Kiungani
JF-Expert Member
- Feb 2, 2007
- 274
- 71
Nape nape nape nape nape.
Ni rahisi ngamia kupenya kwenye tundu la sindano kuliko ccm -magamba kuwatosa magamba wenzao
nape, chiligati, na mkulu siku ile walitoka kwa mbwembwe sasa wananywea wenyewe hivi hawakujua kwamba mapacha watatu ndio walioshikiria ccm na ndio wanoendesha serikali ya kimtandao?
..........................................
Nape na Chiligati wanajua sana nguvu za RACHEL, na kwa upande fulani mimi naamini kabisa kuwa Nape ana nia ya dhati (na kisasi pia) ya kupambana na hawa jamaa RACHEL.
Nape aliamini na bado anaamini kuwa kuondoka kwa Makamba, na kauli za support anazopata kutoka kwa Mwenyeketi JK na Makamu Msekwa, kunampa nguvu na ubavu wa yeye Nape kufuatilia kwa kina kuwaondoa RACHEL.
Hilo ni kosa kubwa sana.
Kwa wanaomjua JK na hata Msekwa na Kinana pia, hawa watatu ni wazuri sana wa kuagiza na kuhakikisha kuwa vidole vyao havigusi moto. Ukiungua, unaungua wewe wao wanachekelea tu kwa mbali.
Hili suala la RACHEL lingeenda mbali na kufukuzwa chini ya siku 90 (kuanzia hiyo April 10), kama kweli JK, Msekwa na Kinana walikuwa na dhati ya kufanya hivyo.
Ukiongezea na ukweli kuwa makombora toka kwa RACHEL kwenda kwa JK kupitia kwa Ridhiwani ndiyo kwanza yalikuwa yanaanza, ni rahisi kuona woga wa kunguru kukimbiza ubavu wake na kuwaacha akina Nape na Chiligati wameshika tama.
Mukama has no clue whatsoever kuhusu nini kinaendelea. Huyu aliandika tu report ya kuchakachua (JF mali ya Chadema, mafisadi, blah, blah, etc), akavuta posho yake akajua yameisha. Huku wenzie wakaona basi 'mpe huyo huyo kazi atekeleze'. Hajui nini anataka, nini kinahitajika na wala nini kifanyike. Makamba ana nafuu sana, na time will tell.