Nape kutikisa Arusha/Moshi Jumamosi wiki hii

Nape kutikisa Arusha/Moshi Jumamosi wiki hii

Kwani habari ya kuandaa maandamano nayo ni waraka wa siri? Aende zake Zanzibar akamuombe radhi Makamu wa rais (sijui wa kwanza au wa pili)!
 
Si barua ya uchochezi..ni taarifa kwa viongozi wa chama kimkoa..il wapate taarifa za Maandamano ya Amani mara baada ya Bunge...Ccm waache uwoga!!......!!ni kama Nape alvowapa taarfa viongoz wa Mby juu ya ujio wa Viongoz wa CCJ...NA WARAKA HAUKUWA WA Siri...NAPE ACHA KUJIFILISI KISIASA
 
nape hovyooo kabisa. Hivi hana kitu cha maana cha kufanya kwa Taifa lake? Ili angalau siku moja tumkumbuke?
 
Tatizo la wanaJamvi wengi wanapoona mabadiko ya CCM yenye negativity basi hawataki kuhakiki kwa kuamini CCM ipo kwenye negative side. Wakiona negativity ya CDM wengi sana wanapinga vikali kana kwamba CDM haiwezi kucheza faulo za kisiasa. Ukekereketwa katika kufikiria siyo kitu cha maana sana kwani hupotosha ukweli. Kuweni Great Thinkers kwa kuchambua mambo yote kwa usawa na siyo kishabiki.
 
akili ya kuambiwa changanya na ya kwako. kataeni kuchangia maendeleo mtabaki na maeneo yenu ziii wakati daktari wa ukatoliki anafaidi posho bila kodi na kuiba wake za watu.

nape amewakamata pabaya chadema.
 
Kumjibu huyu mpuuzi ni kupoteza muda yeye aendelee kuhutubia stand maana anajua hawezi kupata watu akiwa nje ya hapo.Chadema they are not low ndugu Maranya kwamba waanze uchochezi no never na hawawezi kujibu upuuzi wa Nape watu wako busy na mambo ya maana .
 
Nani anaamini Nape ni timamu kifikra !
With respect of your name and comments, I'm convinced that you think mechanically and you don't deserve to be a Great Thinker rather than Great Sinker of rubbish. I'm sorry for whole Jamvi.
 
ila kazi ya nape ni katibu mwenezi asipofanya hivyo unafikiri atakula wapi ndo kazi hiyo..
 
siku hizi kila kitu ni nyaraka za siri!!!
 
Huyu Nape ana laana au nini hasa kinamsumbua? Juzi katoka kuropoka kwamba Maalim Seif alikubali 'yaishe' kwa sababu ya njaa. Leo anasema kadaka waraka wa siri. Kuna siri gani hapo wakati Singida wanajindaa kumhoji Lissu kwa kukataza michango ya kushibisha 'matumbo' ya wakubwa? Hela za maendeleo zipo kama ambavyo hela za 'kupitisha' bajeti zipo. Shida ni kwamba ulafi wa ccm hauna mipaka, wanakula kodi, wanakula hela za madini, wanakula hela za misaada, na sasa wanataka hata hivi shilingi vya pareto na pamba tuwape kwa kisingizio 'michango ya maendeleo'.

Miaka 50 tunachanga tuna nini cha kuonesha? ATC? Reli? Machine Tools? au taa za barabarani? dawa hospitalini au maendeleo ya shule za kata? Kila kukicha wananchi wanachanga madawati hivi huwa yana-expire au wanageuza kuni? Nchi hii ni kama iko kwenye 'reverse' gear!
 
Kenge akikatika mkia anabakia kuwa kenge tu!
Bata akiharisha usimpe dawa. Ndo kawaida zake.
 
Nape umeshindwa kunasa nyaraka za wale twiga waliosafirishwa nje unanasa barua za cdm? Umeshindwa kutuambia nani aliua raia kwenye migodi ya madini leo unajitapa na barua tena zenye kuhamasisha maandamano nchi nzima tena kwa amani? Wewe ni kilaza kweli..
 
Mh. wa propaganda leo kwa kutana na kimbembe baada ya wakazi wa Moshi kumpokea na mabango ya kejeli juu ya CCM kwa mfano bango moja lliandikwa "CCM NI YA NYERERE IMEZEEKA""HATUTAKI KUVUA GAMBA TUNATAKA UMEME"
 
Katika hali inayoweza kutafsirika kama kumwadhibu vikali Katibu Mwenezi wa CCM Nape Nnauye, wakaazi wa mji wa Moshi leo hawakuonekana kabisa kwenye mkutano wake.

Pamoja na strategy yao ya kuufanyia mkutano huo mahali penye pilika pilika za watu (stendi), bado wakaazi wa Moshi waliendelea tu na shughuli zao pembeni mwa mkutano huo kama vile hakuna kinachoendelea.

Kwa wale mnaoufahamu mji wa Moshi, Mkutano huo uliofanyika kwenye sehemu yanakoegeshewa magari yaendayo Mweka, Kirima na Pasua, kati ya jengo la Usalama barabarani mkoa na Stendi kubwa.

Akihutubia watu wachache waliokuwa wameketi kwenye mahema mawili ya kukodi, na wengine kadhaa waliokuwa wamesimama kwenye mabango ya matangazo stendi, Bw. Nape Nnauye alionekana kutumia muda mwingi kuwaaminisha wananchi kwamba yeye ndiye aliyebadili mwelekeo wa chama chake tangu ateuliwe kushika nafasi hiyo.

Pamoja na kusaidiwa na kada maarufu wa CCM mzee Kazidi, kudai kuwa na nyaraka za kichochezi za CHADEMA, bado mkutano ule haukufua dafu.

Nilioondoka eneo hili wakati akiendelea na ufafanuzi wa magamba.

Pengine hili litakuwa onyo kwa wafuasi wa magamba wanaojifanya hawaelewi wananchi anataka nini wakati kama huu.
 
Back
Top Bottom