Nape na Kipindi Maalum - CCM Kujivua Gamba

Nape na Kipindi Maalum - CCM Kujivua Gamba

Nape, asante kwa kutuhakikishia kuwa tuliokuwa karibu tunakata tamaa tusikate tamaa. Katika kipindi cha CCM Kuvua gamba leo nimekusikiliza kwa makini na huu ndio uchambuzi wangu:

1. Safi sana kwa kukumbusha kuwa wale watakaochukia watu wengine juu ya yaliyoazimiwa si sahihi maana ni taratibu au kanuni au maadili yanayogomba dhidi ya vitendo vyao visivyokubalika na si suala au uamzi wa mtu fulani.

2. Nimesikitika kuwa uzito wa maelezo yako ya leo mbele ya luninga katika kipindi maalumu yamepungua uzito wake (diluted in terms of your tone & substance) ukilinganisha na siku ulipopewa dhamana ya Uenezi na katika vikao mbalimbali vilivyofuata mkitambulishwa huko Morogoro, Dar n.k . maana hukumungúnya maneno huko: Niseme wazi kuwa:-

a. Hakuna sababu mpaka leo hamtaki kuwataja waziwazi kwa majina wale walioambiwa kuchukuwa hatua za kutupisha kutokana na malamiko ya wananchi juu ya ufisadi. Haiingii hakilini utueleze maazimio ya kikao lakini usiseme yanamuhusu nani ........................................

Umeeleza vema binafsi mimi sina mapenzi na chama chochote lakini by default CCM ninaichukia. Ukiuliza kuajua kwa nini basi naona kuna baadhi ya majibu umeyatoa. Hivi huko "jikoni" kuna nini hata wale wanaoaminika wakiingia hawaji na mapishi yanayoeleweka kwa watanzania. Tunapikaaaa tunapiaka. ...............

  • Thanks
Reactions: Ame
Mkuu Kibunago, kule katika ngazi ya juu kabisa ya CCM kungekuwa na watu wenye uwezo wa kufikiri kama wewe, kutokuwa waoga na kuchukuwa maamuzi sahihi ya kukisafisha Chama Cha Mapinduzi ili kiwe kile chama ambacho kilipendwa na kuheshimiwa na Watanzania walio wengi basi tungekuwa na matumaini makubwa katika Chama hicho, lakini sasa hivi kumejaa wapuuzi, waongo, mafisadi ambao pamoja na kuona wazi kwamba chama kinatetereka lakini wako tayari kutoa kauli za kipumbavu kila kukicha ili kufurahisha nafsi zao. Safari ya kuizika CCM imeanza rasmi labda watokee watu wenye mtazamo kama wewe na pia hawamuogopi yeyote yule basi ndiyo CCM itaweza kusafishika, vinginevyo ni USANII TUU tena wa hali juu.
 
Mkuu Kibunago,

Kupungua kwa ukali wa kauli za Nape Nnauye ni dalili kwamba amefungwa speed gavana na wenye chama. Nilishasema huko nyuma kwamba swala la kupiga vita ufisadi linahitaji utashi wa Mwenyekiti wa Chama. Kama Mwenyekiti wa Chama naye ni mchafu, hawezi kuwa na ujasiri wa kuwanyooshea kidole wachafu wenzake.

Nape alishasema kile alichotaka kusema na kutekeleza, lakini nguvu yake ina mipaka. Kwa hiyo kama kuna mtu anategemea kwamba Nape ndio atawaondoa mafisadi kwenye chama, hiyo ni ndoto na ndio maana tone ya kuongelea ufisadi imeanza kubadilika na wameanza kujikanyaga kanyaga na kujichanganya. Sina hakika kama wanajua wanachokisema.

Nape alivimba kichwa siku ya Tamasha la Pasaka baada ya JK kusema kwamba anachokisema Nape ndio msimamo wa Chama. Sasa Nape na Mukama ni nani mwenye mamlaka zaidi? Kwanini Mukama anasema hawana list ya mafisadi wala hakuna cha siku 90? Ina maana Nape na Chiligati walijitungia?

Gamba ambalo walitaka kulivua limegoma kutoka, na sasa litaendelea kuwabana na inawezekana likawafanya wawe vipofu na viziwi na huo ndo utakuwa mwisho wao maana watazidi kupoteza mwelekeo.
 
Ni swala la wakati tu, vijana wanasikiliza hoja na kuangalia upepo unakwendaje, siasa si ushabiki ni hoja zenye kuleta mvuto ndiyo mana matokeo uchaguzi hayafanani. kuwepo kwa CHADEMA ni changamoto nzuri kwa kuimarisha CCM, nadhani ndio wanaitumia hiyo nafasi sasa na naona wameanza vema.

Wewe unaishi kwenye pepo ya mabwege, sidhani kama tupo Dunia moja na wewe.
 
Siku naanzisha thread hii niliamini moja kwa moja CCM ya Mh. Kikwete haikuwa na nia ya dhati ya kufanya mabadiliko yoyote ya maana ndani yake. Kauli za Katibu Mukama zinadhihirisha hilo na kwa maana nyingine Nape naye ni pumba nyingine katika chama. Utazungumziaje kutoa siku 90 bila Mukama kujua?
Pengine kwa kuwa wana mtandao ni mabingwa wa kuchezea akili za watanzania na kujipatia madaraka, wanajaribu kwa maksudi kuwahadaa wananchi ili wapate tena 2015. Ikitokea hivyo, sipati picha utajiri wa RA na EL na ule "silent' wa JK utakua kwa kiwango gani kufikia 2020. These people are killing us so fast that no one of us is comprehending.
JK anaonekana kuwa mlipa fadhila mzuri sana kwa wafadhili wake kuliko marais wengi duniani. Amejitolea kwa lolote lakini hawezi kuwasaliti RA, EL na wengine maana walimfaa sana alipokuwa na kiu kali ya title na show off za mercedes benz na bmw zenye nembo ya taifa.
Nisiseme mengi. CCM hawavui gamba wala nini na kama hamuamini subirini muone mwisho wa kauli za Nape kama si aibu tupu!
 
Nape, asante kwa kutuhakikishia kuwa tuliokuwa karibu tunakata tamaa tusikate tamaa. Katika kipindi cha CCM Kuvua gamba leo nimekusikiliza kwa makini na huu ndio uchambuzi wangu:

1. Safi sana kwa kukumbusha kuwa wale watakaochukia watu wengine juu ya yaliyoazimiwa si sahihi maana ni taratibu au kanuni au maadili yanayogomba dhidi ya vitendo vyao visivyokubalika na si suala au uamzi wa mtu fulani.

2. Nimesikitika kuwa uzito wa maelezo yako ya leo mbele ya luninga katika kipindi maalumu yamepungua uzito wake (diluted in terms of your tone & substance) ukilinganisha na siku ulipopewa dhamana ya Uenezi na katika vikao mbalimbali vilivyofuata mkitambulishwa huko Morogoro, Dar n.k . maana hukumungúnya maneno huko: Niseme wazi kuwa:-

a. Hakuna sababu mpaka leo hamtaki kuwataja waziwazi kwa majina wale walioambiwa kuchukuwa hatua za kutupisha kutokana na malamiko ya wananchi juu ya ufisadi. Haiingii hakilini utueleze maazimio ya kikao lakini usiseme yanamuhusu nani .
b. Umesema kuwa siku 90 hazitajwa katika maazimio na kwamba ni waandishi wa habari waliotafsiri hayo. Kumbuka kuwa watu wanarecord yanayosemwa na kiongozi wetu yeyote. Kama kuna mtu alitamka hayo kama yeye ni busara ungeomba radhi na kurekebisha kuwa sasa unaongea kwa niaba ya CCM na tusahau yote ambayo mtu aliongea kama yeye binafsi.

c. Unajua kabisa kuwa sualala Ufisadi ndilo limetupaka matope sana hadi kuleta mbiu ya kujivua magamba. Kwa nini umepata kigugumizi kueleza kama hata barua husika kwenda kwa wahusika zimeshatolewa au bado. Aidha kama mnasoma alama za nyakati hata kwa kufuatana na swali la aliyekuwa anakuinterview, tunaomba ujumbe ufike kunakohusika kuwa itakuwa kichekesho hao watu waachie ngazi tu za nafasi zao katika vikao vya juu vya chama na wakaendelea kuwa Wabunge. Maana umesema mwenyewe kuwa uongozi huo wanaupata kupitia CCM na hivyo, pasipo kujiumauma, waelezwe wajiuzuru Ubunge au nafasi yeyote Serikalini pia. Na Vyombo vyote vya kusimamia sheria na hata Takukuru wachukue nafasi zao kuwafikisha mbele ya sheria juu ya makosa yanayowakabili. Nape, huu ndio unatakiwa kuwa msisito wako popote unapookwenda kama kweli unataka imani na ushindi wa CCM urejee. Wengi tuna imani nawe pamoja na Viongozi wengine wa sasa wa CCM, lakini ebu mseme kile mnachotaka kusema bila kujiuma wala kuhofu mtu maana CCM ni ya WanaCCM na Tanzania ni ya Watanzania wote.

Mtapata vidonda vya tumbo bule nahao mafisadi chama si chetu tena wenye nacho wanahesabika wanalisishana madalaka anatoka baba anaingia mtoto akiuwa analipa faini yanaisha usiumize akili tumia njia mbadara wewe ndo mwenye uwezo wakuwafanya waendelee kuka madalakani au kutoka
 
Ni swala la wakati tu, vijana wanasikiliza hoja na kuangalia upepo unakwendaje, siasa si ushabiki ni hoja zenye kuleta mvuto ndiyo mana matokeo uchaguzi hayafanani. kuwepo kwa CHADEMA ni changamoto nzuri kwa kuimarisha CCM, nadhani ndio wanaitumia hiyo nafasi sasa na naona wameanza vema.

Mkuu Profesa,

Wameanza vyema vipi? Katika siasa hakuna kitu kibaya kama kuendesha shughuli kwa contradictions. Magazeti yaliwapamba sana wajumbe wa Secretariat Mpya pamoja na Operation Vua Magamba ambayo walisema wazi kwamba wanawatema mafisadi. So, expectation ya wananchi ilikuwa kubwa wakisubiri kuona mafisadi wakitoswa.

Leo hii mtendaji mkuu wa chama (Katibu Mkuu) anakana kwamba hawana orodha ya mafisadi na kwamba hakuna barua zilizoandikwa na bado anashindwa/kwepa kujibu kwa ufasaha maswali ambayo anajua wazi kwamba majibu yake yanaongeza utata juu ya utata.

Mukama ndiye aliyeongoza Task Force ya kutafiti sababu za CCM kufanya vibaya kwenye uchaguzi au kwa maneno mengine kuchukiwa na wananchi. Mojawapo ya mambo aliyosema ni pamoja na hoja ya ufisadi, halafu same person anakuja kusema kwamba CCM haina list ya mafisadi.

Mtafiti makini baada ya kuambiwa kwamba mafisadi ndio wanakipaka matope chama chao lazima angeuliza ni mafisadi wepi? Ufisadi upi walioufanya? Lakini report ya Task Force ilikuwa imejaa usanii mwingi sana mpaka wanasema JF ni ya Chadema kumbe hata makada wao kibao wanakesha hapa wakirusha vijembe visivyo na mashiko na wanashindwa kutetea hoja.

Makamba alipoondoka watu walijua kwamba labda sasa angalau CCM itapata uhai, lakini kwa mwendo huu ni bora ya Tambwe Hizza ambaye atakomaa na hoja hata kama haina mashiko ili asije akawa kinyume na msimamo wa chama chake.

Ni aibu kwa Katibu Mkuu kutofautiana na Katibu Mwenezi na pia Naibu Katibu Mkuu wake. Maana Katibu Mwenezi ndio kipaza sauti cha chama, sasa kama kipaza sauti cha chama kinatoa kauli ambazo baadaye zinakuja kupingwa na Katibu Mkuu, then kuna tatizo kubwa zaidi. CCM ina wenyewe na wenyewe ni mafisadi. Nape Nnaye anacheza ngoma asiyoijua, aangalie asije kujuta mbele ya safari.

Kama huo ndo mwanzo mzuri, basi CCM inaelekea kaburini.
 
Mkuu Keil,
Hawa jamaa hawaifuatilii CCM. Nothing good can come out of it kwa kuwa njia wanazotumia kutafuta madaraka ni kubwa na chafu sana kiasi kwamba inapofikia kujaribu kujisafisha na kuwatumikia wananchi wanakuwa hawana nguvu tena. JK ana usafi gani wa kuwatimua kina RA, EL na Chenge.
Iliwahi kuvumishwa habari kwamba wakati bunge likijadili ripoti ya kamati ya bunge juu ya Richmond, RA aliomba kupewa nafasi ya kujibu hoja kupitia kikao cha Bunge akanyimwa kwa kuwa inadaiwa alitaka kumwaga ugali ili aibu iwafike wote maana kwa mujibu wa habari za ndani za CCM hakuna mkubwa msafi humo ndani anayeweza kudai anawaondoa wenzake na yeye kubaki na chama kinachoitwa safi. Wote wananuka na hawaoni haya. CCM wangekuwa na aibu japo chembe EL angejiondoa katika uongozi taratibu na kupotelea kwenye utajiri wake ambao ni wazi umesaidiwa na ufisadi pia lakini no bado anataka urais kwa kuwa anajua akiacha wataingia mafisadi wengine ambao pia ni wabaya wake kama Mzee Six. (By the way hata yeye na timu yake kama kina Nape nk. nao utumbo mtupu. Kimsingi hakuna msafi.)
 
mkama anaishi tegeta nyeshozi barabara ya kuelekea zoo ndipo anaishi mfateni pale kwake mkamuulize kwa nini anawakejeli ila mjue kuna ulinzi mkali c ni kiongozi wa chama kinachotawala alafu nashanga sana hawa makatibu wote wa ccm maka,ba naye anaishi tegeta wazo nkama naye uko uko hivi kuna nini uko wajemen
 
Hakuna ushirika kati ya wafu na wenye uhai ni chukizo kwa Mungu mwenye uhai kushirikiana na roho iliyokufa!
 
Mkuu Kibunago, kule katika ngazi ya juu kabisa ya CCM kungekuwa na watu wenye uwezo wa kufikiri kama wewe, kutokuwa waoga na kuchukuwa maamuzi sahihi ya kukisafisha Chama Cha Mapinduzi ili kiwe kile chama ambacho kilipendwa na kuheshimiwa na Watanzania walio wengi basi tungekuwa na matumaini makubwa katika Chama hicho, lakini sasa hivi kumejaa wapuuzi, waongo, mafisadi ambao pamoja na kuona wazi kwamba chama kinatetereka lakini wako tayari kutoa kauli za kipumbavu kila kukicha ili kufurahisha nafsi zao. Safari ya kuizika CCM imeanza rasmi labda watokee watu wenye mtazamo kama wewe na pia hawamuogopi yeyote yule basi ndiyo CCM itaweza kusafishika, vinginevyo ni USANII TUU tena wa hali juu.

The only exit for CCM na kuepuka gadhabu ya mafisadi ni kutengeneza katiba mpya na yenye power balance hapo kama mwenyekiti ni msafi ange komaa na hilo tatizo kama na yeye ana trace za ufisadi na kama anatafuta succesor waku cover mambo yake hapo sasa atalijua jiji! By the way naomba muelewe kuwa mwanzilishi wa vita vya ufisadi ni Alpha na Omega wengine wote mko katikati na jinsi alivyofanya watu bado mara watanyanyua kila mmoja silaha yake nakuishia kujimaliza wenyewe. Bado nasema mafisadi kiama chenu kimewadi kama ni toba basi nibudi mkaifanya fasta!
 
Kweli Mungu si Athumani.....
Asiye sikia la mkuu.........
Karibu kambi ya fikra mbadala...... Achana na vidonda vya tumbo.
Watanzania tutaijenga Tz wala si ccm.......
USIOGOPE "Kibunago"
 
Naomba kurudia; Jamani! jamani! jamani! CCM hawawezi kuepukana na mafisadi kwa namna yoyote ile kwa sababu hiyo M hapo mwisho si mapinduzi tena siku hizi bali ni Mafisadi.
Tunaofuatilia siasa zao tulijua tangu mwanzo kwamba swala la kuwaondoa baadhi yao katika nafasi mbalimbali za uongozi si kujenga taswira ya chama wala kuongeza mvuto wake kwa wanachi isipokuwa kugawana ulaji na wenzao wanaolalamikia kusahaulika katika kugawana ulaji. Haya ndiyo wengine mnaanza kuyashuhudia kwa kauli zenye tone mpya za Nape na Mukama. Hawa nao walaji tu! Nape alipiga kelele dhidi ya Lowasa mwisho akapata u-DC. Bila kelele hizo asingepata kitu.
Usishangae anachovizia sasa ni uwaziri maana hao anaojifanya kuwasakama sana kwa sasa hawana tofauti na mafisadi wengine ndani ya chama chao na mbaya zaidi wao ndiyo wameshika remote controller inayomwongoza huyo Mwenyekiti ambaye yeye ajipendekeza kumtetea kinafiki. Siwezi kusema sana kuhusu watu baadhi ya watu lakini wengine hawa kama kina Six, Nape, Kilango nk wote ni wasaka ulaji tu.
Six ndo mnafiki kweli. Alisaidia sana bunge kutenda kazi vizuri watu tukamsifu kumbe anafanya hivyo kuwabana mafisadi mwenzake Lowasa na Rostam. Hosea alipojaribu kulipiza kisasi kwa kuhoji posho za wabunge zinazotolewa mara mbili mbili yeye akawa wa kwanza kutetea. Why that kutoka kwa mzee wa "Stds na Speed?"
Narudia tena, CCM ni chama cha mafisadi watupu na watetezi wao waliogawanyika katika makundi. Hakuna wa kuwategemea. Period!
 
nchi hii ni yatima hatuna kiongozi wa Taifa mwenye usafi wa kusafisha wezi wa mali za umma,
historia hiko wazi kulikuwa na kundi la two brother wakati wa kampeni za uchaguzi mwaka 2005 ndani ya ccm, lilivuma sana kumweka JK magogoni,
iweje leo mwasisi mmoja wa kundi awe msafi na mwingine mchafu?

jk kuwashughulikia mafisadi ni sawa na binadamu kuishi na moyo uliokufa, husiosambaza damu mwilini, mafisadi ni rafiki wa jk na wao ni kiungo muhimu kwake kama sisi wanadamu tunavyoitaji damu,
kamwe jk hato wafukuza mafisadi hao ni uhai wa madalaka yake aliyonayo, akifanya hivyo ni sawa na kujitoa roho mwenyewe,
mafisadi wataondoka ccm na kwa taifa ili kama kikwete sio RAIS au MWENYEKITI WA CCM,
kinyume na hapo hizi ni ngonjera za umitashumta zisizo hata na albamu.
kupona kwa ccm ni pale watakapomkataa kikwete na mafisadi wote, yeye ni chanzo cha uozo huu wote kwa njia zifuatazo
kutochukua hatua kwa wezi wa mali za umma
kuwalinda wezi wa mali za umma
kuhacha dini kukashifiana (mfano radio immu moro)
matumizi mabaya ya pesa ya umma ( baraza la mawazi, safari nje ya nchi, watu kupewa vyeo zaidi ya viwili)
mwisho dhuruma ya usipika zidi ya sitta kwa manufaha ya marafiki

Mkuu Kibunago,

Kupungua kwa ukali wa kauli za Nape Nnauye ni dalili kwamba amefungwa speed gavana na wenye chama. Nilishasema huko nyuma kwamba swala la kupiga vita ufisadi linahitaji utashi wa Mwenyekiti wa Chama. Kama Mwenyekiti wa Chama naye ni mchafu, hawezi kuwa na ujasiri wa kuwanyooshea kidole wachafu wenzake.

Nape alishasema kile alichotaka kusema na kutekeleza, lakini nguvu yake ina mipaka. Kwa hiyo kama kuna mtu anategemea kwamba Nape ndio atawaondoa mafisadi kwenye chama, hiyo ni ndoto na ndio maana tone ya kuongelea ufisadi imeanza kubadilika na wameanza kujikanyaga kanyaga na kujichanganya. Sina hakika kama wanajua wanachokisema.

Nape alivimba kichwa siku ya Tamasha la Pasaka baada ya JK kusema kwamba anachokisema Nape ndio msimamo wa Chama. Sasa Nape na Mukama ni nani mwenye mamlaka zaidi? Kwanini Mukama anasema hawana list ya mafisadi wala hakuna cha siku 90? Ina maana Nape na Chiligati walijitungia?

Gamba ambalo walitaka kulivua limegoma kutoka, na sasa litaendelea kuwabana na inawezekana likawafanya wawe vipofu na viziwi na huo ndo utakuwa mwisho wao maana watazidi kupoteza mwelekeo.
 
- Nape is right on the track, mafisadi wanajua kwamba wamepigwa bao ndio maana hata magazeti yao siku hizi yamejaa vichekesho, kila lenye mwanzo huwa lina mwisho, mwisho wao umefika sasa.

- Anaposema Rais wa Jamhuri kwamba kila analosema Nape ni lake, the next ni FULL STOP!

William @ NYC, USA.
 
  • JK ni mchonganishi badala ya kuwa refa .
  • JK ni kama wale majasusi tuliosomama enzi ya vita baridi .wana double deal huku ni CIA na huku ni KGB...
 
Katika mikakati wa kujivua gamba ITV Wamekuwa na vipindi maalumu na leo Nape ndani ya ITV
Nape ametuangusha sana sisi wana mageuzii ndani ya chama chetu kwa kuropoka mambo amabayo yalikuwa nje na maazimio ya kikao namnukuu Bw. Mukama . Haipendezi mwana siasa kijana Nape ambae hata upinzani walikuwa wanajua uwezo wake ameanza kupoteza mwelekeo mapema kabisa kuna nini jamani huyu ndiye kijana pekee ndani ya chama chetu aliyekuwa na mvuto mbele ya watanzania. Kusema kweli 'generation gap ' ndio inatesa chama chetu kwa maana sasa hivi hakuna mwana siasa kijana ndani ya chama ambae anaweza kuvaa viatu vya Bw, Nape. Chonde chonde NAPE kama ukitaka kulinda hesima yako mbele ya umma wa watanzania ambao tukju nyuma yako simamia ulichokuwa unawaeleza wananchi kwenye mikutano yako ya hadhara hata kama Bw.Mukama amekukatisha tamaa
 
Back
Top Bottom