Nape: Kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na si dalili ya udhaifu

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,576
2,000


Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Nnauye amesema kwa mujibu wa nyaraka za chama hicho tawala, kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na si dalili ya udhaifu.

Nape ameyasema hayo leo Alhamisi Aprili 15, 2021 wakati akichangia makadirio ya mapato na matumizi ya ofisi ya waziri mkuu na taasisi zake kwa mwaka 2021/22.

Amesema Rais wa awamu ya sita, Samia Suluhu Hassan ameanza vizuri na kutaka wananchi kumpa ushirikiano, “mzee Mwinyi (Ali Hassan- rais wa awamu ya pili) alituambia kila zama na kitabu chake.”

Amebainisha kuwa wamekuwa na vitabu vitano akirejea marais watano Julius Nyerere, Mwinyi, Benjamin Mkapa, Jakaya Kikwete na John Magufuli akisisitiza kuwa wito wake kwa viongozi, wabunge wenzake, wanachama wa CCM pamoja na Watanzania kumsaidia Samia kwa kumuunga mkono aandike kitabu cha awamu ya sita.

“Tusigombane bila sababu Tanzania ni yetu sote tumsaidie mama naye aandike kitabu chake tusimshike mkono kumwandikia kitabu tumwache aandike kitabu chake na ndugu zangu legacy (alama) haitetewi inajitetea yenyewe.”

“Hasa ile inayofanywa na mtu kama Magufuli itajitetea na kujisimamia miaka labda kama mtu ana mashaka na legacy yake lakini kama hamna mashaka na legacy yake itasikilizwa, itaongewa sisi watoto wajukuu na vitukuu kwa sababu haya waliyoyafanya watayakuta,” amesema.

Amesema sasa hivi hawana sababu ya kugombana na hawana sababu ya kutoana macho.

“Mimi nimekuwa kiongozi katika chama, nimesimamia idara ya maktaba na nyaraka duniani hakuna chama bora kilicho document vya kutosha CCM ni karibia namba moja kwa kila kitu,” amesema.

Amesema kwenye nyaraka zao wamesema kukosoa na kujikosoa ni silaha ya mapinduzi na kujiimarisha na sio dalili ya udhaifu.


Chanzo: Mwananchi
 

citizensindevelopment18

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
860
500
Tunaelekea kuelewa yupi ni yupi yuleeee. Sidhani kuna mstaarabu anayekataa kukosoa kwa lengo la kusonga mbele. Issue ni namna ya ukosoaji na wakati wake. Mlikuwepo kwenye chama mlikwama wapi kukosoa?
 

Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
21,508
2,000
Makamba kisha Nape.

Hii inamaanisha ndani ya ccm kuna watu hawatoi au wamedhamiria kutotoa support kwa rais wa sasa.

Kama hivi hiyo inamaanisha ana watu wachache wa kuwaamini ndani ya chama chake mwenyewe, siyo dalili nzuri.
 

citizensindevelopment18

JF-Expert Member
Apr 1, 2020
860
500
Key point to note, "KILA ZAMA NA KITABU CHAKEEEEEEE"
Sawa kabisa kuwa kila zama na kitabu chake ila tambua kuwa kitabu hicho kwa CCM ni ilani ya uchaguzi. Hakuna rais anayekuja na kitabu kutoka kwake au kanisani/msikitini. Kinachotofautiana ni utekelezaji wa ilani. Kumbukumbu zinaonyesha awamu nyingine zilitekeleza kwa asilimia 35 tu.
 

Stuxnet

JF-Expert Member
Feb 12, 2011
4,476
2,000
Tunaelekea kuelewa yupi ni yupi yuleeee. Sidhani kuna mstaarabu anayekataa kukosoa kwa lengo la kusonga mbele. Issue ni namna ya ukosoaji na wakati wake. Mlikuwepo kwenye chama mlikwama wapi kukosoa?
citizensindevelopment18 usijifanye uko nje ya Tanzania. Magufuli alikuwa anaua, anateka, na alikuwa anaweza kukutafutia kesi isiyo na dhamana kwa issue ya kumkosoa tu.

Kwa hiyo ulidhani akina Nape hawajui kilichompata Ben Saanane, Tundu Lissu na RomaMkatoliki?
 

SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
2,717
2,000
Legacy ya Magofool inatetewa na CHATO GANG.

Bashiru na Doto mumuache mama afanye kazi mbona kawapa vyeo? Alikuwa na uwezo wa kuwatumbua kabisa ili mje huku mtaani kujiajiri nakunywa Double Kick kama sisi wanyonge, ila kwa busara zake amewaacha.
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
39,902
2,000
Tunaelekea kuelewa yupi ni yupi yuleeee. Sidhani kuna mstaarabu anayekataa kukosoa kwa lengo la kusonga mbele. Issue ni namna ya ukosoaji na wakati wake. Mlikuwepo kwenye chama mlikwama wapi kukosoa?
Kama mtu alikuwa dhalimu, na kufanya mauji, kuwabambikia kesi, kuhujumu shughuli zao wote wanamkosoa, unataka mbwembwe gani za kumkosoa? Anayetawala kidhalimu, anakosolewa bila kubembelezwa.
 

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
548
1,000
Mbunge wa Mtama kupitia CCM, Nape Nnauye, amesema anajisikia fahari kushiriki ndani ya chama na nje kwenye mchakato wa kumpata na hatimaye kuwa Rais, hayati John Magufuli kwani amefanya kazi nzuri na alama nyingi ambazo hazitasaulika na dunia inajadili mufunzo aliyoacha. Nape amesema anamshkuru Mungu kwa maisha ya Dkt. Magufuli kwa nchi ya Tanzania

Pia Nape amekishukuru chama cha mapinduzi kwa kusimamia vizuri mchakato wa mpito kwa Rais Magufuli kwenda kwa mama Samia Suluhu na kwake imethibitisha kwamba CCM bado ni chama bora kwa nchi, Afrika na dunia.Pia Nape ameongelea Chama kukosoa na kujikosoa kuwa ni silaha ya Mapinduzi na kujiimarisha wala si dalili ya udhaifu
-
Nape amesema “Tusigombane bila sababu, Tanzania ni yetu sote, tumsaidie Mama naye aandike kitabu chake. Tusimshike mkono kumwandikia kitabu tumwache aandike kitabu chake na ndugu zangu 'legacy' haitetewi inajitetea yenyewe”
-
Amesema 'Legacy' iliyofanywa na Hayati Dkt. Magufuli itajitetea na kujisimamia miaka wajukuu na vitukuu watayakuta hivyo kwa sasa hakuna sababu ya kugombana wala kutoana macho.
 

santesandy

JF-Expert Member
Apr 23, 2012
1,612
2,000
Kaongea point tupuuuuuu, hawa ndo wachache tuliobakiwa nao wanaojitambua.
Angekua anajitambua angejirekodi njia nzima akienda kuungama madhambi?! Mashujaa ni wale waliojitoa nafsi zao kutimiza jukumu hilo la kukosoa, hadi wengine kina mdude wanasota huko! Huyu vuvuzela tu, anatamani wizara ya Bashungua!
 

FUSO

JF-Expert Member
Nov 19, 2010
22,562
2,000
Chama gani kimesimamia transition? Nape acha uongo - kama si Mkuu wa Majeshi sasa hivi tungekuwa tunaongea kichina.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom