Nape kutikisa Arusha/Moshi Jumamosi wiki hii

Jana alipokuwa ana hutubia watu maeneo ya stendi hapa Moshi mjini alitoa kauli zenye maudhi ndani yake na labda bila kujua kuwa kauli zake zina ukakasi alizidi kukandamiza lawama kwa vyama vipinzani huku akishindwa kuona ukweli na uhalisia wa mambo.

Nape alisema Tanzania kuna zaidi ya vyama 17 vya siasa lakini kuna chama kimoja tu kilicho beba matumaini ya watanzania. Chama hicho ni CCM na vyama vingine ni vyama vya WALALAMIKAJI, lakini akiwa anasema hayo mji wa Moshi hasa karibu na eneo alilo kuwa anahutubia palikuwa pametawalia na kelele za majenerata, hapa ndio nashindwa kumuelewa Nape! Hivi wana JF wanao lalamikia umeme nao ni wa vyama pinzani tu! Mbona wabunge wa CCM Wameungana na upinzani kukwamisha bajeti ya Ngeleja? Na wabunge wale nao atawaitaje maana nao walilalamika.

Wizi ulio ibuliwa na vyama pinzani hasa CDM nao ulikuwa ni aina ya malalamiko ambayo Nape anataka kuaminisha kuwa Cdm ni chama cha walalamikaji? Mbona Kina Sita nao ndani ya CCM wanalalamika kuwa kuna watu wanaifilisi nchi kwa biashara zao za kitapeli, je nao ni aina ya walalamikaji wa CCJ na sio CCM?!
Mbona JK nae alisha wahi kulalamika kuwa CDM wanataka kumng'oa madarakani kwa maandamano, vipi nae ni aina ya viongozi wa vyama vya ulalamikaji?!

Una mapungufu ya kimantiki Nape. Rudi darasani ukaketi upya.

Hawa jamaa hawajui nini cha kutetea lakini kila anaye kuja anadai maslahi ya chama na sio Watanzania, hebu tujiulize hawa ambao hawapo CCM si Watz au ni kwamba bado tuna wajinga ambao hawajui kwa sasa hatuhitaji chama tunaitaji maslahi ya nchi, je CDM au chama kingine hakina haki ya kuchukua nchi. Ukweli utabaki pale pale kuwa hakuna chama chenye haki miliki ya nchii hii. Kama ni wananchi wote walitumika katika kufanikisha nchi kuwa pale ilipo, chama tawala inajivunia huku ikumbatia mafisadi wanayofilisi nchi hii kutuletea janga la umeme, njaa na mengineyo hii njama za chama tawala kuwafanya watz wafikiri umeme na njaa. wongo mtupu, maandamano si vurugu ila ni kuonyesha kuwa hali ya wanaolipa kodi bado haisaidii, kumfanya awe huru kila siku kodi kibao zisizo na msingi wowote wa maendeleo ya nchi bali kuwanufaisha hao mafisadi tu. CCM wanaweza kujisifia kitu kimoja tu, kurudisha nchi nyuma miaka 60, miaka kumi nyuma zaidi kabla ya uhuru, hii siasa uchwara wanajitahidi kusifia miaka 50 ya uhuru, hawa jamaa ni matahira wasio na tiba muafaka.
 
nape hana kitu cha maana zaidi ya kulinda mshahara wake tu,kwa nini alikuwa anataka kujitoa ccm na kwenda ccj? Anajua kabisa kuwa ana pretend kuwa ndani ya ccm

Anachofanya nape ni matusi tu kwa watanzania badala ya kueleza sera za chama chake na mikakati ya kuisaidia serikali kuondoa kero kwa wananchi. Hii ya kuvinyooshea kidole chake vyama vya upinzania atajua madhara yake baadaye, maana sasa hivi hata haoni ishara za nyakati zinavyoashiria. Mtanzania wa leo si yule wa jana wa zidumu fikra.
 
Hawa jamaa hawajui nini cha kutetea lakini kila anaye kuja anadai maslahi ya chama na sio Watanzania, hebu tujiulize hawa ambao hawapo CCM si Watz au ni kwamba bado tuna wajinga ambao hawajui kwa sasa hatuhitaji chama tunaitaji maslahi ya nchi, je CDM au chama kingine hakina haki ya kuchukua nchi. Ukweli utabaki pale pale kuwa hakuna chama chenye haki miliki ya nchii hii. Kama ni wananchi wote walitumika katika kufanikisha nchi kuwa pale ilipo, chama tawala inajivunia huku ikumbatia mafisadi wanayofilisi nchi hii kutuletea janga la umeme, njaa na mengineyo hii njama za chama tawala kuwafanya watz wafikiri umeme na njaa. wongo mtupu, maandamano si vurugu ila ni kuonyesha kuwa hali ya wanaolipa kodi bado haisaidii, kumfanya awe huru kila siku kodi kibao zisizo na msingi wowote wa maendeleo ya nchi bali kuwanufaisha hao mafisadi tu. CCM wanaweza kujisifia kitu kimoja tu, kurudisha nchi nyuma miaka 60, miaka kumi nyuma zaidi kabla ya uhuru, hii siasa uchwara wanajitahidi kusifia miaka 50 ya uhuru, hawa jamaa ni matahira wasio na tiba muafaka.

Umenena iliyo kweli, kwani wanachohangaikia ni maslani ya chama na viongozi badala ya maslahi ya taifa na wananchi wake
 
Mzito Kabwela nilijaribu kujizuia vya kutosha kuonyesha hisia zangu maana enzi zetu tuliisoma CCM kama sehemu ya Sylabus na tukaifanyia mtihani hasa. Ninayoifahamu kiitikadi siyo ninayoyaona na kuyasikia kutoka kwa hao waliorithi chama, mbaya zaidi sio hawa vijana, a a bali ni walewale waliosoma na mimi chama hikishuleni na leo hii wanahubiri na kutenda kinyume na mahubiri yao.
 
Back
Top Bottom