Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Mchunguzeni Mpendazoe alipokuwa NEMC alifanya mema? Je yuko tayari tumchunguze?


Mkuu mjadala huu umetekwa na partisan interests kiasi cha kwamba watu hawataki tena kufanya reasoning, kama hiyo reasoning itamaanisha watu kukubali hili au lile mradi aliyetoa hoja anakuwa perceived kuwa wa chama hiki au kile. Hakuwa uhusiano kati ya harakati za Nape kwenye CCJ na kupewa kwake u-DC maana kama ulivyosema, it took months toka wakati wa harakati za CCJ mpaka hapo alipoukwaa u-DC na hapo katikati alishiriki kura za maoni za kuwania ubunge kwa tiketi ya CCM. Wakati wote huo Mpendazoe alikuwa ameshatoka CCJ na kuelekea Chadema na hata kushiriki kwenye kura za maoni Segerea na kushindwa na Rachel Mashishanga na hata kutaka kukimbilia jimbo la Kinondoni. In my view obsession ya Mpendazoe ilikuwa ni ubunge bila kujali ni wapi.

Hoja ni kwamba, hata kama Nape alishiriki kuiasisi CCJ, hakuna wakati hata mmoja aliosimama popote pale ku-renounce CCM au kumsema vibaya Rais na wakati huo wote alikuwa mjumbe wa NEC-CCM. Hapa unafiki unaingiaje? Kwa kutohama kutoka CCM kwenda chama kingine baada ya kuanguka kwa CCJ? Kama ni hivyo basi asiishie kwa Nape, awataje na wengine ambao tunajua walikuwa watoke Chadema pia. Nape amekuwa mpambanaji dhidi ya ufisadi wa ndani ya CCM na alikuwa very clear juu ya hao anaowahusisha na ufisadi na hakuna hata wakati mmoja alipata kutamka kwamba JK ni mmoja wao, sasa hicho kinachoitwa kuzawadiwa cannot arise. Tunaweza kusema if anything, aliyezawadiwa ni Mpendazoe aliyepewa nafasi ya kugombea baada ya kushindwa kwenye primaries.
 
Penye red:

CCM inawajua fika, na isipoanza kuwataja wengine, basi ingojee kuumbuliwa zaidi na Mpendazoe, ambaye bila shaka ataendelea kuwataja wale wengine. CCM haijui ifanye nini katika hili suala maana wale wengine ambao haijawataja Jk tayari amewapa vyeo -- sijui kwa nini. Hawa ni Sitta na Mwakyembe. Pia yuko ule Makonda wa UVCCM mkoa wa Kilimanjaro.

Nionavyo mimi hii tutaona mengi katika hii pandora box aliyoifungua Mpendazoe na utabiri wangu ni kwamba hii ndiyo mwisho wa Nape. Nape angekuwa sharp na witty, angetambua hilo kuweza kutokea na angeweza ku-preempt -- kwa yeye kusema kwamba alijifanya kujiunga CCJ ili kupata siri ya vigogo gani wa CCM wanaisapoti au walikuwa tayari kujiunga na chama hicho. Angalau hapo Nape angepona.

Lakini pia huenda ni kweli alipewa kazi hiyo na chama chake CCM kuifanya (even though this is highly unlikely) lakini baadaye JK alikosa ujasiri (kama kawaida yake) ya kuchukuwa hatua ya kufaa kuwatimua vigogo wote waCCM wale walijihusisha na CCJ.

By the way -- Where is mzee wetu Mwanakijiji? Aliishabikia sana CCJ na bila shaka anaelewa mengi. Huu siyo wakati wa kumwaga yale yaliyojiri? Come on MMKJJ!!
!


Yes -- yuko wapi MMKJJ? Nakumbuka aligomabana na baadhi ya wanaJF humu kutokana na ushabiki wake kwa CCJ. Atueleze yote sasa.
 
Lol...Mh. Mpendazoe amenifurahisha sana...Nape hawezi kupinga hilo kwani ni Ukweli mtupu tena Mpendazoe amezungumza bila kuuma maneno...Mi ndo nilikuwa na Mh. Mpendazoe pale idara ya habari maelezo wakati anatangaza rasmi kuhama CCM na kuingia CCJ,wakati huo nilikuwa katibu mwenezi wa CCJ...

we dickson,hebu jaribu kuwa mtu mzima,si wewe na mpendazote mlokuwa na mkakati wa kuhakikisha CCJ inakufa ili kuimarisha chadema? na yakini kwa kuwa nilikuwa pale makuu ya CCJ kabla na baada ya uharimia wenu wewe,mpendazote na richard,nawajua kindakindaki,mwacheni nape ni mpiganaji wa ukweli,sio longolongo!
 
he! ina maana hawa wachaga ndo wamemteua mpendazote kuwa mkurugenzi wa kitengo cha propaganda? kama tambwe kule CCM?
 
Mwenzetu umejaaliwa matusi ya reja reja na hatuwezi kukubadilisha. Inawezekana kabisa hapo ulipo hata mlo ni tatizo na mimi naomba nikuambie tu kwamba huyo Nape simfahamu personally lakini hapa niko driven na issues bila kujali ni Nape au mwingine yeyote. My reasoning does not revolve around personalities unless personality is an issue.

Tunarudia tena kusema kwamba Mpendazoe has alot of more important issues to address that revealing his bitterness about how he thinks he was duped into jumbping ship to found CCJ. He should recover and continue serving wananchi honourably! If he thinks Nape is wrong discussing people within Chadema, he (Mpendazoe) shouldn't have allowed himself to stoop as low. My feeling remains that the useless sideshows would end if the leaders from across the political devide decide to re-trace their route and serve what is in the best interest of wananchi.
Pole sana ndugu yangu kwa kazi ya kuzoa maji yaliyomwagika jitahidi unaweza ambulia hata nusu glass lakini yatakuwa machafu, kilichobaki si kutetea usaliti wake kwa kuuza siri za makao makuu kwa CCJ ni jinsi gani atairudisha imani yake kwetu, yeye afanye kazi aliyotumwa na NEC asijiingize kwenye siasa za maji taka za kuchokoza mishahara ya wapendwa wa watu wenye hasira za maisha atamwagiwa maji ya oil chafu asiweze takata tena ni ushauri tu.
 
Huu utaratibu Wa kila anayekosoa Chama chetu tunamuandama kwa style ya character assassination Nadhani sio mzuri unafanya CDM ionekane kazi yake kuchafua watu. Ushauri wangu ni kujibu tuhuma kuliko kuandama watu. Huyu Mpendazoe alikuwa wapi kuyasema haya? Ataibuka mwingine naye ataandamwa vivyo hivyo ....

- Mkuu this is great, kwa sababu finally tunaanza kupata the juice from both sides, Chadema wasichoelewa kwenye huu mchezo mpya ni kwamba wananchi wamezoea kusikia machafu ya CCM, tatizo ni kwamba hawajawahi kusikia machafu ya Chadema, sasa the more this game is played ni the more tutasikia mapya machafu ya Chadema!

- Hivi ni vita vya moral authority, ambayo Chadema wamekuwa wakii-command kwa muda mrefu sana, lakini not anymore since last week ndio maana tumewaambia Chadema, wanahitaji mabadiliko ya agenda now maana kwa mwendo huu wa akina Mpendazoe, Chadema is going to pay a very heavy political price, I mean in the end ni uamuzi wa Chadema!

- Can you imagine CCM wakianza kusema jinsi ambavyo wamekua wakimtumia Marando since the formation ya vyama vingi?

Es!
 
Kwa hiyo unachotuambia ni nini? Fine alikuwa mwanzilishi wa CCJ then what. Kwa sababu hata yeye alishiriki akiwa bado yuko CCM, je huo siyo unafiki. Kwa nini hakubaki ndani ya CCJ ili aijenge na kuifanya iwe maarufu badala ya kuhamia CDM? Hivi vyama ni kama mitumbwi ya kukuvusha ng'ambo kwa usalama. Lakini lililo la msingi ni kwamba yeye Nape yuko CCM na anatetea sera au misimamo ya chama chake , kama ambavyo na yeye Mpendazoe ana haki ya kutetea sera na misimamo ya Chadema.

Hii siyo contest ya loyalty kwa chama hiki au kile, na ndiyo maana leo tunaona mwanasiasa huyu yuko kule na kesho yuko huku. Hata hiyo loyalty hupimwa wakati ukiwa ndani ya hicho chama na siyo baada ya kuondoka. Je Mpendazoe anataka kutuambia kwamba alipokuwa CCM kwa miaka yote hii hakuwa na loyalty na kwamba jicho lake lilikuwa kwenye upinzani? Naweza kuelewa frustrations za Mpendazoe hasa baada ya vigogo wenzanke kumchuuza ahame na wenzake watamfuata halafu wakamtosa lakini in politics kupima upepo huwa imo. Nani alijua leo hii Ntagazwa angekuwa huko aliko au Dr. Slaa huyu? Katika siasa haya yote hutokea na yanapotokea mtu hutakiwa kila la heri kule aendako na akishindwa na kurudi hasutwi. Waone Makongoro Nyerere, Wasira, Nsazugwanko na hao akina Mpendazoe, Shibuda, Kahigi, Slaa, Ntagazwa na wengine wengi.

It's a pity and sad that a grown up like you do not know what loyalty mean!
 
- Mkuu this is great, kwa sababu finally tunaanza kupata the juice from both sides, Chadema wasichoelewa kwenye huu mchezo mpya ni kwamba wananchi wamezoea kusikia machafu ya CCM, tatizo ni kwamba hawajawahi kusikia machafu ya Chadema, sasa the more this game is played ni the more tutasikia mapya machafu ya Chadema!

- Hivi ni vita vya moral authority, ambayo Chadema wamekuwa wakii-command kwa muda mrefu sana, lakini not anymore since last week ndio maana tumewaambia Chadema, wanahitaji mabadiliko ya agenda now maana kwa mwendo huu wa akina Mpendazoe, Chadema is going to pay a very heavy political price, I mean in the end ni uamuzi wa Chadema!

- Can you imagine CCM wakianza kusema jinsi ambavyo wamekua wakimtumia Marando since the formation ya vyama vingi?

Es!
Najua kama Marando angekuwa anatumika kuivuruga CDM wala ungetuambia, sisi watu wazima ati.
 
Hili gazeti mbona halijaibalance hii taarifa?zimewekwa tuhuma za EPA na tuhuma za Nape kugombea Ubunge kupitia Chadema bila kuweka majibu ya Nape kwenye masuala hayo, hii sio sahihi, i guess hili ni la Tanzania Daima hili, gazeti la Uhuru la Chadema.

Kimsingi sioni hoja hapa, CCM inatambua kuwa kuna wanachama wake waliokuwa wamekatishwa tamaa na mwelekeo ya chama chao na ndipo walipokuja sasa na mpango wa kujivua gamba ili kuwarudishia wanachama hawa matumaini mapya na kuwafanya warudi kundini, kwa mantiki hiyo CCM hawana shida na Nape kuwahi kutaka kujitoa na kuanzisha CCJ, sasa pilipili wasiyoila yawawashia nini Chadema? naona Nape anawapa tabu sana.

Lakini lingine...hivi unaenda Mbambabay unaongelea mambo ya Nape na CCJ wakati wananchi unaowaambia ata hawajui kama CCJ ni mdudu au ni mnyama? Huku ni kupoteza nafasi ya kuwaeleza wananchi mambo yanayowahusu wao na maisha yao na namna gani Chadema itayabeba matarajio na changamoto zao kwa kesho bora zaidi.

Pole sana ndugu yangu ufahamu wako ni finyu sana. Hivi mpaka leo hujui maana ya utandawazi? kama habari zilikuwa zinahusu watu wa mbamba bay tu sasa wewe zimekufikiaje? hivi jk anapotoa hotuba akiwa dar inakuwa kwa ajili ya watu wa dar tu? au anakuwa anazungumzia watu wa dar tu? wake up man!UTANDAWAZIIIII
 
Najua kama Marando angekuwa anatumika wala ungetuambia sisi watu wazima ati.

- Hivi vita vya kelele zisizo na tija kwa taifa haviwezi kuisaidia Chadema kwa sababu vinaisaidia CCM kutojadili hoja muhimu kwa taifa, na the more vikiendelea ni the more Chadema will lose, Marando alikuwa anatafuta nini kwenye ndege ya Rais Mkapa kila wakati, kule EAC alipelekwa na nani? ha! ha! ha! ndio maana ninasema kwa njia hii mpya ya kuchafuana Chadema will pay more kuliko CCM ambao wamezoewa na machafu!

Es!
 
Sasa naelewa ni kwanini walijiita "Sisi jee?" Means waliona wameachwa kwenye ulaji,wakapiga kelele,wamepewa ulaji sasa wamegeuka attacking dogs.Ni bora wangesema ukweli tu kuwa Mpendazoe hawakumfavor kwasababu si mtoto wa Kigogo,ama hajatokea kwenye lile tabaka.
 
- Mkuu this is great, kwa sababu finally tunaanza kupata the juice from both sides, Chadema wasichoelewa kwenye huu mchezo mpya ni kwamba wananchi wamezoea kusikia machafu ya CCM, tatizo ni kwamba hawajawahi kusikia machafu ya Chadema, sasa the more this game is played ni the more tutasikia mapya machafu ya Chadema!

- Hivi ni vita vya moral authority, ambayo Chadema wamekuwa wakii-command kwa muda mrefu sana, lakini not anymore since last week ndio maana tumewaambia Chadema, wanahitaji mabadiliko ya agenda now maana kwa mwendo huu wa akina Mpendazoe, Chadema is going to pay a very heavy political price, I mean in the end ni uamuzi wa Chadema!

- Can you imagine CCM wakianza kusema jinsi ambavyo wamekua wakimtumia Marando since the formation ya vyama vingi?

Es!

hivi vyama sasa vinapotea njia sasa, watanzania hawaitaji nani ni nani.alifanya nini na wapi.
they want food on the table.tuongee kutokomeza umaskini siyo nape,mpendazoe hao wote ni opportunist.binafsi namfahamu sana nape na yeye analijua hilo his weekeness and strong lakini kuziweka hapa haziwasaidii wa tz.kwahiyo mkuu FS na wewe usiingie kwenye mtego huo.
 
Mkuu wala hakuna shida hapo.

Ninachokiona hapa ni Chadema sasa kuanza kucheza ngoma ya Nape na kumpa Nape sifa ya "mpambanaji aliyekuwa hajaridhishwa na mambo yalivyokuwa yanaendelea ndani ya CCM", hii itawapa zaidi hamasa wananchi ya kutaka kumsikiliza zaidi na kumwamini pale anaposema CCM inabadilika na sasa mafisadi hawana nafasi, itamsaidia sana hii publicity kujenga case yake ya CCM mpya iliyojivua gamba.

Hoja hii itawafanya wasio wanaCCM wamwamini zaidi anapozungumzia kubadilika kwa CCM na kuwapa mtazamo wa pili wale waliokuwa wamekatishwa tamaa na CCM kama alivyokuwa yeye sababu ya kurudi kundini.

Hii ni strength kwa Nape na wala sio weakness kama mnavyodhani, hii publicity ya Nape kama mtu aliyekuwa hajaridhishwa na mambo yalivyokuwa yanaenda ndani ya CCM inampa sasa opportunity nzuri ya kuwafikia wote waliokuwa wamekatishwa tamaa na CCM na ufisadi uliokuwa unaendelea.

Chadema walipaswa walione hili kabla majuto hajawa mjukuu.

Ndugu yangu Butola...unafikiri 2namjengea ushujaa?...Hata kidogo wewe subiri utaona....
 
Pole sana ndugu yangu ufahamu wako ni finyu sana. Hivi mpaka leo hujui maana ya utandawazi? kama habari zilikuwa zinahusu watu wa mbamba bay tu sasa wewe zimekufikiaje? hivi jk anapotoa hotuba akiwa dar inakuwa kwa ajili ya watu wa dar tu? au anakuwa anazungumzia watu wa dar tu? wake up man!UTANDAWAZIIIII

My Point is,unaweza ukaongea na wananchi wa Dar es Salaam kutokea Mbambabay lakini hauwezi kuongea na wananchi wa Mbambabay kutokea Dar es Salaam; huko wananchi wanasikiliza redio binafsi za Malawi tu usiniulize TV na magazeti,sasa ukizingatia kuwa Chadema wanapata chance ya kuongea na Wananchi hao mara moja katika kipindi cha miaka 5 wakati wapinzani wao wa CCM wapo huko fulltime, ni vyema basi Chadema wautumie muda huo vizuri kujenga case yao kwa wananchi hao ili ata wasipoisikia Chadema kwa miaka 2 ijayo bado mioyoni mwao wakumbuke kuna serikali mbadala bora zaidi katika Chadema itakayobeba matarajio yao ya kesho, vinginevyo unaweza ukajikuta umezunguka sana lakini ukashindwa kuweka mizizi yako kwenye maeneo husika, ni ushauri tu!!
 
Back
Top Bottom