Nape: Lowassa kapoteza sifa ya kugombea

Nape: Lowassa kapoteza sifa ya kugombea

[h=1]Nape asema wanaotangaza nia wamepoteza sifa[/h]
Kwa ufupi
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema Dar es Salaam jana kwamba chama hicho kinaamini katika umoja na mshikamano na kwamba wanaotangaza nia ya kugombea urais kabla ya muda wamepoteza sifa kwa kuwa ni kama wanakigawa.





Dar es Salaam.
Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimesema mwanachama yeyote anayetangaza nia ya kuwania nafasi ya urais kabla ya muda mwafaka kutangazwa, anapoteza sifa ya kuwa mgombea.


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alisema Dar es Salaam jana kwamba chama hicho kinaamini katika umoja na mshikamano na kwamba wanaotangaza nia ya kugombea urais kabla ya muda wamepoteza sifa kwa kuwa ni kama wanakigawa.

Juzi, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa alitangaza nia ‘kimtindo’ akisema anaanza rasmi safari aliyoiita ya matumani ya ndoto zake, ambayo pia itatimiza ndoto za Watanzania za kupata elimu bure, maji safi na maendeleo ya uhakika.

Lowassa ambaye amekuwa akitajwa kuwa mmoja wa wagombea wa nafasi ya urais kupitia CCM katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, alitangaza hayo katika ibada ya shukrani ya kuupokea mwaka mpya, katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Monduli.

Nape alisema wanaotangaza nia ya kuwania urais hivi sasa wanafahamu kwamba hawana sifa za kuwa wagombea wa nafasi hizo kwa sababu mbalimbali.

Alisema wanafahamu wazi kwamba vikao vya chama havitawapitisha kutokana na kutuhumiwa kwa rekodi zao pia ni mbaya.

“Suala hili liko wazi katika chama chetu, viongozi wenye sifa waliowahi kuongoza nchi hii hawakujitangaza mapema. Walisubiri na muda ulipofika wakatangaza nia ya kuwania,” alisema Nape.

Alisema kwa hao wanaojitangaza hivi sasa kabla muda, wanakigawa chama na kwamba vikao havitawapitisha labda wafanye hivyo kupitia vyama vingine.

“Labda wagombee urais kupitia vyama vingine lakini si CCM, chama hiki kina misingi na taratibu zake, wanachama wanashikamana hadi muda utakapofika,” alisema.

Alisema viongozi bora hawapatikani kwa kujiandaa wao wenyewe kuchukua nafasi hizo, bali kwa kuombwa na wanachama wenzao katika hatua mbalimbali zinazokubalika.

Urais CCM

Oktoba mwaka jana, Rais wa Zanzibar, Dk Mohamed Ali Shein alielezea kushangazwa na tabia ya baadhi ya wanachama wa CCM kutangaza nia ya kuwania nafasi za uongozi kwa uchaguzi wa 2015 ikiwamo nafasi ya urais wakati wahusika wa nyadhifa hizo bado hawajamaliza muda wao.

Akifungua Mkutano wa Makatibu wa CCM wa Mikoa, Dk Shein aliwataka watu hao kusubiri hadi chama kitakapotoa mwongozo.

Katika ziara ya Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana kwenye mikoa ya Kusini na Nyanda za Juu Kusini, mwishoni mwa mwaka jana, alisema wanaotangaza nia mapema, wanajitengenezea mazingira magumu ndani ya chama.

Mbali na Lowassa, wengine wanaotajwa kuwania nafasi hiyo ni pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, Mbunge wa Songea Mjini, Dk Emmanuel Nchimbi na Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba.




Source: Mwananchi.
 
Acha kupotosha watu weka chote nilichosema. Nilichosema ni kuwa yeyote anayekiuka taratibu za chama katika mchakato ANAJIONDELEA SIFA za kuwa mgombea wa chama hichi!(Labda Chama kiamue kutofuata taratibu zake chenyewe, na kikiziacha hakina namna ya kuendelea kuaminiwa)! Sasa si swala la Lowassa ni swala la KILA ANAYEKIUKA TARATIBU!kama naye anakiuka anaingia kwenye mkumbo huo, sio kwasababu ni Lowassa ila kwasababu ni mwana CCM na taratibu za CCM haziruhusu! Sio swala la Nape ni swala la taratibu,kanuni na sheria zilizowekwa kabla hata Nape hajazaliwa!

Haiwezekani watu wagawe rushwa hovyo tukae kimya tu kisa anayegawa flani!!!! Hivi kuna uwezekano wa kuingia na kiti moto msikitini ukapigiwa makofi?!! Unaweza kupigiwa makofi na kupewa uongozi wa kanisa wakati humwamini Yesu Kristo?!! Watanzania tusiogope kusema ukweli maana ndio utakaoiponya nchi yetu.
Kama mnamgombea ana sifa atachaguliwa tu huna haja ya kuongezea sifa zake kwa rushwa! Haya si yangu ya CCM, na ni kwa madiwani, wabunge na hata urais!
HERI YA MWAKA MPYA 2014!

kaka ni maneno yako haya au kuna mtu ka hack a/c yako jf?kama ni kauli yako basi mkuu una guts.unastahili thumb up.i admire you bro.
 
Acha kupotosha watu weka chote nilichosema. Nilichosema ni kuwa yeyote anayekiuka taratibu za chama katika mchakato ANAJIONDELEA SIFA za kuwa mgombea wa chama hichi!(Labda Chama kiamue kutofuata taratibu zake chenyewe, na kikiziacha hakina namna ya kuendelea kuaminiwa)! Sasa si swala la Lowassa ni swala la KILA ANAYEKIUKA TARATIBU!kama naye anakiuka anaingia kwenye mkumbo huo, sio kwasababu ni Lowassa ila kwasababu ni mwana CCM na taratibu za CCM haziruhusu! Sio swala la Nape ni swala la taratibu,kanuni na sheria zilizowekwa kabla hata Nape hajazaliwa!

Haiwezekani watu wagawe rushwa hovyo tukae kimya tu kisa anayegawa flani!!!! Hivi kuna uwezekano wa kuingia na kiti moto msikitini ukapigiwa makofi?!! Unaweza kupigiwa makofi na kupewa uongozi wa kanisa wakati humwamini Yesu Kristo?!! Watanzania tusiogope kusema ukweli maana ndio utakaoiponya nchi yetu.
Kama mnamgombea ana sifa atachaguliwa tu huna haja ya kuongezea sifa zake kwa rushwa! Haya si yangu ya CCM, na ni kwa madiwani, wabunge na hata urais!
HERI YA MWAKA MPYA 2014!

Heeee!! Kumbe hata wewe kutoka chini ya kilindi cha moyo wao unaamini nchi iko ICU??
Ukombozi uko karibu.
Mungu ibariki TZ!
 
[JFMP3][MENTION]safar;8268232]Nape punguza mdomo usijifanye mungu mtu,mimi naunga mkono lowasa kuwa mgombea kwasababu uweza anawo sababu anayo mwisho
anamaamuzi magumu nchi itanyooka


true
 
  • Thanks
Reactions: Sal
jeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeembeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!!!!!!!!
 
mwacheni kwanza anunue nunue pikipiki vijana wafaidi mbona mnamkatisha tamaa bwana.
 
Nape ni kiongozi wa CCM lakini mwenzake ana kundi kubwa na chama ni watu.Sasa siijui atashindana na huyo jamaa kivipi.Pili Lowassa hakutamka wazi kuwa anataka kugombea ila aliongea kwa mafumbo.

Nape kazi ya kutumika itakuumbua!

Mkuu EL hana chake CCM wanamzuga tuu na kuzitafuna hela zake hao akina Kpt. Komba na wenziwe, nnavyojua mimi EL alishamalizwa kisiasa kwa ishu ya RICHMOND ngoja utaona tuu bado mda kidogo

EL hajasoma alama za nyakati na hajui kuwa anaowaona marafiki mda huu ni wanafiki wakubwa wanaomtumia kujijenga kisiasa kwenye majimbo yao na utakapofika mda ndo atakapojua ukweli
 
Ukweli unabaki pale pale kuwa Nape ni jasiri sana na anajua anafanya nini. Wachumia tumbo wengi wa umri wake hawawezi kufanya wala kuthubutu kufikiria kama Nape. Kwa hiyo mpeni moyo kijana mwenzenu. Wazee wanajua uwezo wake na ndiyo maana wamemwamini. Nape hizi kelele za wasiojua zisikukatishe tamaa bali zizidi kukupa nguvu ya kukaza buti. All the best and Happy New Year!

Are you serious? au ndo unajipendekeza huyu jamaa hamna kitu na ni mchumia tumbo labda kama unamuongelea Nape wa zamani hizo
 
Nape ni LIJ.NGA sana...lina akili kama za MACHADEMA,yote ni maj.nga sana.
 
Nape, we sema sema tu, wakiingia madarakani hao, sijui utajificha wapi

Watafanya nini CCM wenzake hao? CCM wote lao moja, katika CCM hakuna kuwajibishana. Pia wasemacho SIYO waaminicho!! TAFAKALI CHUKUA HATUA!
 
Mhe. Nape, tofautisha kati ya kutangaza nia kabla ya wakati na swala la ugawaji rushwa. Ugawaji rushwa ni swala pana sana na hii hutegemea kada mbali mbali za mtoa rushwa, mpokeaji, mazingira ya rushwa yenyewe mfano, kazini, shuleni, hospitalini na popote pale na hasa kwanini rushwa itolewe na je rushwa hiyo ni ya aina gani au kiwango gani?

Aya ya kwanza umezungumzia kanuni, sheria na taratibu ambazo naamini wewe unasema zimevunjwa na wanasiasa. Aya ya pili unazungumzia rushwa ambayo haina cha mwanasiasa, muuza gongo, mtoto, mtu mzima,tajiri, maskini wala jinsia. Swali ni je? Utoaji rushwa nao unasubiri muda maalum kama ambavyo kutanzania nia inavyosubiri? Kama hapana, kwanini takukuru isiwashuhulikie hao unaowaona wanatoa na kupokea rushwa? Swali lingine, Nape unadhani kusemea rushwa kwenye mitandao na vyombo vingine vya habari ndio kupambana na rushwa au ni kuonesha kwamba kusema tu bila vitendo ni sawa na kuibariki rushwa?
Kazi ya takukuru ni nini? Kama wewe umeshuhudia ugawaji rushwa hovyo ukiwa miongoni mwa watendaji wakuu kwenye dola halafu unabaki kulalamika huoni kwamba utaonekana una agenda yako binafsi, chuki, fitna n.k zilizojificha kwenye habari za uongo ili tu uwapotoshe wanafuatilia taarifa zako kuhusu wabaya wako?
I love the way you are active but don't be active for nothing kaka.
 
Hii nchi beki hazikabi msishangae EDO akaukwa Urais sijui Nape utakimbilia wapi na hicho kitambi
 
Maandiko yanasema "ACHA WAFU WAZIKE WAFU WAO". Je inawezekana mfu akamzika mfu mwenzake? jibu ni ndio. Mtu yeyote anaehusudu dhuluma, rushwa, ufisadi, unyang'anyi, uporaji, ujangili, uhalifu na mambo yote yanayo fanana na hayo kwa mantiki ya Biblia ni mfu au maiti inayotembea (a walking corpse). CCM ikiweza kumpitisha kugombea mtu wa hivyo basi kitakuwa ni chama cha wafu yaani CCW. Huyu lowasa anajurikana kabisa anamakundi ya kimungiki, na hao wanaomshabikia ni wafu wa kawaida tu. Nape usikubali kuwa mfu, ni bora uwetayari kukatwa kichwa kwakusimamia kweli hii
 
Nape haogopi hata wazee..!! Lowasa ni mzee, mheshimiwa, mchapakazi, tajiri, sio mchoyo, ni mfadhili wa ndani, mwenye kuthamini watu, mtoaji wa zaka, sadaka na michango makanisani, mwezeshaji wa vijana, n.k.

Yeye siyo mfanya biashara hizo pesa alizotoa wapi! amekuwa mtumishai wa umma tangu, najua utasingizia anang'ombe sasa hao ng'ombe ni mamilioni mangapi hadi awe anagawa michango makanisani kama njugu? Mnadhani ataupata labda urais wa kumwaga watu damu jeshi limsaidie lakini kama ni kwenye masanduku ya kura ameula wa chuya
 
Nape ni nani katika siasa za Tanzania hata aweze kumzuia kigogo mkubwa wa ccm kama Lowasa kuteuliwa? Namwona kama mropokaji tu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom