Nape na Kipindi Maalum - CCM Kujivua Gamba

Nape na Kipindi Maalum - CCM Kujivua Gamba

Ccm ni wasanii sana. Bahati nzuri watanzania wa leo si wa jana wamshamka. Wanajua ukweli.
 
- Nape is right on the track, mafisadi wanajua kwamba wamepigwa bao ndio maana hata magazeti yao siku hizi yamejaa vichekesho, kila lenye mwanzo huwa lina mwisho, mwisho wao umefika sasa.

- Anaposema Rais wa Jamhuri kwamba kila analosema Nape ni lake, the next ni FULL STOP!



William @ NYC, USA.

William sijakusoma bado; ina maana hata alipo badilisha tone bado anawakilisha kubadilika kwa command iliyotolewa na rais kama kweli hii bado ina hold water kuwa kauli ya rais ni comand?
 
Siku naanzisha thread hii niliamini moja kwa moja CCM ya Mh. Kikwete haikuwa na nia ya dhati ya kufanya mabadiliko yoyote ya maana ndani yake. Kauli za Katibu Mukama zinadhihirisha hilo na kwa maana nyingine Nape naye ni pumba nyingine katika chama. Utazungumziaje kutoa siku 90 bila Mukama kujua?
Pengine kwa kuwa wana mtandao ni mabingwa wa kuchezea akili za watanzania na kujipatia madaraka, wanajaribu kwa maksudi kuwahadaa wananchi ili wapate tena 2015. Ikitokea hivyo, sipati picha utajiri wa RA na EL na ule "silent' wa JK utakua kwa kiwango gani kufikia 2020. These people are killing us so fast that no one of us is comprehending.
JK anaonekana kuwa mlipa fadhila mzuri sana kwa wafadhili wake kuliko marais wengi duniani. Amejitolea kwa lolote lakini hawezi kuwasaliti RA, EL na wengine maana walimfaa sana alipokuwa na kiu kali ya title na show off za mercedes benz na bmw zenye nembo ya taifa.
Nisiseme mengi. CCM hawavui gamba wala nini na kama hamuamini subirini muone mwisho wa kauli za Nape kama si aibu tupu!

Aibu hii haimhusu Nape kabisaaaa! Wapo ambao aibu hii itawapata peupe peee wajiulize ilikuaje hata tukajikuta kwenye aibu kubwa kama hii! Nape did some thing profound at a very calculated and correct timing. With or without knowing so far so good CCM haiwezi kukana tena si chama cha mafisadi hata waje na ushahidi wa malaika maana mahakama ya peoples power imeshawekewa seal kuwa hukumu ilikuwa sahihi kabisa wakati ilipoamuliwa hapo 2007. By the way nimepata ushahidi mwingine yule adui yangu mkubwa ufisadi nimemvunjavunja na kumpiga cha kwenye nerve system hata alipojaribu kupambana nami; I am awaiting for a day when am to sing a great halleluya hosiana the Lord who is my strength is my battle banner!
 
Baada ya Lowassa, Chenge na Rostam kutoa vitisho, Kikwete anywea!

~@@~~@@~~@@~~@@~~@@~~@@~~@@~~@@~~@@~~@@~~@@~


Mukama; CCM haina orodha ya mafisadi



*Yakanusha kuwapa siku 90

Na Mwandishi Wetu

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kwamba japokuwa kuna tuhuma za ufisadi dhidi ya baadhi ya makada na viongozi wake, bado hakina majina rasmi ya watuhumiwa hao, kama inavyodaiwa na vyombo vya habari nchini huku kikikanusha kwamba kilitoa siku 90 kuwatimua wanachama hao.

Kauli hiyo ilitolewa Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa CCM, Bw. Wilson Mukama alipokutana na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari kwa lengo la kufahamiana na kutambulisha sekretarieti mpya ya chama hicho.

Hatua hii inazua maswali mengi miongoni mwa umma na wanachama wa CCM , ambao bado wamegubikwa na utata juu ya nani hasa analengwa katika operesheni hiyo maalumu inayojulikana kama ‘kujivua gamba' ambayo wachambuzi wanasema huenda ikawa ngumu kwa CCM katika utekelezaji wake.

Tayari vyombo vya habari nchini vimekuwa vikiwataja makada watatu wa CCM kuwaoanisha na hatua ya kuvuliwa nydhifa zao ndani ya chama akiwemo Waziri Mkuu aliyejiuzulu Bw. Edward Lowassa, Mwanasheria mkuu mstaafu, Bw. Andrew Chenge na Mbunge wa Igunga, Bw. Rostam Aziz .

Hata hivyo, Bw. Mukama aliyeonekana kukwepa kujibu moja kwa moja maswali ya waandishi hao alibainisha kuwa orodha ya watu 11 wanaodaiwa kuwa mafisadi iliyotolewa na Katibu Mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa sio ya CCM .

"CCM haina orodha ya mafisadi. Kilichopo ni kwamba tunarajia utekelezaji wa hotuba ya mwenyekiti wetu pamoja na maazimio ya Halmashauri Kuu ya chama iliyokaa katika kikao chake mwezi uliopita," alisema Mkama.

Pamoja na hayo Katibu Mkuu huyo alisistiza kuwa CCM imepania ‘kuwatema' wanachama wote wanaohusishwa kwa namna yoyote katika tuhuma za ufisadi kwani uamuzi huo ni moja ya maazimio ya NEC lililopitishwa kwa kauli moja katika kikao hicho.

Akisoma Azimio namba 15 la NEC, alisema NEC ilisisitiza kuwa chama kitaendelea na mapendekezo yake dhidi ya ufisadi aidha viongozi wote waliotuhumiwa, watafakari, wapime na wachukue hatua.

Alisema mbali ya Azimio hilo, hotuba ya Mwenyekiti wa chama hicho Rais Kikwete ilisisitiza kuwataka wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi watafakari na kuchukua hatua.

"Wasipofanya hivyo, basi tunatarajia kwamba chama kitachukua hatua kupitia Tume yake ya Maadili ambayo imeongezewa nguvu na kwa kuongezewa idadi ya wajumbe," alisema.

Hatua hii inakuja ikiwa imebaki mwaka mmoja kwa chama hicho kufanya uchaguzi wake mkuu na miaka minne kabla ya uchaguzi mkuu wa rais, na wabunge na madiwani.

Katika mkutano huo ambao ulitawaliwa na maswali mazito ya waandishi, Bw. Mukama alikanusha pia hatua ya CCM kudaiwa kuwapa siku 90 watuhumiwa ufisadi na bila kufanya hivyo watatimuliwa.

" Haya yakusema siku 90 sijui yametoka wapi, kwa utaratibu NEC inakutana mara tatu kwa mwaka hapo pana miezi minne, huenda mtu alidhani NEC inakutana baada ya miezi mitatu na kudai tumeweka muda huo," alisema.

Alisema mabadiliko yaliyofanyika kwenye Kamati Kuu ya chama na sekretarieti ni hatua ya kawaida ya kitaasisi na kinachotafsiriwa na wananchi ni tofauti kabisa na makusudi ya chama hicho.

"Tunaamini kwamba mageuzi ya kisiasa yanakua kwa kasi sana hapa Tanzania. Sisi kama CCM tunajiweka sawa kukabiliana na mabadiliko haya, kwa kuanzia ngazi ya juu kuelekea chini," alisema Bw. Mukama.

Bw. Mukama alisema kwamba ufumbuzi wa matatizo ya kiuongozi ya CCM ya umeanzia katika ngazi za juu na inatarajiwa kuendelea katika ngazi za chini ili kurudisha imani kwa wananchi
 
Nape, naona aliyekuteua majuzi kwenye sekretariat CCM ili kuwa Meneja Masoko kukinadi chama hicho kwa hali yake ya hivi sasa, japo utakua unamuona kama vile kakupenda vile, ukweli wa mambo ni kwamba kaamua kukuua kabisa kisiasa mwenzetu na wala hukuliona hilo.
 
"HATA MALAIKA AKIINGIA NDANI YA CCM HAWEZI KUPAMBANA NA UFISADI" BY DR. SLAA. Hii inamaana kwamba GAMBA wanalo, na hata wakivua sumu inaongeza.
 
  • Thanks
Reactions: Ame
mi mwenyewe nimetokea huko,ni kweli unayosema,maneno ya mfa maji tu
 
Wana JF

Sisi tumemsikia Nape akisema kwa majina kuwa mapacha watatu (EL, RA na EC) lazima wajiondoe na vyombo vya habari vikanuu Makongoro akipigilia msumari kwa kuwataja hawa mapacha. Dalili zinaonyesha kuwa Mukama anataka kubadili hoja kuwa hakukuwa na hayo maamuzi wala hawana list ya mafisadi. Kama ikifikia hivyo hoja ikabadilishwa na wajamaa kutopewa barua wala kutofukuzwa chama nitamini kuwa ni kweli CCM inawafanya Watanzania ni mabwege je ni kweli watanzania ni mabwege?
 
Kwani wewe ni mwanachama?Vinginevyo imarisha chama chako ili kije kukubalika zaidi 2015.Ya Ngoswe...
 
Oya acheni majungu jamani hii ni nchi yetu wote sasa mtu anapotokea kujaribu kuchukua hatua asipondwe na kusemwa hyo kwa mimi naita wivu nyinyi mnasema ila hamchukui hatua, yeye ni ccm sasa aihame?

Me naona anafanya vzr kama kijana Ongera sana bora vijana wajae ccm sababu ccm ndo inaongoza nchi hvyo ule mpango wa wazee wetu kudanganywa na wajaja unapungua coz vijana ni wajanja kuliko wazee.

Nape hajafanya kitu kibaya mpaka 2mseme wenye makosa wapo kama hawapo tuache majungu hayasaidi.
 
Nape nape nape nape nape.

Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko ccm -magamba kuwatosa magamba wenzao
nape, chiligati, na mkulu siku ile walitoka kwa mbwembwe sasa wananywea wenyewe hivi hawakujua kwamba mapacha watatu ndio walioshikiria ccm na ndio wanoendesha serikali ya kimtandao?

Tofauti na chadema na Slaa hakuna mtu mwingine mwenye ubavu wa kumtosa chenge anajua madudu mengi ten years as ag. Tofauti na chadema na slaa dr wa ukweli hakuna mwingine anaweza kumtosa mzee wmenye mvi amekamata kila kona ya ccm watavua wapi waache wapi? Amekamata hadi spika -kila konaaaaaaa ni mjanja huyu isipokuwa kwa chadema tu na dr slaa ndio maana alisema ccm iangalie sana arusha, tofauti na chadema na dr slaa nani anaweza kumnyoshea roast ni gwiji la magamba anajua kila kila kona akiguswa tu anafungulia -nape ajifunze sasa ataanza kuchukua chake mapema na kuanza kuwapamba. Kifo cha ccm hicho mbele pachungu nyuma pachungu waende wapi???????

Let them dissolve the party.
 
Wanapotosha wao wenyewe CCM sio CDM. Nani kamtuma Nape Nnauye aseme ambacho hakikuazimiwa na NEC? Nani kamtuma Mukama ampinge mjumbe wake wa Sekretarieti Nnauye? Mtajichubua hadi damu na kuitazama CDM lakini mwisho wenu umefika, ha ha ha!

nani amfunge paka kengele!? Nakumbuka chiligati alipokuwa akiwasema mapacha3 RACHEL nlisikia diwani alimpinga kuwa naye ni fisadi,na leo kafutwa udiwani/uanachama. Sasa leo waanzeje kusema majangili yameyeyuka wakati tuliwasikia wenyewe?
 
Nape nia yako BINAFSI ni zuri ila kubadilisha MFUMO FISADI ndani ya hicho chama, hata kwa miaka 900 sawa na umri wa Brahamu nasema wewe peke yako tu hivyo hata siku moja huwezi!!!!!!!!!!!!

Huoni woote wanaanza kujificha mbele ya dhuluma dhidi ya Wa-Tanzania hivi hivi na kukutelekeza kama Osama alivyotelekezwa na wenzie kule Abbotrabad, Pakistan; yaani bado hustuki tuu?????????????

Nape nape nape nape nape.

Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko ccm -magamba kuwatosa magamba wenzao
nape, chiligati, na mkulu siku ile walitoka kwa mbwembwe sasa wananywea wenyewe hivi hawakujua kwamba mapacha watatu ndio walioshikiria ccm na ndio wanoendesha serikali ya kimtandao?

Tofauti na chadema na Slaa hakuna mtu mwingine mwenye ubavu wa kumtosa chenge anajua madudu mengi ten years as ag. Tofauti na chadema na slaa dr wa ukweli hakuna mwingine anaweza kumtosa mzee wmenye mvi amekamata kila kona ya ccm watavua wapi waache wapi? Amekamata hadi spika -kila konaaaaaaa ni mjanja huyu isipokuwa kwa chadema tu na dr slaa ndio maana alisema ccm iangalie sana arusha, tofauti na chadema na dr slaa nani anaweza kumnyoshea roast ni gwiji la magamba anajua kila kila kona akiguswa tu anafungulia -nape ajifunze sasa ataanza kuchukua chake mapema na kuanza kuwapamba. Kifo cha ccm hicho mbele pachungu nyuma pachungu waende wapi???????

Let them dissolve the party.
 
duu . . . . !
U kamoflegy unaendelea huko chama cha mafisad . . .
 
Waheshimiwa wanaJF,
Salaams!

UPDATE:
Katibu Mukama ameamua kuwa wazi. CCM hawana orodha ya mafisadi wala hawajatoa siku 90 kwa mtu. "Kwa ujumla hakuna mwana-CCM msafi kama Mapacha watatu" aaaah!...ha..ha..haaaaah! Guys, I told you CCM ni nyoka kweli. Ndiyo maana hata Mwenyekiti wao hakuwa na mfano wowote mwingine katika kuelezea wanachokusudia kuwaaminisha wadanganyika isipokuwa mageuzi ya mara kwa mara ya nyoka kwa kuvua magamba tena alisahau kusema mwenye sumu kali.

Kama huzijui aina za sumu ya CCM (Nyoka wa magamba) fuatilia kauli za kuwapo udini, ukabila, ukanda nk. hapa nchini wakikusudia kuua nguvu za vyama vya upinzani. Hawa jamaa wakizidiwa wapo tayari hata kuwatumia viongozi wajinga wajinga wa dini ili kuanzisha vurugu ambazo zitasaidia kuwalinda wao na mali zao. Lakini bado naamini tunayo nafasi ya kutetea nchi yetu iliyopoteza mwelekeo. May the Almighty God save us from these people.
Time will tell, and God willing these people will pay for this one day. And they will pay so dearly that no one will ever try to imitate what they have done to our country. (end of update)

Tuko ukurasa mmoja sir! Preach it so that it goes deep into their hearts!
 
Nape nape nape nape nape.

Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko ccm -magamba kuwatosa magamba wenzao
nape, chiligati, na mkulu siku ile walitoka kwa mbwembwe sasa wananywea wenyewe hivi hawakujua kwamba mapacha watatu ndio walioshikiria ccm na ndio wanoendesha serikali ya kimtandao?

Tofauti na chadema na Slaa hakuna mtu mwingine mwenye ubavu wa kumtosa chenge anajua madudu mengi ten years as ag. Tofauti na chadema na slaa dr wa ukweli hakuna mwingine anaweza kumtosa mzee wmenye mvi amekamata kila kona ya ccm watavua wapi waache wapi? Amekamata hadi spika -kila konaaaaaaa ni mjanja huyu isipokuwa kwa chadema tu na dr slaa ndio maana alisema ccm iangalie sana arusha, tofauti na chadema na dr slaa nani anaweza kumnyoshea roast ni gwiji la magamba anajua kila kila kona akiguswa tu anafungulia -nape ajifunze sasa ataanza kuchukua chake mapema na kuanza kuwapamba. Kifo cha ccm hicho mbele pachungu nyuma pachungu waende wapi???????

Let them dissolve the party.

CCM inaweza isi dissolve lakini mafisadi lazima yafie baharini, inaelekea wengi mnapigana bila kujua road map ya vita ni ipi. Sasa nyie sikilizeni wenye macho wawaeleze and keep this for record hakuna mtanzania ambaye hajafanya ufisadi ataingia kwenye hili kaburi la mafisadi kama hata penda kuwamo mwenyewe ama kwakuwa ndumila kuwili au mwenye kujipendekeza kwa manufaa ya tumbo.
 
- Nape is right on the track, mafisadi wanajua kwamba wamepigwa bao ndio maana hata magazeti yao siku hizi yamejaa vichekesho, kila lenye mwanzo huwa lina mwisho, mwisho wao umefika sasa.

- Anaposema Rais wa Jamhuri kwamba kila analosema Nape ni lake, the next ni FULL STOP!
William @ NYC, USA.

kwa kweli binafsi huwa napata shida sana kumuelewa huyu kaka, au kwa kuwa mi si mwanasiasa?
 
Back
Top Bottom