.Sijui unafafanisha kivipi na hayo ya Odinga na USA.
 
attachment.php




"Pamoja na hayo yote, waache (Chadema) kubaka demokrasia."

sauti ya mtu aliyekubali yote baada ya kushikwa pabaya.
 
Watakaowachagua ni wanachadema ambao tayari wanawajua viongozi wao.Sijui unafafanisha kivipi na hayo ya Odinga na USA.

- Mushi jana ulisema wewe si mwanachama wa Chadema, sasa leo ya wanachama wa Chadema yamekufikaje? I mean kwa mtu ambaye sio mwanachama mbona unaonekana kuyajua sana ya huko?

Es!
 
Mimi namwangalia Nape kwa mtazamo tofauti.Ni mtu anayependa kuiona Tz inapata serikali adilifu lakini anakosa nguvu. Ndio maana hata baada ya kupata ukuu wa wilaya ameendelea kutoa kauli za kimapinduzi, wale wanaoitembelea facebook yake wanajua. Hapa ccm wamempa rungu kichaa wanajua ana uwezo wa kupambana. Tatizo ccm hawataweza kumvumilia. Nape nina uhakika atakuja CDM kabla ya 2015 na atakuja na watu wengi kama Odinga na ataivunja ccm. Nape anafanya kazi kubwa ya kuimarisha upinzani ndani ya ccm na atatu
 
Alishaanza kuyatupa magwanda ya kijani njaa hizi jamani zitatuua.

attachment.php
 
Huyu jamaa ni mtu wa kuogopwa sana, hana uwanamapinduzi wowote! Mnafiki na mzandiki. Anatumika kama loud speaker, typical brown nosing type of a guy.
 
kwa sasa anapambana na nani?anapambana kuleta maendeleo au anaropoka upuuzi dhidi ya cdm!mwenye akili kidogo ccm ni magufuli maana anatamka ccm inavyojitahidi bila mafanikio sio nnape.nape karithi cheo cha baba yake moses nnauye!
 
attachment.php


VITA vya maneno kati ya Chadema na CCM jana imechukua sura baada ya Fred Mpendazo kumtaja Katibu Mwenezi na Itikati wa CCM, Nape Mnauye kwa miongoni mwa vigogo sita walianzisha Chama cha Jamii (CCJ) .

Mpendazoe alitoboa siri hiyojana alipokuwa akituhubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mbamba Bay kilichopo katika wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

Mpendazoe alijitoa CCM Machi 30, mwaka jana akiwa Mbunge wa Kishapu na kujiunga na CCJ Aprili 16, mwaka huo kabla ya kuhamia Chadema, baada ya CCJ kukosa sifa na kufutwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

Akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Mbamba bay, mkoani Rvuma jana, Mpendazoe alisema ameamua kuliambia taifa ukweli kuhusu Nape, ili umma uepuke kudanganywa na propaganda za kijana huyo.

"Kelele zote anazopiga Nape kuitetea CCM ni za kinafiki kwani aliwahi kukigeuka chama hicho na kushiriki katika mipango yote ya kuanzisha CCJ".
Hata hivyo, Nape alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusiana madai hayo ya Mpendazoe, hakukataa wala kukubali kushiriki kuanzishwa CCJ, badala yake alisema, "Cha msingi waeleze (Chadema) CCJ ilikufaje, wasiseme ilizaliwaje, maana kuzaliwa ni sherehe na kufa ni kilio."

Nape ambaye hakusema lolote kama kombora la Mpendazoe ni la kweli aliwageuzia kibao Chadema akisema, "Pamoja na hayo yote, waache (Chadema) kubaka demokrasia."

Alifafanua akisema "Watanzania walipiga kura kuichagua CCM iwaongoze kwa miaka mitano ijayo, sasa wanaposema tutaandamana nchi nzima ili serikali iondoke kabla ya muda huo, huku ni kubaka demokrasia na ni uhaini."

Mpendazoe alisisitiza kuwa Nape alishiriki katika kuandaa na kuandika katiba ma miiko ya uongozi ya CCJ, kutafuta fedha za kukuza chama na jengo la kuweka ofisi za chama hicho. Alisema: " Huyo Nape anayepiga kelele za kuitetea CCM ni mnafiki mkubwa pengine kuliko wanafiki wote hivi sasa. Mimi na yeye pamoja na wana-CCM wengine wanne, ndio tulioamua kuanzisha CCJ.

"Nape ndiye aliyepewa jukumu la kutafuta nakala za katiba za vyama tawala vya nchini za Afrika, ili kupata katiba nzuri ya itakayoigwa katika kuandika katiba CCJ." Alisema Nape alilitekeleza vizuri jukumu hilo na kufanikiwa kuipata katiba ya chama tawala cha Afrika Kusini cha ANC, ambacho ndiyo kilitumika kwa kiasi kikubwa kuandaa katiba ya CCJ.

Alisema yeye, Nape na vigogo wengine aliosema atawataja muda ukifika walifanya vikao vyote vya siri hadi wakaanzisha chama hicho cha CCJ.
"Tulifungua mtandao maalum wa kuwasiliana kwa internet, ambao baadaye wenzangu waliufuta baada ya kubadili mawazo dakika za mwisho. Iilipotulazimu kukutana mimi na Nape tulipendelea kukutana katika eneo la vinywaji pale Mlimani City, jijini Dar es Salaam". Alisema walifanya hivyo ili wasitiliwe shaka na maafisa usalama wa taifa waliopewa kazi ya kupeleleza wanaCCM waliohisiwa kutaka kuanzisha chama kipya.

"Nape alibadili mawazo ya kutaka kuihama CCM baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi, kwa kuwa alikuwa na uchu wa madaraka ," aliongeza. Alisema Nape aliisaidia CCJ kwa kukipa siri nyingi ikiwemo mambo yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mikutano ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec)n a hata vikao vilivyokuwa vikifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyopo Lumumba.

"Nape pia alitupa siri kwamba baadhi ya walioanzisha CCJ walikuwa wanakaribia kufukuzwa kwani katika mkutano wa NEC, majina ya baadhi yao yalitajwa na kujadilia kwenye kikao hicho.'

Source: Mwananchi.

My Take:
Kama mwenyewe Nape hakanushi basi atakuwa ni hatari kwa chama chake kauli yake ya 'PAMOJA NA HAYO' inadhihilisha amebanwa kwenye kona.

Sasa ndiyo wakati wa kupata mengi wengine tunajumlisha na kutoa siku ya siku tutakuja na jibu sahihi.


CCM a gang of opportunists and multi faced hypocrites. Kumbe wachumia tumbo tupu.
Deeper in them they know CDM is the ruling party of TZ mass. Ahsante kutujulisha!!!!!!!!!!!
 
Mkuu PJ,

Kila siku naendelea kumnukuu Napoleon Bonaparte.....Never interrupt your Enemy when he's making a mistake.

Walipojivua gamba tu,kabla hata hawajatoka katika chumba cha mkutano wao wa NEC nilishangilia,kwa kweli CCM ni dhaifu kuliko tunavyofikiria.Loh,vituko

Hivi uchaguzi mkuu ni CDM ilishinda..... CCM ipi zaifu?
 
Back
Top Bottom