Nape na Kipindi Maalum - CCM Kujivua Gamba

The Analyst

JF-Expert Member
Feb 26, 2011
464
246
Waheshimiwa wanaJF,
Salaams!

UPDATE:
Katibu Mukama ameamua kuwa wazi. CCM hawana orodha ya mafisadi wala hawajatoa siku 90 kwa mtu. "Kwa ujumla hakuna mwana-CCM msafi kama Mapacha watatu" aaaah!...ha..ha..haaaaah! Guys, I told you CCM ni nyoka kweli. Ndiyo maana hata Mwenyekiti wao hakuwa na mfano wowote mwingine katika kuelezea wanachokusudia kuwaaminisha wadanganyika isipokuwa mageuzi ya mara kwa mara ya nyoka kwa kuvua magamba tena alisahau kusema mwenye sumu kali.

Kama huzijui aina za sumu ya CCM (Nyoka wa magamba) fuatilia kauli za kuwapo udini, ukabila, ukanda nk. hapa nchini wakikusudia kuua nguvu za vyama vya upinzani. Hawa jamaa wakizidiwa wapo tayari hata kuwatumia viongozi wajinga wajinga wa dini ili kuanzisha vurugu ambazo zitasaidia kuwalinda wao na mali zao. Lakini bado naamini tunayo nafasi ya kutetea nchi yetu iliyopoteza mwelekeo. May the Almighty God save us from these people.
Time will tell, and God willing these people will pay for this one day. And they will pay so dearly that no one will ever try to imitate what they have done to our country. (end of update)

Tunaojua tabia ya unafiki wa CCM tuliposikia CCM inatarajia kuondokana na baadhi ya viongozi/wanachama wake wanaotajwa kuhusika na ufisadi mkubwa tulijua maigizo yanaanza hivyo tukakaa tayari. Watu wengi wameshabikia sana habari hiyo lakini wengine tunajua chama hiki kina unafiki mno kiasi kwamba hawa jamaa wasipotaka kuondoka wenyewe basi mambo yatafifia na kupotea.

Kama nakumbuka vizuri kelele zote kuhusu kuwapa watu hao siku 90, kuwaandikia barua nk. zimekuwa zikipigwa na viongozi wao wapya ndani ya Sekretarieti wengine hata bila kuulizwa sasa cha ajabu tayari wameshaanza kupingana wao kwa wao. Wengine wanasema siku 90 na kuwaandikia barua watuhumiwa wa ufisadi hayakuwa maazimio ya vikao vyao n.k n.k n.k
Habari ifuatayo kutoka Gazeti la Nipashe inaonesha hata anayepaswa kuandika hizo barua na lini zitaandikwa haijulikani. Hii inawezekana wapi kama si maigizoni tu? Mkiambiwa CCM wanajaribu kufanya kiini macho katika kushughulikia ufisadi mtasema mnadanganywa?

Barua za mafisadi wa CCM zaumiza Msekwa, Mukama

Na Joseph Mwendapole
23rd April 2011


headline_bullet.jpg
Kila mmoja akwepa ni lini zitaandikwa
headline_bullet.jpg
Wengine wawa mbogo, kuulizwa hayo



Wingu la ufisadi bado linazidi kuwaumiza vichwa viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), baada ya vigogo wa ngazi za juu wa chama hicho kuogopa kuweka wazi iwapo watuhumiwa wa ufisadi ndani ya chama hicho wameshakabidhiwa barua za kuwataka wajiondoe wenyewe.


Kila kiongozi aliyetafutwa jana kuzungumza iwapo tayari chama kimewaandikia barua za kuwataka wajiondoe kwenye chama hicho, aling'aka na kuelekeza aulizwe mwenzake.

Wa kwanza alikuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, ambaye alisema suala hilo halishughulikiwi na idara yake hivyo alielekeza aulizwe Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama.

Alisema kila idara inajukumu lake na kwamba ofisi yake ni ya kuzungumzia masuala ya chama, lakini si mambo yanayohusu masuala ya utendaji.

"Kila idara inawajibu wake, hilo haliko kwenye idara yangu, mimi ni msemaji wa chama nitafuatilia kujua kama zimeshaandikwa na kuwasilishwa kwa wahusika ila anayeweza kulisemea ni Katibu Mkuu," alisema na kuongeza:

"Jumatano watu wote wakiwa ofisini nitakuwa katika nafasi nzuri ya kulizungumzia hilo, nitafuatilia kujua kama zimeshaandikwa na kukabidhiwa kwa wahusika au la, lakini kwa sasa sijui lolote kuhusu hizo barua," alisema Nnauye ambaye kabla ya kushika wadhifa huo alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Masasi.

Alipotafutwa Naibu Katibu Mkuu Bara, John Chiligati, alisema anayeweza kulisema suala hilo ni msemaji wa chama, Nnauye kwa kuwa si kila mtu anaweza kuzungumzia masuala ya chama.

"Chama kinamzungumzaji wake ambaye ni Nape, mtafute Nape maana kila mtu akianza kuzungumza mambo ya chama itakuwa vurugu, ukimpata yeye atakueleza vizuri," alisema.

Alipotafutwa kuzungumzia suala hilo, Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, alikuwa mkali na kuelekeza kuwa aneyefaa kuulizwa ni Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa.

"Hayo unayoniuliza sikuwahi kuagiza yafanyike na wala si wajibu wangu, mtafute Makamu Mwenyekiti ndiye atakueleza, kwanza kwa sasa niko kijijini kwangu kuna mambo mengine nafanya," alisema Mukama na kukata simu.

Alipotafutwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho, Pius Msekwa aligeuka mbogo na kuhoji mwandishi anatafuta habari hizo kwa ajili ya kuzipeleka wapi.

Baada ya kuulizwa iwapo chama hicho kimeshawaandikia barua watuhumiwa wa ufisadi, Msekwa alikuwa mkali na kumweleza mwandishi kuwa masuala hayo ni ya ndani ya chama na hayamhusu.

"Hizi habari unatafuta za nini wakati hazikuhusu, unajua kuna habari za kuandika na zingine si za kuandika, hizi ni za kwetu ndani ya chama na hazikuhusu unataka za nini kwaheri," alisema Msekwa na kukata simu.

Wiki iliyopita, Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ilimuagiza Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilson Mukama, kuwaandikia barua viongozi wanaotakiwa kujiuzulu kuwafahamisha kwamba, kama hawatafanya hivyo kikao kijacho cha NEC kitawafuta uongozi.

Watuhumiwa hao wa rushwa na ufisadi wakiwemo wajumbe wa NEC taifa, wamepewa muda wa miezi mitatu sawa na siku 90 wapime uzito wa tuhuma zinazowakabili, wajiuzulu wenyewe.

Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Pius Msekwa, alieleza msimamo huo mjini Dodoma wakati wa mkutano wa kuwatambulisha wajumbe wa sekretarieti mpya akiwemo Katibu Mkuu, Wilson Mukama.

Hatua hii ni mchakato wa CCM kujivua gamba. Tayari wajumbe wa Sekretarieti na Kamati Kuu walikwisha kujiuzulu na kutoa fursa ya kuteuliwa wengine. Maamuzi yaliyofanyika Dodoma wiki mbili zilizopita.


CHANZO: NIPASHE
 
Ni unafiki tu wa CCM kutaka kuwazuga Watanzania. Ooh! Tunavua gamba, sijui gamba hili ni nani aliyewavalisha na aliwavalisha lini na kitu gani kilichowafanya wakubali kulivaa gamba hilo. CCM haisafishiki hata kwa miaka chungu nzima ijayo. Rushwa na ufisadi ndani ya chama hicho imesambaa kwa kiasi kikubwa na tunaweza kuifananisha na ugonjwa wa saratani ambao umeshesambaa sehemu kubwa ya mgonjwa mhusika na hakuna matumaini tena ya kupona.
 
Kuna mtoto wa kigogo ambaye anataka kuanzisha tawi la CCM ni NY. Kumbe anajaribu kuwazuga WTZ. Duh! inatia aibu kuona watoto wa vigogo wa CCM bado wanaendeleza ufisadi wa baba zao kwa njia yoyote ile.
 
account zote ziwe audited na ripoti zote ziwekwe wazi. Watakaogundulika wamefanya ubadhirifu wavuliwe uongozi na kuchukuliwa hatua za kisheria. Kuvua magamba kusiwalenge viongozi wa juu tu bali viongozi wote wa chama kuanzia mashina hadi jumuiya za chama wakaguliwe.
 
Hiii ni sawa na ile ya panya na paka! panya gani ataenda kumkamata paka????
 
safi sana, hivi zile siku tisini si alitoa msekwa na sasa kawa mbogo, sasa ni kusubiri siku tisini zifike afu tujue, ngoja tuanzishe thread nyingine tuiite COUNTDOWN TO THE VERDICT! hapo tuweke story za kila siku kuelekea siku 90, will help us to see how things unfold na kuuona utapeli wa CCM aka Chama Cha Magamba
 
safi sana, hivi zile siku tisini si alitoa msekwa na sasa kawa mbogo, sasa ni kusubiri siku tisini zifike afu tujue, ngoja tuanzishe thread nyingine tuiite COUNTDOWN TO THE VERDICT! hapo tuweke story za kila siku kuelekea siku 90, will help us to see how things unfold na kuuona utapeli wa CCM aka Chama Cha Magamba

mkuu umetoa wazo zuri countdown ya siku hizo 90 ili tujue hii movie ya ccm na mafisadi inaishaje
 
Ni unafiki tu wa CCM kutaka kuwazuga Watanzania. Ooh! Tunavua gamba, sijui gamba hili ni nani aliyewavalisha na aliwavalisha lini na kitu gani kilichowafanya wakubali kulivaa gamba hilo. CCM haisafishiki hata kwa miaka chungu nzima ijayo. Rushwa na ufisadi ndani ya chama hicho imesambaa kwa kiasi kikubwa na tunaweza kuifananisha na ugonjwa wa saratani ambao umeshesambaa sehemu kubwa ya mgonjwa mhusika na hakuna matumaini tena ya kupona.

Hili lilifahamika tangu mapema hizi ni mbinu za CCM na serikali ya JK kupunguza pressure ya wananchi na si jingine.Ukifuatilia maamuzi mengi ya CCM hayalengi masilahi ya Wananchi bali yanalenga kulinda masilahi yao,harakati zao nikuvuta muda tu na kutufanya watanzania kua katika hali ya "FISI NA MKONO WA MTU AKIFUATILI KWA MATUMAINI YA KUA UTAANGUKA WAKATI WOWOTE"Fuatilia mtililiko wa maamuzi yao.Hakuna mafisadi wala makundi CCM uamuzi tunavuja makundi ikaundwa tume nakupewa muda kuvunja makundi,Hakuna ufisadi Jk anatoa muda wa kujivua magamba unafika muda wa kujivua magamba zinatolewa siku 90!Tusije tukashaanga baada ya siku 90 tukasikia ahadi nyingine.Anachokifanya Jk na CCM ni kuvuta muda na kupima upepo.Magamba yapo mmekaa vikao tulichokitegemea ni uamuzi sio ngojera siku 90 za nini?WANANCHI NI PEOPLES POWER PEKEE ITAKAYO TUONDOA KATIKA USANII HUU MASIKIO YA CCM NA JK HAYASIKII LUGHA NYINGINE ZAIDI YA HII.MUNGU IBARIKI TANZANIA.
 
mkuu umetoa wazo zuri countdown ya siku hizo 90 ili tujue hii movie ya ccm na mafisadi inaishaje
ngoja basi nikusanye habari afu tuweke hiyo thread, nacheck tarehe waliyotoa hizo siku tisini, nini kimetokea toka wakati ule hadi leo, na tutaendela kushare kadiri siku zinavyoenda hadi tutapifika siku tisini, maana CCM ni movie tamu kulizo hizo za kina kanumba, wacha tuitazame kwa pamoja :)
 
Leo usiku katika kituo cha ITV kutakuwa na kipindi maalum cha CCM kujivua gamba, nadhani sasa upotoshaji wa CDM juu ya kujivua gamba kwa umma utakuwa mwisho.

Kwa muda mrefu CDM wamekuwa wakipotosha maana halisi ya kujivua gamba, tofauti na tafsiri yake halisi.
 
Wakijivua gamba itabidi tuwaogope kama ukoma maana kasi yao ya wizi itakuwa imeongezeka maradufu na ujanja ujanja wao utazidi kuliko ule wa nyoka halisi. Dawa ya hawa ccm ni kuwakata kichwa tu.
 
Issue ni kuweka historia sawa na kuwaziba mdomo watu wanaopotosha falsafa ya kujivua gamba.
 
Leo usiku katika kituo cha ITV kutakuwa na kipindi maalum cha CCM kujivua gamba, nadhani sasa upotoshaji wa CDM juu ya kujivua gamba kwa umma utakuwa mwisho.

Kwa muda mrefu CDM wamekuwa wakipotosha maana halisi ya kujivua gamba, tofauti na tafsili yake kama halisi.

Kuna ngoma huchezwa mikoa ya pwani inaitwa Toko Mile bila shaka wewe ni Jongwe kwenye hilo....
 
Leo usiku katika kituo cha ITV kutakuwa na kipindi maalum cha CCM kujivua gamba, nadhani sasa upotoshaji wa CDM juu ya kujivua gamba kwa umma utakuwa mwisho.

Kwa muda mrefu CDM wamekuwa wakipotosha maana halisi ya kujivua gamba, tofauti na tafsili yake kama halisi.

Hapo penye red sijakuelewa!

Naona mna haha sasa - Mara TBC1 mara ITV mara Channel 10 - shame on you!

Anywayz mimi na familia yangu tutakuwa tunaangalia Soccer Chat ikifuatiwa na mtanange kati ya Barcelona FC & Real Madrid - siwezi kupoteza UMEME (wa mgao?) kuangalia MAGAMBA!
 
Back
Top Bottom