Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Nape ni mwanzilishi wa CCJ

amewashika pabaya chadema mnaanza kutumia zomea zomea yenu kumnyamazisha.

huwezi nyamazisha ukweli.
Kumetokea mtindo kila mwana CCM anasema Nape kawashika CDM halafu wanafuraaaahiiiiii kwa kutamka tu lakini kila nikiangalia alipowashika wala sipaoni au yeye ndiye kaminywa nini.
 
Hii ndiyo CCM. Rushwa inanukia kila mahali. Maskini hawa watu hawajui hizo kanga ni hela zao za Kodi zilizoibiwa na CCM ! Sasa huyu ametumwa kuhamasisha wananchi au kugawa takrima ??? Ni aibu Kubwa.
attachment.php

Alipoambiwa kwenda kueneza sera za chama yeye akafikiri ni kueneza kanga za chama.
 
yani huyu dogo namsikitikia sana kwa sababu anajua uozo ulioko ccm lakini kaamua kuivuta hyo harufu chafu ya magamba ya nyoka hakika kipindi hichi analo
 
KADA wa Chadema, Fred Mpendazoe amewataja mawaziri wawili wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, mbunge mmoja wa CCM na makada wengine wawili wa chama hicho tawala kuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa katika harakati za kukihama na kujiunga na CCJ. Mpendazoe ambaye alikuwa kada wa kwanza wa CCM kuhamia CCJ wakati huo akiwa Mbunge wa Kishapu, aliwataja waanzilishi hao wa CCJ kuwa ni pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri mmoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

Kwa mujibu wa Mpendazoe, katika kundi hilo pia wamo kada wa Jumuia ya Umoja wa Vijana wa CCM na mbunge mmoja kutoka Mkoa wa Mbeya. Hatukuandika majina ya baadhi ya viongozi waliotajwa kwa sababu hatukufanikiwa kuwapata kujibu tuhuma hizo.Hata hivyo, Sitta alipipogiwa simu alisema asingeweza kuzungumza lolote kuhusu madai hayo akisema anasubiri kusoma alichosema Mpendazoe.

Mpendazoe aanika walioanzisha CCJ
 
Kwa kuwa team nzima ya CDM, imeshajulikana kuwa inatumika kama presha group na horse,s mouth ya mafisadi wa ndani na nje ya CCM, wala sishangai kauli ya Mpendazoe.
 
good to know these things as they reveal true colors of our leaders and where they stand in principle
 
Sasa nadhani wananchi wameanza kuijua vizuri CCM na watu wake, huyu Nape mwezi uliopita alikuwa anatutangazia kujivua gamba ni kuwaondoa Lowassa, Rostam na Chenge hiyo wameona haiwezekani sasa wamebadilisha slogan wanasema chama kimezeeka sasa kujivua gamba ni kubadilisha mfumo ili kiendane na wakati. Mimi naomba tuendelee kuhesabu siku zikifika 90 ndio tutaijua CCM vizuri
 
KADA wa Chadema, Fred Mpendazoe amewataja mawaziri wawili wa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete, mbunge mmoja wa CCM na makada wengine wawili wa chama hicho tawala kuwa ni miongoni mwa watu waliokuwa katika harakati za kukihama na kujiunga na CCJ. Mpendazoe ambaye alikuwa kada wa kwanza wa CCM kuhamia CCJ wakati huo akiwa Mbunge wa Kishapu, aliwataja waanzilishi hao wa CCJ kuwa ni pamoja na Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na Naibu Waziri mmoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.

Kwa mujibu wa Mpendazoe, katika kundi hilo pia wamo kada wa Jumuia ya Umoja wa Vijana wa CCM na mbunge mmoja kutoka Mkoa wa Mbeya. Hatukuandika majina ya baadhi ya viongozi waliotajwa kwa sababu hatukufanikiwa kuwapata kujibu tuhuma hizo.Hata hivyo, Sitta alipipogiwa simu alisema asingeweza kuzungumza lolote kuhusu madai hayo akisema anasubiri kusoma alichosema Mpendazoe.

Mpendazoe aanika walioanzisha CCJ
Hapo ndipo JK ajue ana kazi ya ziada ndani ya chama chake.
 
SIJUI NIKUITE KAKA AMA DADA LAKINI NWAY,NASHUKURU KWA BUSARA ZAKO NDUGU YANGU NA KUANDIKA LUGHA AMBAYO CDHANI KAMA NI SAHIHI LAKINI HAMANA SHIDA,uBARIKIWE SANA....

Sikuwa na mfano wa kulinganisha na matendo yenu ya kizandiki, I am sorry if I offend you, acha tu nikukumbushe lugha ya siasa haina mipaka utaitwa mwizi, malaya, muongo,jaribu kuwa mvumilivu, mwambie jamaa yako Mpendazoe siasa za uongo majukwaani hazitamfikisha popote, kwa ujumla kisiasa hata kwenye jimbo lake la kishapu alikuwa hakubaliki tena. Labda nikuulize maswali ya msingi kwanini hamkuendelea na juhudi zenu za kuisajili CCJ? Je ilikuwa kuna ulazima gani kwenu kushiriki kwenye uchaguzi mkuu wakati chama kilikuwa bado kichanga? Uchu wa madaraka na tamaa ya fedha ndizo zilizowakwamisha msimtumie Nape kwenye kufeli kumbuka PENYE NIA PANA NJIA kama mlikuwa na nia ya kumkomboa mtanzania msingefeli. Mlikimbilia Chadema si kwa sababu ya sera ndio maana mlishinikiza mpewe nafasi za kugombania ubunge, kumbuka suala la Nape kujiunga ama kutokujiunga CCJ ni suala binafsi na ni lazima liheshimiwe ni sawa sawa na mchungaji Slaa alivyoikimbia kazi ya utumishi wa Mungu na kujiingiza kwenye siasa. Nape tutamhukumu sisi wenyewe CCM. Mwageni sera za maendeleo, acheni siasa za uongo na unafiki
Chama
Gongo la Mboto DSM.
 
Yeye alikurupuka na kuachia Ubunge,unajua hata baba wa taifa alisema mtu akikueleza jambo la kipumbavu wakati anajua ni la kipumbavu na wewe ukakubaliana nae anakudharau sana kwani anajua kuwa na wewe unajua ni la kipumbavu na ukakubaliana nalo.hii ndiyo iliyotokea kwa Mpendazoe na hao werevu sita anaowasema majuto mjukuu.:dance:
 
Ndungu Nape, Kada machachari wa CCM,
Kwanza napenda kukupongeza kwa kupewa nafasi kubwa sana katika Chama Cha Mapinduzi. Mimi binafsi naamini kwamba jukumu ulilopewa ni kubwa sana kwa kulinganisha na umri na uzoefu wako. Kwa hiyo, nakushauri

(1) kutafuta ushauri mkubwa na kushirikiana kwa ukaribu sana na viongozi wasistafu na wale wenye uzoefu mkubwa na Chama.
(2) Usijibu tuhuma zozote ndani ya muda mfupi kwani waweza usiwe umejipanga vizuri. Sasa hivi tuhuma zitakuwa nyingi sana kwani upinzani ulionao sasa ni ndani ya Chama (wenye nguvu zaidi) na nje ya Chama. Tuhuma zozote za chama au za kwako, shauriana na hawa wazee wasitafu ili wakusaidie jinsi ya kujibu.
(3)Angalia mwelekeo wa wakubwa kama unaendana na maneno, akili na matendo yao ili usijeukawa unakimbia pekee yako huku wengine wakikuzomea badala ya kukushangilia.

Narudia tena jukumu ulilopewa ni kubwa kuliko umri na uzoefu wako. Yatakuandama mengi sana tena yenye changamoto nyingi sana na usipokuwa makini siasa zako zinaweza kuwa ngumu sana baadaye.

Asante.
 
Mweleze Kijana ila ana uhuru wa Kuchagua Mbivu na Mbichi!! Kula la Kheri Napa Kanyaga Twende
 
Ni kweli kabisa, huyu dogo kapewa majukumu makubwa sana na kukisemea chama cha CCM! Kumbuka unachosema hadharani ndilo tamko la CCM, kwa hiyo uwe makini, usiropoke hovyo hovyo! Hakuna atakayekulaumu kwa kuchelewa kujibu hoja ila utalaumiwa kwa kutoa majibu yatakayozidi kukiangamiza chama bila ya wewe kujua. Waona wazee wako, wapo wenye busara na uzoefu wa kujibu tuhuma, siyo kuropoka tu. Na kumbuka hiyo nafasi yako wapo wengi wanaitamani, na wapinzani wako ndani ya chama wana nguvu kuliko unavyofikiri wewe
 
mshauri, awaUlize wakongwe watamwelimisha, mfupa uliomshinda makamba yeye anaufakamia bila mahesabu - alitakiwa ku-differentiate
dy over dx when x approching 0, bila hivyo sasa haya ndiyo madhara yake.
 
Alikosea sana kusimama majukwaani na kuanza kuwanyooshea vidole waleeeee, ALIPASWA KUTUMIA HEKIMA NA BUSARA NYINGI KATIKA KUFIKISHA UJUMBE NA SI KUPAYUKA PASIPO VITENDO MADHUBUTI. NA ZOEZI LAO LIKISHINDWA BASI ITAKUWA NI FEDHEHA KUBWA NA MWANZO WA KUPOROMOKA KWAKE, IPO SIKU ATATAMANI KUJIVUA GAMBA.
 
Ushauri mzuri na si kwa Nape tu,bali kwa viongozi na wanasiasa wengine wote including upinzani.Hata kwenye maisha yetu ya kawaida pia una apply.Ukishutumiwa au unapotaka kusema kitu au kujenga hoja,usikurupuke.Tulia,ondoa jazba/hasira,jipange,tafiti,omba ushauri kwa wenzio wenye uzoefu/hata wasio na uzoefu,kisha changanya na za kwako-halafu ndiyo unatoka public.
 
Ndungu Nape, Kada machachari wa CCM,
Kwanza napenda kukupongeza kwa kupewa nafasi kubwa sana katika Chama Cha Mapinduzi. Mimi binafsi naamini kwamba jukumu ulilopewa ni kubwa sana kwa kulinganisha na umri na uzoefu wako. Kwa hiyo, nakushauri

(1) kutafuta ushauri mkubwa na kushirikiana kwa ukaribu sana na viongozi wasistafu na wale wenye uzoefu mkubwa na Chama.
(2) Usijibu tuhuma zozote ndani ya muda mfupi kwani waweza usiwe umejipanga vizuri. Sasa hivi tuhuma zitakuwa nyingi sana kwani upinzani ulionao sasa ni ndani ya Chama (wenye nguvu zaidi) na nje ya Chama. Tuhuma zozote za chama au za kwako, shauriana na hawa wazee wasitafu ili wakusaidie jinsi ya kujibu.
(3)Angalia mwelekeo wa wakubwa kama unaendana na maneno, akili na matendo yao ili usijeukawa unakimbia pekee yako huku wengine wakikuzomea badala ya kukushangilia.

Narudia tena jukumu ulilopewa ni kubwa kuliko umri na uzoefu wako. Yatakuandama mengi sana tena yenye changamoto nyingi sana na usipokuwa makini siasa zako zinaweza kuwa ngumu sana baadaye.

Asante.
LINCOLINMTZA, ni ushauri mzuri ila ili ushauri huu umfikie mlengwa, nakushauri mpostie kwenye wall yake kule fb ambako wana CCM ndiko wanakoshinda kutwa kucha kwa kusifiana na kuiimbiana nyimbo za shangwe na mapambio, kwa vile wanaamini jf ni ya Chadema!.

Mkuu Nape ni memba humu, baada ya kupata ulaji mnene, ameshauriwa atembelee jf wakati akiwa hana cha kufanya, unfortunatelly amekuwa busy sana, hajakosa cha kufanya ikiwemo kushinda fb ni sehemu ya shughuli zake!.
 
Kwa hiyo unachotuambia ni nini? Fine alikuwa mwanzilishi wa CCJ then what. Kwa sababu hata yeye alishiriki akiwa bado yuko CCM, je huo siyo unafiki. Kwa nini hakubaki ndani ya CCJ ili aijenge na kuifanya iwe maarufu badala ya kuhamia CDM? Hivi vyama ni kama mitumbwi ya kukuvusha ng'ambo kwa usalama. Lakini lililo la msingi ni kwamba yeye Nape yuko CCM na anatetea sera au misimamo ya chama chake , kama ambavyo na yeye Mpendazoe ana haki ya kutetea sera na misimamo ya Chadema.

Hii siyo contest ya loyalty kwa chama hiki au kile, na ndiyo maana leo tunaona mwanasiasa huyu yuko kule na kesho yuko huku. Hata hiyo loyalty hupimwa wakati ukiwa ndani ya hicho chama na siyo baada ya kuondoka. Je Mpendazoe anataka kutuambia kwamba alipokuwa CCM kwa miaka yote hii hakuwa na loyalty na kwamba jicho lake lilikuwa kwenye upinzani? Naweza kuelewa frustrations za Mpendazoe hasa baada ya vigogo wenzanke kumchuuza ahame na wenzake watamfuata halafu wakamtosa lakini in politics kupima upepo huwa imo. Nani alijua leo hii Ntagazwa angekuwa huko aliko au Dr. Slaa huyu?

Katika siasa haya yote hutokea na yanapotokea mtu hutakiwa kila la heri kule aendako na akishindwa na kurudi hasutwi. Waone Makongoro Nyerere, Wasira, Nsazugwanko na hao akina Mpendazoe, Shibuda, Kahigi, Slaa, Ntagazwa na wengine wengi.

You sound too rhetoric my friend.

Ukweli unabaki palepale NNAPE NAUYE SI MWAMINIFU NDANI YA CCM na the way Mpendazoe put it, Nnape Nnauye is one of the most hypocratic guys in CCM by the moment.

Huyu jamaa inafaa atimuliwe toka CCM maana inaonekana bado ana harufu ya CCJ na si ajabu bado ana mikakati ya kuendelea na uaNzishaji wa chama kingine baada ya CCJ kusambaratika. Ukimsikiliza kwa makini yale anayoongea si ya kweli baali ni ya kutaka kuisambaratisha CCM!Bado ana hasira na EL,AC na RA.

Tunaambiwa kwamba yale anayoongea Nnape si yale waliyokubaliana kwenye Central Comittee. Habari za kuaminika zinalonga kwamba EL alimfuata JK kuhusiana na tetesi za kwamba EL,RA na AC wamepewa siku 90 wajitoe CCM vinginevyo watang'olewa kwa nguvu. Unajua JK alimjibu nini EL?HAKUNA KITAKACHOTOKEA, that means kelele zote za Nnape ni USANII TU nothing is gonna happen! Upo hapo????
 
LINCOLINMTZA, ni ushauri mzuri ila ili ushauri huu umfikie mlengwa, nakushauri mpostie kwenye wall yake kule fb ambako wana CCM ndiko wanakoshinda kutwa kucha kwa kusifiana na kuiimbiana nyimbo za shangwe na mapambio, kwa vile wanaamini jf ni ya Chadema!.

Mkuu Nape ni memba humu, baada ya kupata ulaji mnene, ameshauriwa atembelee jf wakati akiwa hana cha kufanya, unfortunatelly amekuwa busy sana, hajakosa cha kufanya ikiwemo kushinda fb ni sehemu ya shughuli zake!.

Pasco maneno mazito lakini ya ukweli !
 
Back
Top Bottom