Crashwise
JF-Expert Member
- Oct 23, 2007
- 22,227
- 8,760
- Thread starter
- #21
Acha kupotosha watu weka chote nilichosema. Nilichosema ni kuwa yeyote anayekiuka taratibu za chama katika mchakato ANAJIONDELEA SIFA za kuwa mgombea wa chama hichi!(Labda Chama kiamue kutofuata taratibu zake chenyewe, na kikiziacha hakina namna ya kuendelea kuaminiwa)! Sasa si swala la Lowassa ni swala la KILA ANAYEKIUKA TARATIBU!kama naye anakiuka anaingia kwenye mkumbo huo, sio kwasababu ni Lowassa ila kwasababu ni mwana CCM na taratibu za CCM haziruhusu! Sio swala la Nape ni swala la taratibu,kanuni na sheria zilizowekwa kabla hata Nape hajazaliwa!
Haiwezekani watu wagawe rushwa hovyo tukae kimya tu kisa anayegawa flani!!!! Hivi kuna uwezekano wa kuingia na kiti moto msikitini ukapigiwa makofi?!! Unaweza kupigiwa makofi na kupewa uongozi wa kanisa wakati humwamini Yesu Kristo?!! Watanzania tusiogope kusema ukweli maana ndio utakaoiponya nchi yetu.
Kama mnamgombea ana sifa atachaguliwa tu huna haja ya kuongezea sifa zake kwa rushwa! Haya si yangu ya CCM, na ni kwa madiwani, wabunge na hata urais!
HERI YA MWAKA MPYA 2014!
mkuu nape kwanza kheri ya mwaka mpya 2014, binafsi nimesikia magazetini sijaipata habari yote.
halafu ili tukuone wewe siyo mnafiki tuambie siku 90 ulizompa lowasa, chenge, kikwete zinaisha lini?
ni kweli nape kabla hujahongwa ukuu wa wilaya ulikuwa msema ukweli lakini baada ya hapo na kupewa ukatibu mwenezi ukawa mtukanaji hata hapa huchelewi kuikana hii ID..