CCM maji ya shingo leo hii hata adui yao mkuu Mtikila akitangaza kujiunga CCM atapokelewa kwa shangwe kubwa.Wako tayari kwa lolote,wanadhani ya kua wanajinusuru kume wanajitosa'Huyu Nnape alikuwa anatoa siri za Chama cha Magamba (CCM), kwenda kwenye CCJ, sasa hivi anadai kwamba anakitetea CCM, si unafiki huo wandugu? Mimi namshauri Nnape aachie watu wengine majukwa, akafanye kazi ya u-DC, nafikiri hiyo ataifanya vizuri zaidi kuliko kujaribu kuvuruga hoja za msingi dhidi ya chama chake!
Maneno mazito haya yaani ilikuwa afanye kazi ya kukigawa bila mwenyewe kujijua kama alivyokuwa Makamba au afanye kazi angali anajua anafanya nini kweli haya ni mapya kwangu.Hata mimi nimeipenda mkuu, Ukiangalia hii tthread nyuma utaona niligusia hiki kitu na sikujua kuwa mpendazoe ameshefyatuka. Nape ni mtu asiye makini kabisa kwa sababu ameacha fingerprint kila sehemu. Asingekuja kwa kasi CDM wasingemaliza kwani alikuwa afanye kazi moj akubwa sana kwa CDM kwa kutengeneza makundi CCM. lakini siasa ndiyo ilivyo hili limekuja pre mature sana na ndiyo maana hawataki kumaliza kila kitu. Amini usiamini CDM wana details nyingi sana na zingine alileta huyo huyo nape. Nape kama sio papala na urimbukeni wake angefanya kazi nzuri sana kwa chadema, kazi yao ingekuwa ni ku pick prey tu na kuioka. Any way inabidi ipatikane strategy ya kumrudisha kwenye line yake ya mwanzo. All in all kisiasa amekwisha kabisa ila ni kumrudisha kiaina tu. si ajabu tukaanza kumtetea hapa kama akionekana kama anaweza kuendeleza kazi lakini future yake kwishney
Tehe tehe tehe tehe..Ndugu yangu inaonekana umekereheka kweli kuhusu Mpendazoe kumtaja Nape kama mmoja wa waanzilishi wa CCJ...Haha haha haha haha....Bila shaka Mpendazoe alitaka kuuelewesha UMMA ili ujue Nape ni nani na ni ukweli usiopingika kuwa ndo alikuwa mmoja wa watu waliokuwa wanatupa taarifa za nini kinaendelea ndani ya Serikali...Bado wapo wengine na kama alivyosema Mpendazoe tutawataja wakati utakapofika...CCM imejaa viongozi wanafki...Ambao wanajifanya CCM kumbe hamna lolote....Tehe tehe tehe...Asante sana Mpendazoe....
![]()
VITA vya maneno kati ya Chadema na CCM jana imechukua sura baada ya Fred Mpendazo kumtaja Katibu Mwenezi na Itikati wa CCM, Nape Mnauye kwa miongoni mwa vigogo sita walianzisha Chama cha Jamii (CCJ) .
Mpendazoe alitoboa siri hiyojana alipokuwa akituhubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kijiji cha Mbamba Bay kilichopo katika wilaya mpya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Mpendazoe alijitoa CCM Machi 30, mwaka jana akiwa Mbunge wa Kishapu na kujiunga na CCJ Aprili 16, mwaka huo kabla ya kuhamia Chadema, baada ya CCJ kukosa sifa na kufutwa na Msajili wa Vyama vya Siasa.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika mji wa Mbamba bay, mkoani Rvuma jana, Mpendazoe alisema ameamua kuliambia taifa ukweli kuhusu Nape, ili umma uepuke kudanganywa na propaganda za kijana huyo.
Kelele zote anazopiga Nape kuitetea CCM ni za kinafiki kwani aliwahi kukigeuka chama hicho na kushiriki katika mipango yote ya kuanzisha CCJ.
Hata hivyo, Nape alipoulizwa na gazeti hili jana kuhusiana madai hayo ya Mpendazoe, hakukataa wala kukubali kushiriki kuanzishwa CCJ, badala yake alisema, "Cha msingi waeleze (Chadema) CCJ ilikufaje, wasiseme ilizaliwaje, maana kuzaliwa ni sherehe na kufa ni kilio.
Nape ambaye hakusema lolote kama kombora la Mpendazoe ni la kweli aliwageuzia kibao Chadema akisema, "Pamoja na hayo yote, waache (Chadema) kubaka demokrasia."
Alifafanua akisema "Watanzania walipiga kura kuichagua CCM iwaongoze kwa miaka mitano ijayo, sasa wanaposema tutaandamana nchi nzima ili serikali iondoke kabla ya muda huo, huku ni kubaka demokrasia na ni uhaini."
Mpendazoe alisisitiza kuwa Nape alishiriki katika kuandaa na kuandika katiba ma miiko ya uongozi ya CCJ, kutafuta fedha za kukuza chama na jengo la kuweka ofisi za chama hicho. Alisema: Huyo Nape anayepiga kelele za kuitetea CCM ni mnafiki mkubwa pengine kuliko wanafiki wote hivi sasa. Mimi na yeye pamoja na wana-CCM wengine wanne, ndio tulioamua kuanzisha CCJ.
Nape ndiye aliyepewa jukumu la kutafuta nakala za katiba za vyama tawala vya nchini za Afrika, ili kupata katiba nzuri ya itakayoigwa katika kuandika katiba CCJ. Alisema Nape alilitekeleza vizuri jukumu hilo na kufanikiwa kuipata katiba ya chama tawala cha Afrika Kusini cha ANC, ambacho ndiyo kilitumika kwa kiasi kikubwa kuandaa katiba ya CCJ.
Alisema yeye, Nape na vigogo wengine aliosema atawataja muda ukifika walifanya vikao vyote vya siri hadi wakaanzisha chama hicho cha CCJ.
Tulifungua mtandao maalum wa kuwasiliana kwa internet, ambao baadaye wenzangu waliufuta baada ya kubadili mawazo dakika za mwisho. Iilipotulazimu kukutana mimi na Nape tulipendelea kukutana katika eneo la vinywaji pale Mlimani City, jijini Dar es Salaam. Alisema walifanya hivyo ili wasitiliwe shaka na maafisa usalama wa taifa waliopewa kazi ya kupeleleza wanaCCM waliohisiwa kutaka kuanzisha chama kipya.
Nape alibadili mawazo ya kutaka kuihama CCM baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi, kwa kuwa alikuwa na uchu wa madaraka , aliongeza. Alisema Nape aliisaidia CCJ kwa kukipa siri nyingi ikiwemo mambo yaliyokuwa yakijadiliwa kwenye mikutano ya Halmashauri Kuu ya CCM (Nec)n a hata vikao vilivyokuwa vikifanyika katika ofisi ndogo ya CCM iliyopo Lumumba.
Nape pia alitupa siri kwamba baadhi ya walioanzisha CCJ walikuwa wanakaribia kufukuzwa kwani katika mkutano wa NEC, majina ya baadhi yao yalitajwa na kujadilia kwenye kikao hicho.'
Source: Mwananchi.
My Take:
Kama mwenyewe Nape hakanushi basi atakuwa ni hatari kwa chama chake kauli yake ya 'PAMOJA NA HAYO' inadhihilisha amebanwa kwenye kona.
Sasa ndiyo wakati wa kupata mengi wengine tunajumlisha na kutoa siku ya siku tutakuja na jibu sahihi.
Sitaki kweli kuzungumzia.... picha iseme yenyewe..
![]()
Unaweza kufafanua umafia wa CCM ukoje huku wewe ungali ndani yake.Nyote ni wenye uchu na madaraka ndio maana hamjijui kisiasa mpo wapi; Mpendazoe hanasababu ya kuelewesha umma sasa hivi, kama Mpendazoe na wewe lengo lenu ili ni kutetea maslahi ya watanzania msingekuwa mnahangaika kuhama vyama kama machangudoa wanaotafuta wanaume kila kona, hamkupata nafasi ndani ya CCM naamini lengo lenu ilikuwa ni kumtumia Nape ili mfanikiwe malengo yenu kisiasa, vinginevyo mtanzania gani wa kawaida angemjua Mpendazoe? Kutokana na uchu wenu wa madaraka kisiasa mliingia mkenge huyo Nape hakuwa mshiriki wenu alikuwa hapo kuwa zuga tu CCM iliwateka kiakili; mmesahau CCM inajiendesha kimafia?Kumbuka CCM inatumia wanaccm kuua upinzani, mlichokuwa mnatafuta ni ruzuku, nenda mkawadanganye Mbamba Bay hapa Dar hamuwezi kusema upuuzi huo.
Chama
Gongo la Mboto DSM.
kama amelalamikia facebook,si mngekwenda ku comment hukohuko facebook?kwanini na nyie mmeyaleta hapa jf?
Unaweza kufafanua umafia wa CCM ukoje huku wewe ungali ndani yake.
Naona ES kajitahidi sana sana kwa kutumia hoja za nguvu!!!!! lakini it so happens kwamba nguvu ya hoja hushinda eventually. Hata aseme nini -- Nape ni msaliti tu kwa CCm -- na kwa vile chama hicho hakina direction, dira, wala credibility, ataachwa tu hivi hivi.
katika ujasiri, huwezi kumlinganisha Nape na Mpendazoe, they are a world apart! Mpendazoe wazi wazi alikihama CCM, akingia CCJ, halafu openly tena akakihama CCJ na kuingia CDM. SO OPENLY. Huyu Nape alijificha ficha hadi amekuja kugunduliwa! Aibu kubwa hii!
Many people including CCM supporters are really tired on how the party is trudging along.
Nape akae kimya tu, yakianikwa hapa na vi note vyake pamoja na mfadhili wake (IPP) basi ataumbuka sana. Kaingizwa mtegeno na obsession yake ya kutaka ku revenge kwa EL. Kila siku wanaswahili wanasema "hasira hasira" au wanjanja kabisa wanasema "hasira ni za Bwana"
Kumbuka kuwa mafisadi huwa wanakodi mpaka ma consultant kuwa kuwatengenezea njia. usije shangaa kuona kuwa huu ulikuwa ni mpango mzima. Kwa sababu doc kutoka usalama wa taifa ilishawaeleza wote hata nape kuwa ni mwanzilishi wa CCJ. Inakuwaje sasa anapewa vyeo kama sio process ya kuwatoa nje wote sita na wakawa hawana pa kukimbilia.
Halafu inaonekana nape IQ ni kama ya @NYC kwa sababu kama alitaka kucheza siasa huwezi kwenda kichwa kichwa namna hiyo. Lazima uwe mtu wa kutest hata meseji zako kabla hujaingia kichwa kichwa na hapa jf ni free area ya kufanya hivyo. Sasa hawa wanajifanya kujua sana na siasa hawaziwezi. Angalia mchezo wa CDM na kutaja tinga tinga ilikuwa ni move kali sana sasa yeye na mke wake fyatu. Bado hao vigogo wanne waliobaki + na huyo mfadhili wao.
Duniani watu wa kuchukiwa ni ndumila kuwili, kuna afadhali hao mafisadi kuliko hawa kwani fisadi ukimkuta kwenye kumi na nane humwachi!
Cr@P at its's best...mzee inaonekana yale mafrustartion ya kura za maoni bdo hayajaisha.....siku hizi unamwaga upupu tu
Usitafute sympathy kwa watu sijawahi kusema huna elimu hata siku moja usijihisi ila group ulilojiunga nalo si la weledi kama la zamani kwa hiyo watu wakikujibu kama wanavyojibu hao usilalamike kwa kuwa umelichagua mwenyewe. Mfano tu hapa topic ni Nape mwanzilishi wa CCJ lakini utetezi wako unaleta data zisizohusiana na topic yenyewe maana yake ni nini umezidiwa hoja au huna hoja ni sawa na wanaopindisha hoja za thread huo ni udhaifu.