Nape ni mwanzilishi wa CCJ | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Quinine, May 15, 2011.

 1. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #1
  May 15, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,060
  Trophy Points: 280
  VITA vya maneno kati ya Chadema na CCM jana imechukua sura baada ya Fred Mpendazo kumtaja Katibu Mwenezi na Itikati wa CCM, Nape Mnauye kwa miongoni mwa vigogo sita walianzisha Chama cha Jamii (CCJ) .

  Mpendazoe alitoboa siri hiyojana alipokuwa akituhubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mbamba Bay kilichopo katika wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma.

  Mpendazoe alijitoa CCM Machi 30, mwaka jana akiwa Mbunge wa Kishapu na kujiunga na CCJ Aprili 16, mwaka huo kabla ya kuhamia Chadema, baada ya CCJ kukosa sifa na kufutwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.

  Akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Mbamba bay, mkoani Rvuma jana, Mpendazoe alisema ameamua kuliambia taifa ukweli kuhusu Nape, ili umma uepuke kudanganywa na propaganda za kijana huyo.

  "Kelele zote anazopiga Nape kuitetea CCM ni za kinafiki kwani aliwahi kukigeuka chama hicho na kushiriki katika mipango yote ya kuanzisha CCJ".

  Hata hivyo, Nape alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusiana madai hayo ya Mpendazoe, hakukataa wala kukubali kushiriki kuanzishwa CCJ, badala yake alisema, "Cha msingi waeleze (Chadema) CCJ ilikufaje, wasiseme ilizaliwaje, maana kuzaliwa ni sherehe na kufa ni kilio."

  Nape ambaye hakusema lolote kama kombora la Mpendazoe ni la kweli aliwageuzia kibao Chadema akisema, "Pamoja na hayo yote, waache (Chadema) kubaka demokrasia."

  Alifafanua akisema "Watanzania walipiga kura kuichagua CCM iwaongoze kwa miaka mitano ijayo, sasa wanaposema tutaandamana nchi nzima ili serikali iondoke kabla ya muda huo, huku ni kubaka demokrasia na ni uhaini."

  Mpendazoe alisisitiza kuwa Nape alishiriki katika kuandaa na kuandika katiba ma miiko ya uongozi ya CCJ, kutafuta fedha za kukuza chama na jengo la kuweka ofisi za chama hicho. Alisema: " Huyo Nape anayepiga kelele za kuitetea CCM ni mnafiki mkubwa pengine kuliko wanafiki wote hivi sasa. Mimi na yeye pamoja na wana-CCM wengine wanne, ndio tulioamua kuanzisha CCJ.

  "Nape ndiye aliyepewa jukumu la kutafuta nakala za katiba za vyama tawala vya nchini za Afrika, ili kupata katiba nzuri ya itakayoigwa katika kuandika katiba CCJ." Alisema Nape alilitekeleza vizuri jukumu hilo na kufanikiwa kuipata katiba ya chama tawala cha Afrika Kusini cha ANC, ambacho ndiyo kilitumika kwa kiasi kikubwa kuandaa katiba ya CCJ.

  Alisema yeye, Nape na vigogo wengine aliosema atawataja muda ukifika walifanya vikao vyote vya siri hadi wakaanzisha chama hicho cha CCJ.

  "Tulifungua mtandao maalum wa kuwasiliana kwa internet, ambao baadaye wenzangu waliufuta baada ya kubadili mawazo dakika za mwisho. Iilipotulazimu kukutana mimi na Nape tulipendelea kukutana katika eneo la vinywaji pale Mlimani City, jijini Dar es Salaam". Alisema walifanya hivyo ili wasitiliwe shaka na maafisa usalama wa taifa waliopewa kazi ya kupeleleza wanaCCM waliohisiwa kutaka kuanzisha chama kipya.

  "Nape alibadili mawazo ya kutaka kuihama CCM baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi, kwa kuwa alikuwa na uchu wa madaraka ," aliongeza. Alisema Nape aliisaidia CCJ kwa kukipa siri nyingi ikiwemo mambo yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mikutano ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec)n a hata vikao vilivyokuwa vikifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyopo Lumumba.

  "Nape pia alitupa siri kwamba baadhi ya walioanzisha CCJ walikuwa wanakaribia kufukuzwa kwani katika mkutano wa NEC, majina ya baadhi yao yalitajwa na kujadilia kwenye kikao hicho.'


  Source: Mwananchi.

  My Take:
  Kama mwenyewe Nape hakanushi basi atakuwa ni hatari kwa chama chake kauli yake ya 'PAMOJA NA HAYO' inadhihilisha amebanwa kwenye kona.

  Sasa ndiyo wakati wa kupata mengi wengine tunajumlisha na kutoa siku ya siku tutakuja na jibu sahihi.
   
 2. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #2
  May 15, 2011
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kwa hiyo unachotuambia ni nini? Fine alikuwa mwanzilishi wa CCJ then what. Kwa sababu hata yeye alishiriki akiwa bado yuko CCM, je huo siyo unafiki. Kwa nini hakubaki ndani ya CCJ ili aijenge na kuifanya iwe maarufu badala ya kuhamia CDM? Hivi vyama ni kama mitumbwi ya kukuvusha ng'ambo kwa usalama. Lakini lililo la msingi ni kwamba yeye Nape yuko CCM na anatetea sera au misimamo ya chama chake , kama ambavyo na yeye Mpendazoe ana haki ya kutetea sera na misimamo ya Chadema.

  Hii siyo contest ya loyalty kwa chama hiki au kile, na ndiyo maana leo tunaona mwanasiasa huyu yuko kule na kesho yuko huku. Hata hiyo loyalty hupimwa wakati ukiwa ndani ya hicho chama na siyo baada ya kuondoka. Je Mpendazoe anataka kutuambia kwamba alipokuwa CCM kwa miaka yote hii hakuwa na loyalty na kwamba jicho lake lilikuwa kwenye upinzani? Naweza kuelewa frustrations za Mpendazoe hasa baada ya vigogo wenzanke kumchuuza ahame na wenzake watamfuata halafu wakamtosa lakini in politics kupima upepo huwa imo. Nani alijua leo hii Ntagazwa angekuwa huko aliko au Dr. Slaa huyu?

  Katika siasa haya yote hutokea na yanapotokea mtu hutakiwa kila la heri kule aendako na akishindwa na kurudi hasutwi. Waone Makongoro Nyerere, Wasira, Nsazugwanko na hao akina Mpendazoe, Shibuda, Kahigi, Slaa, Ntagazwa na wengine wengi.
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  May 15, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  sasa nagudua kwanini watu makini huwa hawakurupuki kuisakama cdm kwani mwisho wa siku utaumbuka..
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  May 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  kUMBE NDIO MAANA ANAHANGAIKA VILE??

  KWELI CCM HAWAKO MAKINI... PAMOJA NA KUWA NA DOLA NA SECURITY SYSTEM YOTE NA ITELLIGENCE, WAMESHINDWA KUJUA NAPE ALIKUA CCJ??
   
 5. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #5
  May 15, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Lol...Mh. Mpendazoe amenifurahisha sana...Nape hawezi kupinga hilo kwani ni Ukweli mtupu tena Mpendazoe amezungumza bila kuuma maneno...Mi ndo nilikuwa na Mh. Mpendazoe pale idara ya habari maelezo wakati anatangaza rasmi kuhama CCM na kuingia CCJ,wakati huo nilikuwa katibu mwenezi wa CCJ...
   

  Attached Files:

 6. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Hili gazeti mbona halijaibalance hii taarifa?zimewekwa tuhuma za EPA na tuhuma za Nape kugombea Ubunge kupitia Chadema bila kuweka majibu ya Nape kwenye masuala hayo, hii sio sahihi, i guess hili ni la Tanzania Daima hili, gazeti la Uhuru la Chadema.

  Kimsingi sioni hoja hapa, CCM inatambua kuwa kuna wanachama wake waliokuwa wamekatishwa tamaa na mwelekeo ya chama chao na ndipo walipokuja sasa na mpango wa kujivua gamba ili kuwarudishia wanachama hawa matumaini mapya na kuwafanya warudi kundini, kwa mantiki hiyo CCM hawana shida na Nape kuwahi kutaka kujitoa na kuanzisha CCJ, sasa pilipili wasiyoila yawawashia nini Chadema? naona Nape anawapa tabu sana.

  Lakini lingine...hivi unaenda Mbambabay unaongelea mambo ya Nape na CCJ wakati wananchi unaowaambia ata hawajui kama CCJ ni mdudu au ni mnyama? Huku ni kupoteza nafasi ya kuwaeleza wananchi mambo yanayowahusu wao na maisha yao na namna gani Chadema itayabeba matarajio na changamoto zao kwa kesho bora zaidi.
   
 7. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Siasa bwana..........,
   
 8. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #8
  May 15, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60

  Tehe tehe tehe tehe..Ndugu yangu inaonekana umekereheka kweli kuhusu Mpendazoe kumtaja Nape kama mmoja wa waanzilishi wa CCJ...Haha haha haha haha....Bila shaka Mpendazoe alitaka kuuelewesha UMMA ili ujue Nape ni nani na ni ukweli usiopingika kuwa ndo alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanatupa taarifa za nini kinaendelea ndani ya Serikali...Bado wapo wengine na kama alivyosema Mpendazoe tutawataja wakati utakapofika...CCM imejaa viongozi wanafki...Ambao wanajifanya CCM kumbe hamna lolote....Tehe tehe tehe...Asante sana Mpendazoe....
   
 9. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #9
  May 15, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Nawashangaa CCM wanamtegemea mtu kama NAPE awafikishe ng'ambo ya pili!
  At last mtu wa kufanya kazi ya NAPE awe ametulia, na ana historia ya kutosha na chama, na si kigeugeu!
  NDIYO haya ya kuchaguana kwa Nafasi aliyokuwa nayo Marehemu baba...Fadhila!
   
 10. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #10
  May 15, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kwa spidi hii, Huu mwaka tutajua mpaka rangi ya nguo zao za *****,
   
 11. Pasco_jr_ngumi

  Pasco_jr_ngumi JF-Expert Member

  #11
  May 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 1,811
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  ndo raha ya kimbelembele......................napeeeeeeeeee,,,,,,,, ingia CHADEMAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
   
 12. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #12
  May 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  almost a cr@p
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  May 15, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  chadema wala ccm hawahitaji myopic nape

  they need someone better
   
 14. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #14
  May 15, 2011
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Mkuu PJ,

  Kila siku naendelea kumnukuu Napoleon Bonaparte.....Never interrupt your Enemy when he's making a mistake.

  Walipojivua gamba tu,kabla hata hawajatoka katika chumba cha mkutano wao wa NEC nilishangilia,kwa kweli CCM ni dhaifu kuliko tunavyofikiria.Loh,vituko
   
 15. Rejao

  Rejao JF-Expert Member

  #15
  May 15, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 9,239
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Siasa tamu sana! Kumbe Nape ana uchu wa madaraka kiasi hicho? Shame upon you Nape! Unaidhalilisha CCM
   
 16. F

  FJM JF-Expert Member

  #16
  May 15, 2011
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Nape ajifunze toka kwa Lowassa. Siku zote Lowassa amekuwa anaongelea sera na si issue za mtu mmoja mmoja tena personal isssues. Hivi Nape hajiulizi pamoja na 'wingu' zito linalomzunguka Lowassa kwa nini haongelewi sana kwenye mikutano ya hadhara? Na sio tu Nape, ni vigumu sana kwa kiongozi yeyote toka ccm (hata wa kata) kuanzisha siasa za mambo binafsi maana wana 'skeleton' wengi mno kwenye makabati yao.

  Sikio la kufa... - And I am sure kuna mambo zaidi ndani ya kabati la Nape.
   
 17. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #17
  May 15, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,060
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mbopo kama huoni tatizo wewe utakuwa na tatizo, uaminifu wa Nape kwa chama chake uko wapi mtu anataka kukisaliti chama kabaki huko kwa sababu ya u-DC bado mnaamini kweli ni loyal kwa chama if so then something is wrong somewhere in CCM, kitakuwa ni opportunistic party ndiyo maana kuna siku Prof. Safari na Marando walisema kama ni unafiki Nape ni number one siku ile sikuwaelewa.
   
 18. Sizinga

  Sizinga JF-Expert Member

  #18
  May 15, 2011
  Joined: Oct 30, 2007
  Messages: 7,922
  Likes Received: 454
  Trophy Points: 180
  Dah jamaa kweli alikuwa na uchu wa madaraka
   
 19. Butola

  Butola JF-Expert Member

  #19
  May 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,221
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mkuu wala hakuna shida hapo.

  Ninachokiona hapa ni Chadema sasa kuanza kucheza ngoma ya Nape na kumpa Nape sifa ya "mpambanaji aliyekuwa hajaridhishwa na mambo yalivyokuwa yanaendelea ndani ya CCM", hii itawapa zaidi hamasa wananchi ya kutaka kumsikiliza zaidi na kumwamini pale anaposema CCM inabadilika na sasa mafisadi hawana nafasi, itamsaidia sana hii publicity kujenga case yake ya CCM mpya iliyojivua gamba.

  Hoja hii itawafanya wasio wanaCCM wamwamini zaidi anapozungumzia kubadilika kwa CCM na kuwapa mtazamo wa pili wale waliokuwa wamekatishwa tamaa na CCM kama alivyokuwa yeye sababu ya kurudi kundini.

  Hii ni strength kwa Nape na wala sio weakness kama mnavyodhani, hii publicity ya Nape kama mtu aliyekuwa hajaridhishwa na mambo yalivyokuwa yanaenda ndani ya CCM inampa sasa opportunity nzuri ya kuwafikia wote waliokuwa wamekatishwa tamaa na CCM na ufisadi uliokuwa unaendelea.

  Chadema walipaswa walione hili kabla majuto hajawa mjukuu.
   
 20. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #20
  May 15, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,908
  Likes Received: 12,060
  Trophy Points: 280
  Bwana Butola kama unadhani hii ni strength kwa Nape ni mawazo yako wengine tunaona ni kama kijana kadandia treni kwa mbele, unafikiri ndani ya CCM hakuna watu wanaoweza kusema kama anavyofanya yeye, jibu ni rahisi tu wanajijua madhambi yao hawataki kuanzisha vita vya mawe wakati wao wako kwenye nyumba ya kioo, wamemtanguliza Nape kama kafara wao sasa aangalie watakavyomruka hataamini macho yake. Ni hivi karibuni tu utasikia Nape anavutwa shati na kutulizwa amuulize Magufuri na Tibaijuka, si umesikia kuna vigogo sita waanzilishi wa CCJ ambao bado wako CCM na vyeo vyao sasa unadhani watapenda kutajwa kama alivyotajwa Nape.
   
Loading...