Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Nape ni mwanzilishi wa CCJ

Kwa kuwa team nzima ya CDM, imeshajulikana kuwa inatumika kama presha group na horse,s mouth ya mafisadi wa ndani na nje ya CCM, wala sishangai kauli ya Mpendazoe.

ChiefmTz

Mbona hueleweki my friend!

Hiyo nyekundu ina-raise a lot of un-answered questions! Yaani Chama cha upinzani makini kama CDM KINACHOPINGA UFISADI KWA NGUVU ZOTE kitumiwe tena na mafisadi wa CCM kweli???Unataka kusema hata JK naye anatumiwa na CDM???CDM kwa sasa ndicho chama tarajiwa kuchukua uongozi wa nji hii.Full stop! Seems that you don't what you're talking. You may wish to review your statements before you spat your rubbish.

No body will be convinced by your garbages!
 
Kwa hiyo unachotuambia ni nini? Fine alikuwa mwanzilishi wa CCJ then what. Kwa sababu hata yeye alishiriki akiwa bado yuko CCM, je huo siyo unafiki. Kwa nini hakubaki ndani ya CCJ ili aijenge na kuifanya iwe maarufu badala ya kuhamia CDM? Hivi vyama ni kama mitumbwi ya kukuvusha ng'ambo kwa usalama. Lakini lililo la msingi ni kwamba yeye Nape yuko CCM na anatetea sera au misimamo ya chama chake , kama ambavyo na yeye Mpendazoe ana haki ya kutetea sera na misimamo ya Chadema.

Hii siyo contest ya loyalty kwa chama hiki au kile, na ndiyo maana leo tunaona mwanasiasa huyu yuko kule na kesho yuko huku. Hata hiyo loyalty hupimwa wakati ukiwa ndani ya hicho chama na siyo baada ya kuondoka. Je Mpendazoe anataka kutuambia kwamba alipokuwa CCM kwa miaka yote hii hakuwa na loyalty na kwamba jicho lake lilikuwa kwenye upinzani? Naweza kuelewa frustrations za Mpendazoe hasa baada ya vigogo wenzanke kumchuuza ahame na wenzake watamfuata halafu wakamtosa lakini in politics kupima upepo huwa imo. Nani alijua leo hii Ntagazwa angekuwa huko aliko au Dr. Slaa huyu?

Katika siasa haya yote hutokea na yanapotokea mtu hutakiwa kila la heri kule aendako na akishindwa na kurudi hasutwi. Waone Makongoro Nyerere, Wasira, Nsazugwanko na hao akina Mpendazoe, Shibuda, Kahigi, Slaa, Ntagazwa na wengine wengi.


Mkuu ukiangalia historia ya Ntagazwa na Slaa kuingia Chadema ni tofauti sana na imenyooka na hawakurudi nyuma . Mpendazoe amehamia Chadema baada ya CCJ kunyimwa usajili wa kudumu kama ulikuwa hujui ujue sasa ndiyo maana akahama kwa kuwa hapakuwa na njia nyingine zaidi . CCJ ilisha pigwa stop yeye ulitaka abakie anafanya nini ?
 
Ndungu Nape, Kada machachari wa CCM,
Kwanza napenda kukupongeza kwa kupewa nafasi kubwa sana katika Chama Cha Mapinduzi. Mimi binafsi naamini kwamba jukumu ulilopewa ni kubwa sana kwa kulinganisha na umri na uzoefu wako. Kwa hiyo, nakushauri

(1) kutafuta ushauri mkubwa na kushirikiana kwa ukaribu sana na viongozi wasistafu na wale wenye uzoefu mkubwa na Chama..
Unaongelea wenye uzoefu wa kuwa Mafisadi au?
 
Maana Viongozi wengi wastaafu kila mmojawao amekuja kuonekana hajaleta mchango wowote kwa watanzania ukimtoa Nyereree.....wametuachia umaskini na ufukara kupindukia
 
Huwezi kupigana na MAFISADI/CCM halafu wakati huo huo unapigana na upinzani / CHADEMA.

Either ungana na MAFISADI upigane na CHADEMA, au ungana na CHADEMA upigane na UFISADI/CCM....

Huwezi kufanya vyote kwa pamoja, kumbuka upo CCM na sio CCJ (hehehe, just kidding).

Lakini seriously, chagua upande watu tujue moja.
 
Bado dogo ana kale ka - mentality kuwa ukiwa CCM unakuwa kila kitu (kuna picha nimeona humu ndani akigawa kanga inadhalilisha wale waliokuwa wamenyoosha mikono kama wanaomba).
Kwa sababu yeye anafikiri bado watanzania ni wakufirishwa ndo maana anaongea utumbo kila apatapo jukwaa.
Taratibu kastuka kwamba anapiga ngumi ukuta, anaanza kuumia mwenyewe.
 
Ushauri wa Lwaitama kwa Nape huu hapa

Mimi nadhani ndugu zangu wanahabari tunasaidia kupindisha hoja juu ya dhana ya ufisadi...Kuwa na mshahara mkubwa au kuwa na kipato kikubwa ulichopata kwa makubaliano na waajiri wako au kwa juhudi zako halali au za ndugu zako si ufisadi...Kutembelea gari la kifahari ulilopewa au kuazimwa au kununua kwa kipato halali chako au ndugu yako... ilo pekee alikufanyanyi mtu kuwa fisadi...Ufisadi, kwa maana yenye mashiko kisiasa, ni kushiriki kwenye vitendo vya kupata kipato cha siri kama malipo kwa kutumia cheo chako serikalini au katika chama tawala kufanikisha malengo yakujitajirisha kinyume cha sheria ya mtu au kakundi ka watu..Sasa ndugu yangu Nape kusema eti Dr. Slaa naye ni fisadi maana yake ni nini kimantiki? Kama Dr. Slaa ni fisadi basi kwa vile tu Chadema wamempa mshahara mkubwa kwa cheo chake cha ukatibu wa chama taifa ( ambayo si sawa na kuwa mbunge wa jimbo moja!!!!) sasa CCM wanajivua gamba kwa nini yalabi? Kama hiyo ndiyo dhana ya ufisadi ya ndugu yangu Nape basi haina maana kusambabisha uwezekano wa mifarakano ndani ya CCM kwa kutaka mafisadi wake wajiuzuru....Wanyime tu mishahara mikubwa!!!!!Eti?!!!..

Maana sasa kumbe ufisadi ni kupokea milioni 7 au hata 10 kwa kazi ya chama chako cha kisiasa kitaifa eti vile uliwai kusema wabunge wajimbo moja la watu wasiozidi milioni moja wasipate mshahara "mkubwa" wa milioni 7????!!! Hii inamantiki kweli??!!! Kashfa ya EPA, rada, Richmond...makashfa yenye harufu ya rushwa kubwa kubwa ya watu wenye madaraka makubwa makubwa serikalini, sasa yanalinganishwa na eti Dr. Slaa kulipwa mshahara wa milioni 7 au hata 10 kwa kazi ya ukatibu wa chama kitaifa chenye Wabunge na Madiwani na wafuasi kibao nchi nzima????!!!...Kweli kabisa hiyo ndiyo dhana ya ufisadi ya ndugu yangu Nape???

Huyu ndiye Nape anayetaka mimi na wewe tumwamini kuwa anakisaidia chama cha wakulima na wafanyakazi cha CCM kijivue gamba??? Gamba la nini kama si matajiri wanaoajiri mamia ya wafanyakazi na hivyo ni wanyonyaji lakini wameteka chama cha wakulima na wafanyakazi badal ya kuanzisha chama chao cha liberal democratic union au republican??? Gamba la nini kama si wafanya biashara wakubwa wakubwa wenye kutuhumiwa ufisadi kama ule wa EPA, Richmondi na Rada??? ...Kumbe ndugu yangu Nape tafsiri yake ya ufisadi ni kule kuwa na mshara wa milioni 7 au hata 10...Ina maana Maximo aliye kuwa kocha wa TFF na Gavana wa Benki Kuu ni fisadi vile waanapokea/walipokea mshahara mkubwa tulio wapangia sie? Kweli ndugu huyu Nape anataka tumwamini kuwa ni mpambanaji dhidi ya ufisadi? Kwa nini tusiamini kuwa lengo la uteuzi wake ni kupotosha umma juu ya dhana mzima ya ufisadi ili baadaye kusiwepo hata mmoja hatayeondoka CCM kwa kutajwa kuwa fisadi??? Yaani ufisadi ndani ya CCM utaondoka kwa kuzunguka nchi nzima tukishutumu ufisadi wa Dr. Slaa wa Chadema??!!!Maana sasa CCM itakachoitaji kufanya ni kuchapisha nakala za malipo ya mishahara ya wote wanaotuhumiwa kuwa mafisadi, eti? Hapo kweli sasa mafisadi watabaki akina Dr. Slaa na Gavana wa Benki Kuu, na Mkurugenzi Mkuu wa TRA, siyo?Tuache utani bwana!!!!Nape? Unatukatisha tamaa sisi CCM wafu!!! Tulidhani kumekucha kumbe bado giza totoro?!!
Wakatabahu,
Mwalimu Lwaitama
 
KILA NINAPOKUMBUKA ENZI ZILE ZA SHULE YA MSINGI, NAKUMBUKA WIMBO MZURI SANA, " Tazama ramani utaona nchi nzurii... yenye mito na mabonde mengii ya nafakaa.."nilifanya juhudi za kuutafuta wimbo huu katika maktaba za TBC, bahati nzuri niliupata nikanunua ile cassete, baadaye nikagundua ni (Marehemu) mzee Moses Mnauye, baba mzazi wa Nape, ndiye mtunzi na mwimbaji wa wimbo huu!!!!!!!! nikiusikia wimbo huu mimi huwa natoa machozi, ila KWA NINI NAPE HANA HATA CHEMBE YA HEKIMA? mrithi wa moses hakupaswa kuwa hivyo!!!!!!!! nape jipange sana bado una safari ndefu sana ndugu, nisikuchukie kwa uccm wako ila nikuchukie kwa upeo wako mfupi.

"KILA CHIPUKIZI HUCHIPUKA NA KUKUA KWA UFANANO WA SHINA LAKE"
 
Nape Nnauye anaendeleza ngonjera zake. Anadai uamuzi dhidi ya mafisadi upo palepale, hautabadilishwa kwa kelele za magazeti wala maandamano bali kupitia vikao ndipo wanapoweza kutengua uamuzi huo.
Akizungumza na Sauti ta America Nape amesema ni vizuri watuhumiwa hao wakaondoka wenyewe badala ya kusubiri kuondolewa kwa aibu.

Maoni yangu: Nape amechanganyikiwa. Sidhani kama bado kuna wazo la kumfukuza mtu yeyote ndani ya CCM. Hii ni kwa sabau yeye mwenyewe ni gamba tena gamba gumu, sio mwanachama mwaminifu kwa chama chake. Sio msafi kiasi cha kuwanyoshea kidole wenzake. Mengi yamejadiliwa sana hapa lakini kwa kuwa yeye mwenyewe anendelea na ngonjera zake hatuna budi kumpuuza
 
To hell with nepi! Anatafuta jinsi ya ku-cover his naked back but with no avail!
 
Kwani ni maandamano gani yamefanywa kupinga harakati za kuwaondoa mafisadi???? Huyu jamaa mzima kweli au ameanza kulewa madaraka
 
Nape Nnauye anaendeleza ngonjera zake. Anadai uamuzi dhidi ya mafisadi upo palepale, hautabadilishwa kwa kelele za magazeti wala maandamano bali kupitia vikao ndipo wanapoweza kutengua uamuzi huo.
Akizungumza na Sauti ta America Nape amesema ni vizuri watuhumiwa hao wakaondoka wenyewe badala ya kusubiri kuondolewa kwa aibu.

Maoni yangu: Nape amechanganyikiwa. Sidhani kama bado kuna wazo la kumfukuza mtu yeyote ndani ya CCM. Hii ni kwa sabau yeye mwenyewe ni gamba tena gamba gumu, sio mwanachama mwaminifu kwa chama chake. Sio msafi kiasi cha kuwanyoshea kidole wenzake. Mengi yamejadiliwa sana hapa lakini kwa kuwa yeye mwenyewe anendelea na ngonjera zake hatuna budi kumpuuza

Nimejaribu kumwelewa Nape nimeshindwa, maneno tuuuuu, vitisho tuuuu, vitendo hakuna!
 
Nape amesha mjibu Mpendazoe au bado analia lia ? Mpendazoe kasema jambo Nape anatakiwa kumjibu tujue anako simamia ni wapi
 
Kwakweli nape sasa anaona ugumu wa hizi kazi za siasa. Hivi nape bado yuko ktk probation au fully emloyed?
 
Nape Nnauye anaendeleza ngonjera zake. Anadai uamuzi dhidi ya mafisadi upo palepale, hautabadilishwa kwa kelele za magazeti wala maandamano bali kupitia vikao ndipo wanapoweza kutengua uamuzi huo.
Akizungumza na Sauti ta America Nape amesema ni vizuri watuhumiwa hao wakaondoka wenyewe badala ya kusubiri kuondolewa kwa aibu.

Maoni yangu: Nape amechanganyikiwa. Sidhani kama bado kuna wazo la kumfukuza mtu yeyote ndani ya CCM. Hii ni kwa sabau yeye mwenyewe ni gamba tena gamba gumu, sio mwanachama mwaminifu kwa chama chake. Sio msafi kiasi cha kuwanyoshea kidole wenzake. Mengi yamejadiliwa sana hapa lakini kwa kuwa yeye mwenyewe anendelea na ngonjera zake hatuna budi kumpuuza

Hivi kaka utaendelea kutumika mpaka lini? kwa malipo gani haya yanayokufanya ukubali kuonekana kichekesho hivi? Jisikie aibu kidogo, wewe mtu mzima! Au nyie ndo mko lile kundi la Marando na Komu ambao wanadai kwamba Nape amekula hela za EPA halafu hawajaweka chochote hadharani. Maisha ya Marando yamekuwa yanaendeshwa na mafisadi, ndo maana walimkodia ndege kwenda kuchafua watu Tabora! Nape hawezi kutishwa na makelele ya watalii!
 
Nape amesha mjibu Mpendazoe au bado analia lia ? Mpendazoe kasema jambo Nape anatakiwa kumjibu tujue anako simamia ni wapi

Mtu mwenye akili yake timamu hawezi kupoteza muda kujibu utumbo. Kama yeye bado ana bifu la kuchuuzwa akalalamike na mkewe huko!
 
Back
Top Bottom