Vita umeanza mwenyewe, sasa unalia nini?
Nape unarusha mawe, Vita umeianzishaa!
Mawe warusha vyovyote, hata hauna malengo
Ulianza na Mafisadi, sasa umewagwaya
Mara Slaa mwana zuoni, jiwe ukamrushia,
Umekuwa kama chizi, Unarusha bila dira,
Dawa ya moto motoni, Dawa ya mawe unaipata,
Ulianza na Mafisadi, Aibu umeipata
Aibu umeipata, Mafisadi sasa wako
Sasa unawatetea, Magamba ni nguo zako
Umma hauna chelea, wanapima kwa vigezo
Ulianza na Mafisadi, sasa umetota jasho
Vita umeianzisha, subiri utaipata
Wameanza kupuuza, kumbe hauna dira
Dira yako yote tamaa, na uchu wa madaraka
Ulianza na Mafisadi, sasa unawatetea
Eti kwa ufinyu wako, wadhani bado twalala,
wataka kutuadaa, ili kutupumbaza,
Hatudanganyi kwa kanga, kwa chumvi wala kofia
Ulianza na Mafisadi, mbona wamekushinda
Shirikisha akilizo, Fikiri kabla ya kunena,
Mja na mwana vitendo, Tanzania ndio baba,
Tetea kwanza nchi yako, ndipo utaeleweka,
Mafisadi ulianza nao, sasa unawatetea.