Nape na Kipindi Maalum - CCM Kujivua Gamba

Mafisadi waliokuwa ndani ya CCM na ukizingatia ndicho chama tawala hawa si maadui wa CCM peke, la ni maadui wa taifa zima maana wamekigeuza chama kinachotawala kuwa chao na kukiendesha chenyewe na serikali yake kifisadi na kusababisha machungu mengi sana katika maisha ya wengi humu Tanzania.

Nimesikiliza kwa Makini Mdahalo wa Chuo Kikuu juu ya Muswada wa Katiba, ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Mnauye alinena kuhusu umuhimu wa kupambana na hali ilivyo katika siasa za leo na umuhimu wa vijana kujiunga na mapambano haya, na leo amefafanua kinagaubaga jinsi wanachama wenye nia njema walivyokuwa na wakati mgumu katika kuleta mabadiliko ndani ya CCM. Kijana amekaa vizuri, anahitaji full support ya vijana wengine maana nina uhakika wazee hata waliobaki wako ambao hawako hepi na kasi ya kijana huyu na wenzake.

Huyu ndiye kijana aliyewahi kufukuzwa uanachama "kutoka duniani hadi mbinguni" na aliwahi kunenwa vibaya na viongozi wake kwa msimamo wake dhidi ya wanaolinda ufisadi na udhalimu ndani ya CCM.

Usikate tamaa, kaka tunakuona kama mkombozi katika chama, simamia mabadiliko, nafasi uliyonayo itumie vema kwa kasi hiyohiyo.

CHADEMA haya yanayotokea humo ndani mwenu... mi sisemi...
 
NAPE MNAUYE, JANUARY MAKAMBA NA WILSONI MUKAMA HEBU KAZUNGUKENI TENA MIKOANI NGWE YA PILI MKAWATANGAZIE WANANCHI KWA KAULI YA OPERESHENI CCM VUA GAMBA
HAPO AWALI ILIKUA NI MZAHA TUUU!!!!

Nauye na Mukama, hebu kaandikeni tena imprest ili mwende upya mzunguko wa pili mikoa yote kwenda kuwambia wananchi kwamba yale mliowambia hapo awali (Operesheni CCM kuvua Gamba RACHEL) kule kuvua gamba ndani ya siku 90 wala hamkuimanisha saaaaana vile kwani ilikua ni gia tu kwamba Sekretarieti Mpya CCM Mtoke Vipi vle, au sio???

Msisahau kuwafahamisha wananchi ukweli wa mambo kwamba lile Gamba la CCM iliokusanyika kwa zaidi ya miaka 50 sasa wala haichuniki hata kwa panga hivyo mmeamua wenyew magamba sugu wenye wakajitilie wenyewe sahihi barua kwenda kwa MAFISADI ambao kimsingi mnasingiziwa tu wala hawapo kwani ni siku nyingi walishahamia katika nchi nyingine iitwayo KUSADIKIKA hivyo hapa Tanzania hawapo tena.

Hebu fanyeni hima kidogo kabwa mambo hayajabumburuka zaidi.​
 
Ni swala la wakati tu, vijana wanasikiliza hoja na kuangalia upepo unakwendaje, siasa si ushabiki ni hoja zenye kuleta mvuto ndiyo mana matokeo uchaguzi hayafanani. kuwepo kwa CHADEMA ni changamoto nzuri kwa kuimarisha CCM, nadhani ndio wanaitumia hiyo nafasi sasa na naona wameanza vema.
 
Nilikuwa sijawahi kumsikiliza huyu mchonga Nape. Kumbe ni mbabaishaji kuliko hata Makamba. Anaonekana anasumbuliwa na makundi ya CCM kuliko hata Makamba.....
 
Wazee wa CCM, mumemuweka Nape, kilaza, ili aturubuni kizaz cha leo? Mmekoma, kwshney!
Nenden kaburini kwa mwalimu mumuombe awavue hlo gamba.
SIASA ZA MANENO HATUTAKI, TUMEWACHOKA, MIAKA 50 NCHI MASKINI, TWAHTAJI CHAMA KIPYA.. Labda CCM ifutwe kabsa, tena eti mapinduz, mapnduz gan mumeleta??
 
mh hao kina nape and the gang kelele zao si majukwaani na ktk media hatuwaamini kabisa! Tunasubiri hizo 90 days ndo tuseme otherwise is blah! Blah! Blah! As ussual lakini si umeona Mukama ashaanza kuneutralize issue we wait and see and we would decide if to congratulate them
 
Nape mbabaishaji sana nimeacha kuangalia game nimsikilize kumbe anaongea upuuzi uliojaa ubabaishaji tu. Kweli magamba yanaharibu akili za vijana wetu. Kumbe kijana hata uwe na akili gani ukishaingia kwenye chama cha magamba akili inapotea
 
  • Thanks
Reactions: Ame
Amefanya nini ambacho hakijawahi kufanywa na walio mtangulia? Je barua zimeshatoka? Je ameshawataja mafisadi? Je Ameshawaambia warudishe pesa zetu? Kama ni bra bra, sizadhani kama tunazihitaji
 
NAPE MNAUYE, JANUARY MAKAMBA NA WILSONI MUKAMA HEBU KAZUNGUKENI TENA MIKOANI NGWE YA PILI MKAWATANGAZIE WANANCHI KWA KAULI YA OPERESHENI CCM VUA GAMBA
HAPO AWALI ILIKUA NI MZAHA TUUU!!!!

Nauye na Mukama, hebu kaandikeni tena imprest ili mwende upya mzunguko wa pili mikoa yote kwenda kuwambia wananchi kwamba yale mliowambia hapo awali (Operesheni CCM kuvua Gamba RACHEL) kule kuvua gamba ndani ya siku 90 wala hamkuimanisha saaaaana vile kwani ilikua ni gia tu kwamba Sekretarieti Mpya CCM Mtoke Vipi vle, au sio???

Msisahau kuwafahamisha wananchi ukweli wa mambo kwamba lile Gamba la CCM iliokusanyika kwa zaidi ya miaka 50 sasa wala haichuniki hata kwa panga hivyo mmeamua wenyew magamba sugu wenye wakajitilie wenyewe sahihi barua kwenda kwa MAFISADI ambao kimsingi mnasingiziwa tu wala hawapo kwani ni siku nyingi walishahamia katika nchi nyingine iitwayo KUSADIKIKA hivyo hapa Tanzania hawapo tena.

Hebu fanyeni hima kidogo kabwa mambo hayajabumburuka zaidi.​
 
Nape, asante kwa kutuhakikishia kuwa tuliokuwa karibu tunakata tamaa tusikate tamaa. Katika kipindi cha CCM Kuvua gamba leo nimekusikiliza kwa makini na huu ndio uchambuzi wangu:

1. Safi sana kwa kukumbusha kuwa wale watakaochukia watu wengine juu ya yaliyoazimiwa si sahihi maana ni taratibu au kanuni au maadili yanayogomba dhidi ya vitendo vyao visivyokubalika na si suala au uamzi wa mtu fulani.

2. Nimesikitika kuwa uzito wa maelezo yako ya leo mbele ya luninga katika kipindi maalumu yamepungua uzito wake (diluted in terms of your tone & substance) ukilinganisha na siku ulipopewa dhamana ya Uenezi na katika vikao mbalimbali vilivyofuata mkitambulishwa huko Morogoro, Dar n.k . maana hukumungúnya maneno huko: Niseme wazi kuwa:-

a. Hakuna sababu mpaka leo hamtaki kuwataja waziwazi kwa majina wale walioambiwa kuchukuwa hatua za kutupisha kutokana na malamiko ya wananchi juu ya ufisadi. Haiingii hakilini utueleze maazimio ya kikao lakini usiseme yanamuhusu nani .
b. Umesema kuwa siku 90 hazitajwa katika maazimio na kwamba ni waandishi wa habari waliotafsiri hayo. Kumbuka kuwa watu wanarecord yanayosemwa na kiongozi wetu yeyote. Kama kuna mtu alitamka hayo kama yeye ni busara ungeomba radhi na kurekebisha kuwa sasa unaongea kwa niaba ya CCM na tusahau yote ambayo mtu aliongea kama yeye binafsi.

c. Unajua kabisa kuwa sualala Ufisadi ndilo limetupaka matope sana hadi kuleta mbiu ya kujivua magamba. Kwa nini umepata kigugumizi kueleza kama hata barua husika kwenda kwa wahusika zimeshatolewa au bado. Aidha kama mnasoma alama za nyakati hata kwa kufuatana na swali la aliyekuwa anakuinterview, tunaomba ujumbe ufike kunakohusika kuwa itakuwa kichekesho hao watu waachie ngazi tu za nafasi zao katika vikao vya juu vya chama na wakaendelea kuwa Wabunge. Maana umesema mwenyewe kuwa uongozi huo wanaupata kupitia CCM na hivyo, pasipo kujiumauma, waelezwe wajiuzuru Ubunge au nafasi yeyote Serikalini pia. Na Vyombo vyote vya kusimamia sheria na hata Takukuru wachukue nafasi zao kuwafikisha mbele ya sheria juu ya makosa yanayowakabili. Nape, huu ndio unatakiwa kuwa msisito wako popote unapookwenda kama kweli unataka imani na ushindi wa CCM urejee. Wengi tuna imani nawe pamoja na Viongozi wengine wa sasa wa CCM, lakini ebu mseme kile mnachotaka kusema bila kujiuma wala kuhofu mtu maana CCM ni ya WanaCCM na Tanzania ni ya Watanzania wote.
 
Wewe kitu kimoja haukijuhi na siasa...huyo ni mpiga debe na hayo magamba yenu ni zaidi ya Nape kwa kila sehemu,siasa ni pesa kama hautaki endelea kufatilia,alafu eti CCM inarecover,siyo kweli ukweli ni huu CCM inakufa,alafu hata ikija,wakati CDM kinaemerge CCM kilikuwa strong na sashv CCM inadhoofu wakati ndo kwanza kumekucha kwa CDM,indikeita zinawashwa nje ndani,CDM inatwanga kotekote
 
Asante Kibunago! Ni wachache sana wenye guts za uliyoeleza. Bahati mbaya wanaCCM wengi ni wagonjwa wakufikiri zaidi ya ushabiki wa kijinga hapa JF wapi na hata mitaani. Ifike wanachama muwe na uwezo wa kukemea wazee walioishiwa fikra zaidi ya kuwaza Gombe Sugu ni mizigo. Kila mwenye akili anajua hili la Magamba ni changa la macho litawagharimu sana
 
Mafisadi waliokuwa ndani ya CCM na ukizingatia ndicho chama tawala hawa si maadui wa CCM peke, la ni maadui wa taifa zima maana wamekigeuza chama kinachotawala kuwa chao na kukiendesha chenyewe na serikali yake kifisadi na kusababisha machungu mengi sana katika maisha ya wengi humu Tanzania.

Nimesikiliza kwa Makini Mdahalo wa Chuo Kikuu juu ya Muswada wa Katiba, ambapo Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Mnauye alinena kuhusu umuhimu wa kupambana na hali ilivyo katika siasa za leo na umuhimu wa vijana kujiunga na mapambano haya, na leo amefafanua kinagaubaga jinsi wanachama wenye nia njema walivyokuwa na wakati mgumu katika kuleta mabadiliko ndani ya CCM. Kijana amekaa vizuri, anahitaji full support ya vijana wengine maana nina uhakika wazee hata waliobaki wako ambao hawako hepi na kasi ya kijana huyu na wenzake.

Huyu ndiye kijana aliyewahi kufukuzwa uanachama "kutoka duniani hadi mbinguni" na aliwahi kunenwa vibaya na viongozi wake kwa msimamo wake dhidi ya wanaolinda ufisadi na udhalimu ndani ya CCM.

Usikate tamaa, kaka tunakuona kama mkombozi katika chama, simamia mabadiliko, nafasi uliyonayo itumie vema kwa kasi hiyohiyo.

CHADEMA haya yanayotokea humo ndani mwenu... mi sisemi...
Cdm kumetokea nini ndg yangu hebu tupe michapo!
 
hapa ni upuuzi tupu!!!!!!!!!!! nape anaropoka kama makamba tu, hata huyo mzee mukama leo nimewasikia wapemba wakiulizia kwake ili wakamduuuuuu,kwani jana amewakejeli kuhusu muungano.
 
Nadhani ndugu zangu hamna kazi ya kufanya kuwafuatilia hawa wasanii ni kupoteza muda wenu. matokeo ya mechi ya leo mpira umekwisha, MADRID 1 NA BARCA 1. BARCE imesonga mbele mpaka fainali. nadhani hii ndio habari ya maana kuliko hao pumbavu wanaodhani Watanzania ni mazezeta.
 
Back
Top Bottom