Nape kutikisa Arusha/Moshi Jumamosi wiki hii

Nape kutikisa Arusha/Moshi Jumamosi wiki hii

magwanda ukiona hawaleti picha jua nape amefunika moshi.

nape amewakamata pabaya chadema. baba endelea kuwavuta hao chadema walizidi siasa chafu za kuiba nyaraka. na wewe endelea kuwaibia.
 
Sijui unailinganisha na nini au huelewi unachokisema? Kwa taarifa yako CCM ndiyo chama kinachoongoza dola ya Tanzania. Sasa unaitafuta CCM gani?
katiba mpya na ufisadi ni hoja au sera za ccm?
 
magwanda ukiona hawaleti picha jua nape amefunika moshi.nape amewakamata pabaya chadema. baba endelea kuwavuta hao chadema walizidi siasa chafu za kuiba nyaraka. na wewe endelea kuwaibia.
ndio maana nasema huwezi kuwa timamu ukawa ccm ! Hiki ni kielelezo cha wajinga wa ccm
 
Kama ni kweli haya mabango yalikuwepo, basi message delivered. Manake Nape hataki kuamini kwamba CCM sasa imechoka na kwamba watanzania hatutaki tena blabla tunataka mabadiliko waliyotuahidi. Watabaki kupendwa na kushangiliwa na wale masikini wa kusini mwa Tanzania. Yaani Mtwara na Lindi ndiyo mikoa masikini zaidi, na yenye elimu duni zaidi, lakini ndiyo iliyompokea vizuri zaidi Nape. Hapo ndo unapoamini kwamba kweli umasikini wa watanzania ndo mtaji wa CCM.

Ukimsikiliza Nape, utadhani ni yeye ndiye aliye na ufunguo wa mabadiliko ya CCM. Anaamini yu na umaarufu kuliko mtu mwingine yeyote CCM.
 
Sijui unailinganisha na nini au huelewi unachokisema? Kwa taarifa yako CCM ndiyo chama kinachoongoza dola ya Tanzania. Sasa unaitafuta CCM gani?
Hehehe, chama kinaongoza dola au dola inaongoza chama? Hivi CCM inaongoza dola gani wakati hakuna hata mmoja ndani ya CCM mwenye uwezo wa kumwajibisha yeyote ndani ya serikali? Ili muweze kuongoza dola fuateni ushauri wa kwenye signature yangu. Kwa sasa hamuongozi dola bali dola inawaongoza. Hapo mlipo hamna mamlaka hata ya kumkemea mkuu wa wilaya akivurunda, sasa mnaongoza dola gani? Nani yupo juu ya mwenzie, serikali au chama?
 
Binafsi niliwahi kumsikia Nape akihutubia mkutano wa hadhara. Nashawishika kusema wale wanaondamana naye kila mara waanze kutafuta daktari mzuri wa masikio maana siku si nyingi ngoma ya sikio itapasuka! Very unusual sound toka kwa huyu mtoto.
 
CCM Genge la wahuni wanaotumia madaraka kupora mali za nchi hii. Hakika ipo siku tutawatumbukiza CCM zealots wote pale ferry wazame wapotee kabisa ktk uso wa TZ hii
 
angemkaribisha babu , ndesa pesa angejaza watu mpk achanganyikiwe lol
 
Sijui unailinganisha na nini au huelewi unachokisema? Kwa taarifa yako CCM ndiyo chama kinachoongoza dola ya Tanzania. Sasa unaitafuta CCM gani?

Acha uongo bana dola ya Tz inaongozwa na CDM, wee huoni wakisema serikali ifanye hivi bac inado, ikisema CCM, hakuna utekelezaji wowote-hat ilani inayotekelezwa naona kama ni ile ya CDM kwa sasa. In short ccm mahtuti wa ICU so CDM ni kaimu chama kinachotawala now
 
Nani asie na uhakika kuwa nape ni mbumbumbu kama wajinga wengine !
 
kama si jf nadhani mimi binafsi ningekuwa simjui nape. Watu waliokuwepo wakiwemo makada wa ccm na uvccm mtu yeyote mwenye mic anaweza kuwakusanya.
 
Leo Nape alikuwa na mkutano wa hadhara katika eneo la stend ya mabasi, mkutano ulihudhuriwa na wachache.

Maneno haya ni sehemu ya hotuba yake:

CCCM oyee, baba wa kambo, ndimu, kujivua gamba, sumu ya nyoka, ccm baba mzazi, chama cha democrasia na maandamano, kibanzi, ngedere, dr feki, tatizo la bei ni mafuta si ccm, chama chetu, amani ya nchi yetu, mji wa moshi ni mchafu, anayeingia kitandani na bibi harusi nnatekeleza seri mume, wapambe watabaki mlangoni, hurusiwi kuchungulia nani ya mama, mshahara wa dr, mbunge analipwa mil 2.5 , katibu wetu ni mzee wa mipasho, mzee kazidi njoo wapashe, tanzania kuna chama kimoja tu, ni ccm, vingine ni makundi ya watu, baba wa kambo anamtaka mama yako, mimi ndio nimepewa mamlaka ya kuisema serikali, chama cha kambarage, sera ya chama chetu, tunasema ukweli, nyoka wa shaba,ikulu, vyama 18 vimesajiliwa, hakuna serikali mchanganyiko, nguvu ya umma

Alikuwa hana mtiririko mzuri katika kuwasilisha hotuba yake;
Sauti ilikuwa juu sana mithili ya anayehubiri.

Kama hali ni hivi, CCM kwisha habari yake.

Kaka na wewe hukuwa na kamera kama mimi? Hebu bandika picha ya waliofika kumsikia
 
Ukimsikiliza Nape, utadhani ni yeye ndiye aliye na ufunguo wa mabadiliko ya CCM. Anaamini yu na umaarufu kuliko mtu mwingine yeyote CCM.

Anataka kutuaminisha nini huyu nape?..hebu imajini Dr slaa afanyie mkutano stand itakuaje?..
 
Anataka kutuaminisha nini huyu nape?..hebu imajini Dr slaa afanyie mkutano stand itakuaje?..

Walichagua kauwanja kale wakijua fika kuwa hakuna atakayekuja isipokuwa wauza karanga na wanaosubiri usafiri. Wangeenda Memorial ama Mashujaa ama Manyema ingebidi wawe na malori.
 
Dah, mbona sion sehemu yoyote ya kipigo alichopewa?
Yaelekea mkuu wewe ni mwandish mzuri sana wa magazet ya udaku
unafikir mnaona basi? mngekuwa mnaona tusingekuwa gizani sasa hivi..angalia hapo nilipopigia mistari
Mh. wa propaganda leo kwa kutana na kimbembe baada ya wakazi wa Moshi kumpokea na mabango ya kejeli juu ya CCM kwa mfano bango moja lliandikwa "CCM NI YA NYERERE IMEZEEKA""HATUTAKI KUVUA GAMBA TUNATAKA UMEME"
 
Back
Top Bottom